umenikumbusha kisa cha binti wa kimasai, siku moja mzungu alikuwa anahubiri umasaini binti akapanda juu ya mti amwone mzungu, mzungu akahamaki akamwambia binti shuka utukufu wa bwana u juu yako, baada ya mkutano binti akapewa magauni mawili na nguo ya ndani, kesho yake mamake akajiwahi mapemaa, mzungu kufika akahamaki mama shuka mzungu akauambia umati yatupasa kuwatunza wake zetu.Haiwezekani nikeshe mitandaoni nikiposti picha mbalimbali za Magufuli huku nikiandika "Magufuli jembe; Hapa kazi tu; Mtaisoma namba; Magufuli nitamchagua tena 2020; CCM oyee; wapinzani wajinga tuu; Makonda ni shujaa; nk." Na nisiwe appreciated, sijawahi hata kuonana na kiongozi wa chama ngazi ya Kata.
Lakini anatokea MTU mmoja anaimba nyimbo anasema "Kichaa kapewa rungu; We MTU gani hutaki kushauriwa wala kukosolewa, umerogwa wewe, unajiona ni ndugu yake Yesu; hakuna Uhuru wa habari wala taarifa ya habari, wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali; kuna viongozi wavuta bange, wapoo, maana wana maamuzi ya kise... Wapoo, na waliopoteza marinda, wapoo, kuna viongozi waliofoji vyeti wapooo; Mhe. hivi unamjua BASHITE?
Hili ni jipu jipya toka Kolomije; nk." Anaalikwa IKULU (State house) kwenda kula mishikaki na Rais (Mwenyekiti wa CCM), Waziri anampongeza na kumtaka atembelee Bungeni akapongezwe zaidi.