Ningekuwa Speaker (Tiba ya Verbal Diarrhorea)

Sun Tzu

Member
Mar 2, 2010
78
23
Ningekuwa Speaker ningeanzisha "Naughty Corner" na ili kuwapa wananchi fursa ya kutofautisha kati ya "Bunge Naught Corner" ningeshauri ijengwe mbali kutoka "Mirembe".

Kanuni za huko ni kama ifuatavyo:

Mbunge akishindikana kwenye Ukumbi wa kawaida wa Bunge kwa kutumia kanuni za "Naughty Corner" ambazo ni kama ifuatavyo:

Mbunge atapangiwa masaa mawili ya kwenda Naughty Corner akiingia huko kutakuwa na "Paid Live TV Coverage" kwenye Digital and Cable na Jimboni kwa Mbunge anapotoka.

Kanuni namba 1: Mbunge aliatofautishwe yeye na Chama Chake na Watanzania Wengine itabidi atoe nguo zote kwanza.

Kanuni namba 2: Mbunge ataruhusiwa kuanza kujitukana akipenda atatukana kila kiungo au umbile la mwili wake.

Kanuni namba 3: Mbunge ataruhusiwa kumchagua mbunge yeyote anayetaka kumchambua na kumtukana bila kuomba mwongozo wa Speaker. Lengo ni kumaliza ku-purge au kumaliza verbal Diarrhoea.

Kanuni namba 4: Mbunge ataruhusiwa kukitunkana Chama Chake

Kanuni namba 5: Mbunge ataruhusiwa kuitukana hadharani familia yake na wazazi wake akipenda hii inaruhusiwa kwenye Naughty Corner

Kanuni namba 6: Mbunge anaruhusiwa kuwatukana wapiga kura wa jimbo lake au wale waliompa nafasi ya Viti Maalumu na kutumia fursa hiyo kuwaomba wamchaguwe tena.

Kanuni namba 7: Mbunge ataruhusiwa kuvaa nguo zake na kuwaomba msamaha watanzania kama akipenda.

Kanuni namba 8: Mbunge anauruhusiwa kuomba aongezewa muda kukaa Naughty Corner kama hasira na matusi yake hayajaisha kabla ya Kurudi tena Jengoni. "Bungeni"

Mapato yatakayopatikana kutoka kwenye Naughty Corner yatasaidia kuiendesha Kamati ya Bunge ya Uongozi na Maadili, kwani Hii Live TV itakuwa moja ya sehemu mihimu ya kuliingizia Bunge kipato.


Na lile Bunge tulilolichaguwa la Kutunga Sheria na Kuisimamia Serikali katika mambo yake kwa niaba ya Wananchi litapata fursa ya kufanya kazi yake.:music:
 
Back
Top Bottom