Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA....

Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA....

Ushaur wa maana sana huu lakini hawakawii kukwambia umekengeuka...
 
Huwa naogopa sana sana kuweka elimu yangu kando na kuongozwa na hisia au mahaba niue...ni ujinga
 
Kwasasa, na tangu kuzaliwa kwangu, sina chama.
Kutokana na jinsi ninavyofuatilia comment zako wewe ni mwanasheria/wakili msomi inafaa sana uwe mwanachama wa chadema, au mojawapo wa vyama vya upinzani ili uwe huru kusaidia wanyonge wanaonyanyasika ndani ya taifa letu.

Lakini hilo la kumshauri mbowe asigombee tena inatakiwa ufafanue kwani ni tatizo gani ambalo anaweza kulisababisha endapo atagombea na kushinda uwenyekiti, na kwako binafsi ni sababu ipi unayoiona ambayo itapelekea chama kushindwa kustawi zaidi chini ya Mbowe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA ningefanya mambo mbalimbali. Kwanza, ningetambua kuwa CHADEMA ni chama 'chenye wenyewe'. Yaani, katika CHADEMA kuna waanzailishi wake na ndiyo wenye chama chao. Hivyobasi, ningekuwa na wajibu wa kulijua hilo; kuwatii na kuwaheshimu wenyechama chao na kuwa na mipaka katika kujadili na kutoa maoni yangu.

Pili, ningejiuliza, kwa kuwa kwangu CHADEMA nimechangia/nimefanya nini la kukumbukwa? Yaani, nimechangia kipi hasa katika kuifikisha CHADEMA ilipo sasa. Si kinyume chake, yaani, nimepata nini tangu nikiwa CHADEMA hadi sasa. Utii wangu na kupambana kwangu kama mwanachama wa CHADEMA vingejikita katika kipimo cha mchango wangu.

Tatu, ningemsifu Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa mchango wake, hasa wa kiuongozi, hata kuifikisha CHADEMA ilipo. Ningemsifu kwa kushiriki tangu kuanzishwa kwa CHADEMA chini ya Mzee Edwin Mtei hadi kupata Wabunge na hatimaye kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Nimgemsifu katika falsafa zake za 'kiuanaharakati' zilizokiinua chama. Ningewaomba wanachama wenzangu tumuandalie zawadi nzuri Mwenyekiti wetu kumpongeza kwa mafanikio yaliyofikiwa tangu awe Mwenyekiti. Mwisho mwishoni, ningewaomba wanachama wenzangu tumshauri Mwenyekiti Mbowe asigombee tena Uenyekiti mwakani. Tungemfanyia sherehe baab-kubwa!

Nne, ningejenga hoja na wenzangu ya kuwa makini katika kupokea wanachama toka vyama vingine ambao huhamia hasa wakati wa uchaguzi mkuu. Hawa huhamia kimaslahi kuliko kupendezwa na Ilani, Itikadi na Falsafa za chama. Baada ya uchaguzi, hata kama wameshinda katika nafasi wanazoaminiwa, huwa na ukakasi katika kusema na kutenda kwao.

Tano, ningewashauri wanachama wenzangu na viongozi wetu wa CHADEMA KUJIKITA KATIKA MAMBO MAWILI MAKUBWA. La kwanza ni ujenzi wa Ofisi kuanzia Makao Makuu hadi huko kwenye ofisi za Wilaya. La pili, ni kuendelea kujitangaza, hata kama ni kimyakimya, hasa katika sehemu za vitongoji na vijiji. Baadaye, tujikite ngazi kwa ngazi kwa uchaguzi wa S/Mitaa, Udiwani na Ubunge.

Hakika, ningekuwa mwanachama wa CHADEMA, ningeyafanya hayo.
Kijana mzuri kabisa. Jambo moja zuri ni kumuacha Mhe. Mbowe akaandaa mrithi wake ili wakati Magufuli anaondoka madarakani ( 2025) na kwenye uongozi wa chama chake naye aondoke. Watu wapya waingie kwenye shughuli za kisiasa.
 
CCM ndiyo hahitaji hata kuumizwa kichwa kujua kuwa ni mali ya nani.
 
Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA ningefanya mambo mbalimbali. Kwanza, ningetambua kuwa CHADEMA ni chama 'chenye wenyewe'. Yaani, katika CHADEMA kuna waanzailishi wake na ndiyo wenye chama chao. Hivyobasi, ningekuwa na wajibu wa kulijua hilo; kuwatii na kuwaheshimu wenyechama chao na kuwa na mipaka katika kujadili na kutoa maoni yangu.

Pili, ningejiuliza, kwa kuwa kwangu CHADEMA nimechangia/nimefanya nini la kukumbukwa? Yaani, nimechangia kipi hasa katika kuifikisha CHADEMA ilipo sasa. Si kinyume chake, yaani, nimepata nini tangu nikiwa CHADEMA hadi sasa. Utii wangu na kupambana kwangu kama mwanachama wa CHADEMA vingejikita katika kipimo cha mchango wangu.

Tatu, ningemsifu Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa mchango wake, hasa wa kiuongozi, hata kuifikisha CHADEMA ilipo. Ningemsifu kwa kushiriki tangu kuanzishwa kwa CHADEMA chini ya Mzee Edwin Mtei hadi kupata Wabunge na hatimaye kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Nimgemsifu katika falsafa zake za 'kiuanaharakati' zilizokiinua chama. Ningewaomba wanachama wenzangu tumuandalie zawadi nzuri Mwenyekiti wetu kumpongeza kwa mafanikio yaliyofikiwa tangu awe Mwenyekiti. Mwisho mwishoni, ningewaomba wanachama wenzangu tumshauri Mwenyekiti Mbowe asigombee tena Uenyekiti mwakani. Tungemfanyia sherehe baab-kubwa!

Nne, ningejenga hoja na wenzangu ya kuwa makini katika kupokea wanachama toka vyama vingine ambao huhamia hasa wakati wa uchaguzi mkuu. Hawa huhamia kimaslahi kuliko kupendezwa na Ilani, Itikadi na Falsafa za chama. Baada ya uchaguzi, hata kama wameshinda katika nafasi wanazoaminiwa, huwa na ukakasi katika kusema na kutenda kwao.

Tano, ningewashauri wanachama wenzangu na viongozi wetu wa CHADEMA KUJIKITA KATIKA MAMBO MAWILI MAKUBWA. La kwanza ni ujenzi wa Ofisi kuanzia Makao Makuu hadi huko kwenye ofisi za Wilaya. La pili, ni kuendelea kujitangaza, hata kama ni kimyakimya, hasa katika sehemu za vitongoji na vijiji. Baadaye, tujikite ngazi kwa ngazi kwa uchaguzi wa S/Mitaa, Udiwani na Ubunge.

Hakika, ningekuwa mwanachama wa CHADEMA, ningeyafanya hayo.
Kwa point zipi kwamba asigombee tena? Wewe ndio wale wale wa CCM wanaolalamika kuwa Mbowe ndie anaeiua CHADEMA na hawamtaki
 
andiko lako lina ukakasi , hao wenye chadema unaowataja kwenye namba 1 yako ni akina nani ?

Jibu rahisi ni hili.
Kampuni binafsi inapoingia sokoni na watu kuweka mitaji yao (wanachama), kampuni inakuwa ya wenye hisa (wananchama/wawekezaji). Sasa tatizo hapo liko wapi!
'Rebuttal' ya hoja zake zote ni rahisi sana.
 
Back
Top Bottom