Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 20,598
- 44,425
Huyu dada ni mpangaji mwenzangu hapa Kunecity (DSM). Hii ishu ilianza wiki kadhaa nyuma nilimskia mpanga mwenzangu akiongea na ndugu zake wa kaskazini uko nadhani ni moshi. Alikua anawashawishi kutoa kiasi kadhaa si chini ya laki 5 alianza na mwanamke akamshawishi kwa siku kadhaa uyo bidada akaingia kingi sasa ikabaki kumshawishi baba ake nae ajiunge na iyo biashara. Kiukweli mi sikujua ni biashara gani na wala sikutaka kufatilia nikidhani ni mitikasi ya mjini tu hapa na ukizingatia imekaa kifamilia familia basi ata sikutaka kujua.
Sasa jana jioni ndo nikajua bila hata kutarajia kumbee bwana ni walewale ndugu zetu wa lete watu wako wawili na wao wakileta wawili unapata commision ya million kadhaa na blah blah zao zile. Ayo yote nimeyajua alipokua anamshawishi rafiki yake nae aingie kingi daah nikamsikitia bidada wa watu anamwambia unamjua tajiri namba 2 duniani nae alipitia huku huku aliacha shule akaanza izi biashara mpaka akawa tajiri. Jaman jaman hawa watu wanatumia dawa gani kushawishi watu yani ukimskia uyu dada utadhani yeye ndie mwanzilishi wa hii kampuni X. Anazidi kumshawishi ati atapata offer kibao kutembelea nchi mbalimbali na kulala hoteli za nyota 3 hadi 5 pale akifanya kazi yake vyema na izo offer sio lazima apate yeye zote anaweza kuamua tu nani ambless akalale hoteli aliyoambiwa yeye alale na anamchagua mtu wake yeyote tu wa karibu.
Tatizo sijazoeana na uyu mdada ni salamu tu na kupita ivi walau ningeshauri chochote ila ndo ivo kazama mazima kwa hiyo kampuni kubwa duniani kwa usambazaji wa vitu mbalimbali na kama mjuavyo maisha ya kimjini mjini haya kuingilia mambo ya watu nikaona bora nije kuwapa story wanaJF.
Mimi hawa jamaa nilishawahi kwenda hadi uko ofisini kwako ilikua ni moroco nadhani mwaka juzi wana story nyingi za kufikilika. Nakumbuka niliwatafuta baada ya kupata mawasiliano yao fb nikaambiwa niende uko ofisini kwao basi bna tukaingizwa kwenye kiukumbi hapo hapo ofisini kwao kwasababu tulikua wengi kidogo. Wakatoa ushawishi waoo na shuhuda za uongo na ukweli, mwisho nikaja kugundua kua mule ndani walengwa tupo wachache ila wengi ni wenzao waliojifanya nao ni mala ya kwanza kwenda pale ili ukifika wakati wa kutoa pesa wale wenzao waanze kutoa kwa hamasa na sie walengwa tuhamasike tutoe chap aisee niliwastukia pale nikayeya walikua wanapiga simu mpaka walichoka sasa.
Bidada kauvaa ni suala la muda tu.