Ningekuwa mwana-CCM hakika leo leo ningehama chama

Hapo zamani za kale Abunuwasi alimuendea mfalme akamwambia anaweza kumshonea suti ya thamani sana ambayo wenye dhambi watakuwa hawaioni na wasio na dhambi tu ndio watakuwa wanaiona. Mfalme akampa kazi Abunuwasi ya kutengeneza suti ya aina hiyo kwa ajili yake. Kwa siku kadhaa Abunuwasi alijifungia katika chumba akawa bize anashona suti ya mfalme. Baada ya siku tatu, mfalme akamtuma msaidizi wake akaangalie kazi inavyoendelea, yule msaidizi akaingia chumba alichokuwa akishonea Abunuwasi lakini hakuona kitu japo alimuona Abunuwasi akifanya vitendo kama vile yuko bize anashona nguo. Msaidizi akamwambia Abunuwasi, ‘Nimetumwa na mfalme niulizie umefikia wapi?” Abunuwasi akamjibu, “Kwani we huoni jinsi suti ilivyoanza kupendeza, ila bado namalizia nguo nyingine nataka kuanzia nguo za ndani ziwe ni hizi za kitambaa ambacho hakionekani kwa wenye dhambi”. Hakika yule msaidizi alikuwa haoni kitu lakini ili aonekane hana dhambi akaanza kusifu jinsi nguo zilivyoshonwa kwa ufundi. Akatoka na kurudi kumueleza mfalme kuwa Abunuwasi kamshonea nguo nzuri sana si za dunia hii kwa jinsi zilivyo nzuri. Mfalme alifurahi sana, kesho yake akamtuma msaidizi mwingine, nae kama yule wa jana akarudi kwa mfalme na ripoti nzuri sana ya maendeleo ya koti, pia akaleta taarifa nzuri kuwa kesho yake Abunuwasi angemaliza kazi na angeleta nguo ili mfalme azivae. Kesho yake mapema Abunuwasi akaingia katika kasri la mfalme akiwa kama kashika lundo la nguo, ambazo mwenyewe alisema wasio na dhambi tu ndio wataziona. Wasaidizi wa mfalme wote hawakuwa wanaona kitu lakini walianza kupiga makofi wakisifu jinsi nguo zilivyokuwa nzuri, hamna aliyekuwa anataka kuonekana ana dhambi. Hatimae Abunuwasi akamkabidhi mfalme nguo, mfalme nae hakuwa anaona kitu lakini ili asiambiwe ana dhambi akajidai eti nae anaziona akaanza kumsifu Abunuwasi kwa umahiri wake wa kuchagua rangi na hata ufundi wake mkubwa wa kushona. Abunuwasi akamuomba mfalme azivae zile nguo, wakaingia faragha mfalme akavua nguo zake na akaanza kuvaa nguo asizoziona kwa msaada wa Abunuwasi. Kwa vile alivua nguo zote na kuvalishwa mpya zisizoonekana, rohoni mwake alikuwa anajiona yuko uchi lakini akaona akitangaza haoni kitu wananchi wangemshangaa kuwa mfalme ana dhambi, hivyo akaendelea kusifia na kujiangalia kwenye kioo akisifu nguo zilivyompendeza. Kisha akalazimika kutoka nje ili wananchi waone nguo mpya za mfalme. Wote walikuwa wanamwona mfalme yuko uchi lakini wakawa wanaogopa kuonekana wana dhambi hivyo kila mtu akawa anashangilia na kusifu uzuri wa nguo za mfalme. Lakini ghafla mtoto moja mdogo kwa sauti kubwa akamuuliza baba yake, “Baba mbona mfalme yuko uchi?”. Minong’ono ikaanza mwishowe watu wakaanza kumuunga mkono mtoto, mfalme nae sasa aibu ikamshika kwani alijua sasa watu wote wanamuona yuko uchi, akatimka na kujificha kwenye kasri lake na hadithi yangu imeisha hapo.
Hadithi yako inatufundisha nn???
 
upo ushahidi kwamba vijana wanaounga mkono ccm wana uwezo mdogo mno ! Wengi ni wahanga wa dhiki za familia zao , unaweza kuta huyu lizaboni anaishi kwa mmoja wa viongozi wa ccm , baada ya kukimbia dhiki kwao .

Kwa hali kama hiyo hata wakinyanyaswa vipi hawawezi kuhama ccm , watakula nini ?
Chunguza upya uone kina nani wana io dhiki unayoisema.Mtu kuwa na wavu na mali ya mtu mwingine huoni kama ni umaskin wa hali ya juu.Watu wanahisi makonda akiondoka ndo umaskin wao utaisha.Tunakua maskini sababu tunatumia mda vibaya kufuatilia umbea.
 
Haiwezekani nikeshe mitandaoni nikiposti picha mbalimbali za Magufuli huku nikiandika "Magufuli jembe; Hapa kazi tu; Mtaisoma namba; Magufuli nitamchagua tena 2020; CCM oyee; wapinzani wajinga tuu; Makonda ni shujaa; nk." Na nisiwe appreciated, sijawahi hata kuonana na kiongozi wa chama ngazi ya Kata.

Lakini anatokea MTU mmoja anaimba nyimbo anasema "Kichaa kapewa rungu; We MTU gani hutaki kushauriwa wala kukosolewa, umerogwa wewe, unajiona ni ndugu yake Yesu; hakuna Uhuru wa habari wala taarifa ya habari, wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali; kuna viongozi wavuta bange, wapoo, maana wana maamuzi ya kise... Wapoo, na waliopoteza marinda, wapoo, kuna viongozi waliofoji vyeti wapooo; Mhe. hivi unamjua BASHITE?

Hili ni jipu jipya toka Kolomije; nk." Anaalikwa IKULU (State house) kwenda kula mishikaki na Rais (Mwenyekiti wa CCM), Waziri anampongeza na kumtaka atembelee Bungeni akapongezwe zaidi.

Hakika Tanzania imepoteza mwelekeo kwa 90%!
Yaani ukisoma matukio yanayotokea na maamuzi ya huyu Rais Magufuli lazima uone wazi kuwa LIKO TATIZO KUBWA!!?
Rais aliyeko madarakani yuko Ikulu by chance na hakuwahi kufikiria au kufikiriwa kuwa Rais!!!!Iam Very very sorry to most Tanzania citizens!!!
 
Chunguza upya uone kina nani wana io dhiki unayoisema.Mtu kuwa na wavu na mali ya mtu mwingine huoni kama ni umaskin wa hali ya juu.Watu wanahisi makonda akiondoka ndo umaskin wao utaisha.Tunakua maskini sababu tunatumia mda vibaya kufuatilia umbea.
Makonda ameingiaje hapa ?
 
Haiwezekani nikeshe mitandaoni nikiposti picha mbalimbali za Magufuli huku nikiandika "Magufuli jembe; Hapa kazi tu; Mtaisoma namba; Magufuli nitamchagua tena 2020; CCM oyee; wapinzani wajinga tuu; Makonda ni shujaa; nk." Na nisiwe appreciated, sijawahi hata kuonana na kiongozi wa chama ngazi ya Kata.

Lakini anatokea MTU mmoja anaimba nyimbo anasema "Kichaa kapewa rungu; We MTU gani hutaki kushauriwa wala kukosolewa, umerogwa wewe, unajiona ni ndugu yake Yesu; hakuna Uhuru wa habari wala taarifa ya habari, wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali; kuna viongozi wavuta bange, wapoo, maana wana maamuzi ya kise... Wapoo, na waliopoteza marinda, wapoo, kuna viongozi waliofoji vyeti wapooo; Mhe. hivi unamjua BASHITE?

Hili ni jipu jipya toka Kolomije; nk." Anaalikwa IKULU (State house) kwenda kula mishikaki na Rais (Mwenyekiti wa CCM), Waziri anampongeza na kumtaka atembelee Bungeni akapongezwe zaidi.
Wewe umeshawahi kuonana na Mbowe toka umeanza kubwabwaja humu?
 
Back
Top Bottom