Haiwezekani nikeshe mitandaoni nikiposti picha mbalimbali za Magufuli huku nikiandika "Magufuli jembe; Hapa kazi tu; Mtaisoma namba; Magufuli nitamchagua tena 2020; CCM oyee; wapinzani wajinga tuu; Makonda ni shujaa; nk." Na nisiwe appreciated, sijawahi hata kuonana na kiongozi wa chama ngazi ya Kata.
Lakini anatokea MTU mmoja anaimba nyimbo anasema "Kichaa kapewa rungu; We MTU gani hutaki kushauriwa wala kukosolewa, umerogwa wewe, unajiona ni ndugu yake Yesu; hakuna Uhuru wa habari wala taarifa ya habari, wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali; kuna viongozi wavuta bange, wapoo, maana wana maamuzi ya kise... Wapoo, na waliopoteza marinda, wapoo, kuna viongozi waliofoji vyeti wapooo; Mhe. hivi unamjua BASHITE?
Hili ni jipu jipya toka Kolomije; nk." Anaalikwa IKULU (State house) kwenda kula mishikaki na Rais (Mwenyekiti wa CCM), Waziri anampongeza na kumtaka atembelee Bungeni akapongezwe zaidi.