Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA ningefanya mambo mbalimbali. Kwanza, ningetambua kuwa CHADEMA ni chama 'chenye wenyewe'. Yaani, katika CHADEMA kuna waanzilishi wake na ndiyo wenye chama chao. Hivyobasi, ningekuwa na wajibu wa kulijua hilo; kuwatii na kuwaheshimu wenyechama chao na kuwa na mipaka katika kujadili na kutoa maoni yangu.
Pili, ningejiuliza, kwa kuwa kwangu CHADEMA nimechangia/nimefanya nini la kukumbukwa? Yaani, nimechangia kipi hasa katika kuifikisha CHADEMA ilipo sasa. Si kinyume chake, yaani, nimepata nini tangu nikiwa CHADEMA hadi sasa. Utii wangu na kupambana kwangu kama mwanachama wa CHADEMA vingejikita katika kipimo cha mchango wangu.
Tatu, ningemsifu Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa mchango wake, hasa wa kiuongozi, hata kuifikisha CHADEMA ilipo. Ningemsifu kwa kushiriki tangu kuanzishwa kwa CHADEMA chini ya Mzee Edwin Mtei hadi kupata Wabunge na hatimaye kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.
Nimgemsifu katika falsafa zake za 'kiuanaharakati' zilizokiinua chama. Ningewaomba wanachama wenzangu tumuandalie zawadi nzuri Mwenyekiti wetu kumpongeza kwa mafanikio yaliyofikiwa tangu awe Mwenyekiti. Mwisho mwishoni, ningewaomba wanachama wenzangu tumshauri Mwenyekiti Mbowe asigombee tena Uenyekiti mwakani. Tungemfanyia sherehe baab-kubwa!
Nne, ningejenga hoja na wenzangu ya kuwa makini katika kupokea wanachama toka vyama vingine ambao huhamia hasa wakati wa uchaguzi mkuu. Hawa huhamia kimaslahi kuliko kupendezwa na Ilani, Itikadi na Falsafa za chama. Baada ya uchaguzi, hata kama wameshinda katika nafasi wanazoaminiwa, huwa na ukakasi katika kusema na kutenda kwao.
Tano, ningewashauri wanachama wenzangu na viongozi wetu wa CHADEMA KUJIKITA KATIKA MAMBO MAWILI MAKUBWA. La kwanza ni ujenzi wa Ofisi kuanzia Makao Makuu hadi huko kwenye ofisi za Wilaya. La pili, ni kuendelea kujitangaza, hata kama ni kimyakimya, hasa katika sehemu za vitongoji na vijiji. Baadaye, tujikite ngazi kwa ngazi kwa uchaguzi wa S/Mitaa, Udiwani na Ubunge.
Hakika, ningekuwa mwanachama wa CHADEMA, ningeyafanya hayo.