Ningemweka Rais Magufuli kwenye list ya wazalendo kama angefanya haya

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
10,288
2,000
1. Angewaomba wana CCM wote hasa wabunge watubu kwa kukiingiza taifa hasara toka tupate Uhuru.

2. Kwa niaba ya serikali yake ya sasa na serikali zilizopita angewaomba watanzania msamaha kama ishara ya kuanza upya safari.

3. Angewashukuru na kuwapongeza wapinzani kwa kazi nzuri walitofanya kupigania raslimali zetu.

4. Angepiga marufuku wabunge wa CCM kushabikia mashauri ya kijinga bungeni.

5. Angemwonya spika kuwafukuza wabunge wa upinzani bila sababu hasa pale wanapoibua tuhuma zinazo lenga kulinda maslahi ya Tanzania.

6. Aruhusu mchakato Katiba mpya sawa sawa na maoni ya wananchi siyo ile ya ccm.Sasa Jana hajasema chochote juu ya wabunge wa chama chake ambao ndio chanzo cha haya yote.
 
MAGACHA

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,042
2,000
Kwanza,Rais magufuli anasema hii ni vita ya kiuchumi,anasema tunaibiwa sana,na anaongea kwa hisia kuonyesha anavyokerwa na yanayofanyika,
Pili ripoti ya pili ya madini inasema,accacia ni kampuni hewa,

Mimi nilitegemea yafuatayo baada ya ripoti ya pili kuwasilishwa ili kudhihirisha vita halisi ya uchumi,kuliko kuchamba wapinzani

a)kuanzia muda huu,shughuli zote za migodi zisimame,vyombo vya ulinzi na usalama simamia hili kuanzia sasa

b)kampuni iliyotajwa,accacia,naamuru wanasheria kuwapeleka mahakamani,na hapo walipo wasiendelee na shughuli yoyote ya kuchimba madini na kusafirisha

Hapo ningeelewa kuwa hii kweli ni vita lakini tusifanywe wajinga kwa hili kwa sababu zifuatazo

Mpaka sasa shughuli zote za uchimbaji na usafirishaji wa madini unaendelea,sasa kama sio ujinga vita iko wapi hapa

Tusitake kuwaaminisha watanzania kuwa tunapigana vita ya uchumi kwa kuzuia makanikia halafu usiku na mchana dhahabu zinasafirisha mpaka Leo tar 14/June dhahabu inasombwa tena kwa kasi, tusifanywe wajinga hakuna cha vita,hizi ni mbwembwe za kujihami kwa wapinzani

Nashangaa mpaka muda huu kampuni hewa inaendelea kuchimba madini na kusafirisha
 
Lizarazu

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
6,151
2,000
Alishakwambia kwamba atalinda chama kwa gharama yoyote ile, sasa wewe huoni kwamba endapo atafanya moja wapo ya hayo uliyotaja atakuwa msaliti wa chama?

Yaani awashukuru wapinzani kabisa!!! ? amerogwa.
 
HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,065
2,000
Tena kampuni hewa na iliyotuibia inaombwa itulipe kwanza halafu ndio tukae nayo meza moja kujadiliana maisha mapya....
Kama hili kamapuni ni la kiwizi mezanmoja ya nini na mwizi wa mali yetu?
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
10,288
2,000
Tena kampuni hewa na iliyotuibia inaombwa itulipe kwanza halafu ndio tukae nayo meza moja kujadiliana maisha mapya....
Kama hili kamapuni ni la kiwizi mezanmoja ya nini na mwizi wa mali yetu?
watalipwaje bila mahakama, labda kama wanaomba rushwa..
 
singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
4,242
2,000
Mi mwenyewe nimeshangaa rais anapeleka chuki upinzani wakati ndo wameibua hichi anachokifanya. Kwa hili rais anagawa raia bila kujijua, tena ingebidi uwape tuzo wale wabunge waliokomaa mpaka kutimuliwa, kuchafuliwa na kutukanwa kwa kuipigania nchi. Rais chama chako kimejaa wagonga meza. Hebu tupe mfano wa mbunge wa chama chako alieongea juu ya hili unalolifanya
 
mungwabi

Member
Apr 17, 2015
91
125
1. Angewaomba wana CCM wote hasa wabunge watubu kwa kukiingiza taifa hasara toka tupate Uhuru.

2. Kwa niaba ya serikali yake ya sasa na serikali zilizopita angewaomba watanzania msamaha kama ishara ya kuanza upya safari.

3. Angewashukuru na kuwapongeza wapinzani kwa kazi nzuri walitofanya kupigania raslimali zetu.

4. Angepiga marufuku wabunge wa CCM kushabikia mashauri ya kijinga bungeni.

5. Angemwonya spika kuwafukuza wabunge wa upinzani bila sababu hasa pale wanapoibua tuhuma zinazo lenga kulinda maslahi ya Tanzania.

Sasa Jana hajasema chochote juu ya wabunge wa chama chake ambao ndio chanzo cha haya yote.
 
mungwabi

Member
Apr 17, 2015
91
125
TE="mungwabi, post: 21592579, member: 285118"][/QUOTE]
Hayo uliyoyasema ni sawa. Lakini hata sasa ni mzalendo sana. Naomba utendee haki.
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
5,320
2,000
Kwanza,Rais magufuli anasema hii ni vita ya kiuchumi,anasema tunaibiwa sana,na anaongea kwa hisia kuonyesha anavyokerwa na yanayofanyika,
Pili ripoti ya pili ya madini inasema,accacia ni kampuni hewa,

Mimi nilitegemea yafuatayo baada ya ripoti ya pili kuwasilishwa ili kudhihirisha vita halisi ya uchumi,kuliko kuchamba wapinzani

a)kuanzia muda huu,shughuli zote za migodi zisimame,vyombo vya ulinzi na usalama simamia hili kuanzia sasa

b)kampuni iliyotajwa,accacia,naamuru wanasheria kuwapeleka mahakamani,na hapo walipo wasiendelee na shughuli yoyote ya kuchimba madini na kusafirisha

Hapo ningeelewa kuwa hii kweli ni vita lakini tusifanywe wajinga kwa hili kwa sababu zifuatazo

Mpaka sasa shughuli zote za uchimbaji na usafirishaji wa madini unaendelea,sasa kama sio ujinga vita iko wapi hapa

Tusitake kuwaaminisha watanzania kuwa tunapigana vita ya uchumi kwa kuzuia makanikia halafu usiku na mchana dhahabu zinasafirisha mpaka Leo tar 14/June dhahabu inasombwa tena kwa kasi, tusifanywe wajinga hakuna cha vita,hizi ni mbwembwe za kujihami kwa wapinzani

Nashangaa mpaka muda huu kampuni hewa inaendelea kuchimba madini na kusafirisha
Wana hera zetu bana Japo ni uzembe wa Serikali ya CCM siyo kwamba tuna pinga jitihada za Rais JPM serikali ya CCM ndiyo imetufikisha hapa ina sikitisha sana
 
ngalakeri

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
1,289
2,000
Pamoja na uzi mzuri na uchaguzi mzuri uliofanya wewe kwao wale ni mchochezi, si mzalendo, mpinga maendeleo, umehongwa, ingekuwa vitani ungepigwa risasi n.k
 
Ohooo

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
807
1,000
Afu kuna mijitu yenyewe ni kuitikia tu kila anachosema rais. Hata ndugai anashangaa eti alikuwa hajui wakati yupo bungeni kwa miaka 17 sasa
 
m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
980
1,000
MNAZUNGUMZIA UPINZANI HUU WA AKINA LOWASA, SUMAYE NA MBOWE? AU UPINZANI UPI MNAOJITANABAHISHA NAO HAPA KUWA UMEIBUA HOJA ZA KUIBIWA RASLIMALI ZETU?

HAO MNAOWAONA WATU MUHIMU SANA KATIKA VITA YA KUPIGANIA RASLIMALI ZETU ZISIIBIWE NDO WEZI WENYEWE NA MATAPELI AMBAO KWA VITENDO TU WAMEJIDHIHIRI PASI MASHAKA. MBOWE SI NDO YULE ALIYETAKA KUDHULUMU N.H.C KWA KUJIFANYA NI MBIA AU SIYO HUYO?

JAMANI TUWE SERIOUS NA UCHAMBUZI WA MAMBO. MAMBO YA HIVYO MUYATENGANISHE NA YA MSINGI.
 
Nyalutubwi

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
573
225
Yote haya ni matokeo ya kuwa na chama tawala kinachoongoza nchi kwa njia za ghiriba.Ni hizi pesa za wizi wa raslimali za Taifa ndizo zinazotumika kununulia uongozi.Hakuna jipya bali mwendelezo wa taratibu ovu za Chama.
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,172
2,000
MNAZUNGUMZIA UPINZANI HUU WA AKINA LOWASA, SUMAYE NA MBOWE? AU UPINZANI UPI MNAOJITANABAHISHA NAO HAPA KUWA UMEIBUA HOJA ZA KUIBIWA RASLIMALI ZETU?

HAO MNAOWAONA WATU MUHIMU SANA KATIKA VITA YA KUPIGANIA RASLIMALI ZETU ZISIIBIWE NDO WEZI WENYEWE NA MATAPELI AMBAO KWA VITENDO TU WAMEJIDHIHIRI PASI MASHAKA. MBOWE SI NDO YULE ALIYETAKA KUDHULUMU N.H.C KWA KUJIFANYA NI MBIA AU SIYO HUYO?

JAMANI TUWE SERIOUS NA UCHAMBUZI WA MAMBO. MAMBO YA HIVYO MUYATENGANISHE NA YA MSINGI.
Pole pole kijana! Hebu wasikie vijana wenzako wanaotendea haki ujana wao!

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom