Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo

Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo

Kafyulilo

Senior Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
106
Reaction score
70
Watanzania wengi bado wapo katika hali ya tahayari kufuatia kufuatia maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA (CC) kuwafukuza wanachama wake watatu ambao walikuwa na majina makubwa ndani ya chama hicho. Ni wazi kuwa CHADEMA haikumuangalia mtu usoni, ikarusha lungu lake bila kujali linamwangukia nani.

Nikiwa kama mwanachama wa CHADEMA, kwanza naunga mkono maamuzi ya CHADEMA kwa ujumla wake kwa kuwa yanajaribu kukitofautisha na vyama vingine vinavyolinda zaidi uenzetu badala ya kusimamia sheria na taratibu za uongozaji wa chama na pia katiba ya vyama vyao. Katika hili, CHADEMA imetuaminisha kwamba hata ikishika dola, itakuwa tayari kumuwajibisha yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na miiko ya uongozi, atakayeisaliti nchi, kuitia aibu na hata kutusababishia hasara au kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa vyenye kuisababishia umaskini nchi yetu na watu wake. Katika hili nakipongeza CHADEMA chama changu.

Pamoja na pongezi hizi, bado naona kwamba maamuzi haya yalikuwa ni ya haraka, na pengine yalitokana na mihemuko ya baadhi ya wanachama. Nasema hivi kwa sababu, katika ushiriki wa MM, M1 na M3 katika uandaaji wa waraka wa siri 2013, mmojawao ambaye ni Kitila Mkumbo alikubali makosa mara moja baada ya waraka huu kugunduliwa, alikuwa tayari kuachia ngazi kama sehemu ya uwajibikaji kwa kosa alilofanya, na hata pale alipotakiwa kwenda mbele ya kamati kujitetea, alifanya hivyo tofauti na wenzake walivyofanya ambao waliamua kutoroka na hata kukimbilia mahakamani. Ni dhahiri kwamba yeye kwa nafasi yake aliyajutia makosa yake na akaonyesha nia ya kutubu na kuendelea kukitumikia chama chake. Tayari Dr. Mkumbo ameshaaminiwa na chama kwa mambo mengi na makubwa, na kwa hakika ameshawekeza vya kutosha kwa ajili ya chama, ilitosha kumsamehe na kumpa onyo.

Nikitazama nyuma, katika utumishi wake ndani ya chama; tofauti na wenzake yeye hajawahi kuwa na kashfa yoyote wala kushiriki kwa namna yoyote kukihujumu chama. Kwa mfano ukimtazama mtu kama Mwigamba, tayari alishawahi kutofautiana na chama kiasi cha kufikia kuondolewa katika nafasi yake ya uhasibu kule makao makuu. Wakati Zitto ameshajihusisha mara kadhaa katika vitendo vyenye kutiliwa shaka ikiwemo kuendesha kikundi cha PM7 ambacho kilifanya kazi ya kuwachafua viongozi kwa nia ya kumjenga Zitto. Lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia kujihusisha na lolote.
Ninawaza ya kwamba kama chama hiki kilikuwa tayari kumsamehe Ben Saanane, ambaye alikuwa ndiye master planner wa mkakati mzima wa kumpindua Mbowe na Slaa kwa faida ya Zitto, hasa baada ya kukosa nafasi BAVICHA, ni kwa vipi kimeshindwa kumsamehe Kitila ambaye alishiriki kuedit tu waraka huu wa kuwaangusha akina Mbowe?

Bado ninaona kwamba Kitila ana mapenzi mema na chama hata kama kwa sasa amekata tamaa na kutamani mbadala wa CCM na CHADEMA. Nafikiri yaanzishwe mazungumzo kati ya chama na Kitila ili kuona ni namna gani anaweza kurudi chamani na ikiwezekana atimize ndoto zake za kuwa mbunge wa Singida kupitia CHADEMA na apewe onyo ili akitumikie chama kwa uaminifu kwa mjibu wa katiba ya chama.

Nina matamanio makubwa ya kuona Kitila anarudi CHADEMA. Kama NCCR mageuzi walimsamehe Kafulila, ni kwa vipi CHADEMA washindwe kumsamehe Kitila na ukizingatia kuwa ni kosa lake la kwanza? Ni lazima tutambue kwamba kama binadamu tuna mapungufu yetu, and we are prone to mistakes. Haitashangaza sana iwapo itatokea kwamba hawa hawa wanaosimama kwenye CC ya CHADEMA na kutoa hukumu kali dhidi ya watu ambao wapo tayari kutubu na kujirekebisha wakafanya madudu makubwa kushinda haya.

Sijamsemea Zitto na Mwigamba kwa kuwa tayari walishakuwa na kashfa za utovu wa nidhamu ndani ya chama kiasi cha kustahili adhabu, lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia katika hayo.

Nawaombeni viongozi wa CHADEMA mpunguze hasira, na kutoa nafasi ya mazungumzo na mwanazuoni huyu, na ninamwomba sana Dr. Kitila apunguze hasira, ajirudi na kukubali mazungumzo na viongozi wa CHADEMA. Waswahili husema kosa moja haliachi mke, nami nasema kosa moja la Kitila lisitufanye tukose mchango wake mhimu kwa chama.

Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki CHADEMA!
 
Last edited by a moderator:
umbea ule ule wa CCM..mara ni mwanaCDM, mara ni walewale walio busy na Ben Saanane...Kilila keshaanza ongea mbaya ktk media ktk ile midahalo yao ya kike isiyo na mvuto..haswaTBC
 
Jipe muda pitia kwenye thread inayohusu masalia (kama sikosei ilikuwa mwishoni mwishoni mwa mwaka 2012) uone jinsi Mkumbo alivyokuwa ndumilakuwili hasa kuhusu swala la madiwani wa Arusha.
 
umbea ule ule wa CCM..mara ni mwanaCDM, mara ni walewale walio busy na Ben Saanane...Kilila keshaanza ongea mbaya ktk media ktk ile midahalo yao ya kike isiyo na mvuto..haswaTBC
Siyo kila anayekuja na mawazo tofauti au mtizamo tofauti ni mwanaCCM. Acheni utoto huo. Ni kwa lipi baya nililomsema Ben Saanane? Sijawahi kutofautiana na Ben Saanane, ila nimemtolea mfano tu, focus ya mjadala hapa ni Kitila, kama una la kuchangia kuhusu Kitila fanya hivyo.
 
Under normal conditions this cannot happen, with due respect and odient to cdm party, members and the entire ledeship I do agree 100% to the forginess of Dr. Mkumbo and allow his comeback to reinforce the party.
 
Jipe muda pitia kwenye thread inayohusu masalia (kama sikosei ilikuwa mwishoni mwishoni mwa mwaka 2012) uone jinsi Mkumbo alivyokuwa ndumilakuwili hasa kuhusu swala la madiwani wa Arusha.
Niliisoma hiyo habari, lakini haikuwahi kupata ushahidi wa moja kwa moja. Lakini pia kama wazo lake lilikuwa ni kutowafukuza badala yake wapewe onyo, basi ni dhahiri kwamba bado ni mtu anayeamini katika msamaha, na yafaa asamehewe.
 
Siyo kila anayekuja na mawazo tofauti au mtizamo tofauti ni mwanaCCM. Acheni utoto huo. Ni kwa lipi baya nililomsema Ben Saanane? Sijawahi kutofautiana na Ben Saanane, ila nimemtolea mfano tu, focus ya mjadala hapa ni Kitila, kama una la kuchangia kuhusu Kitila fanya hivyo.
mbona unakataa utoto kitoto zaidi...wewe ndiye mtoto...huna dili..hembue rudia ulichoandika.Wabongo mnajishusha sana hadhi kwa fikra za njaa hizi...wewe mhemko nani anao...?Kitila kaadhibiwa km sheria zitakavyo na hakuwa ameonewa.sasa mnataka msamaha wa lazima?HIyo logic ya wapi.. Acha undezi wewe
 
Ignored!
 
kitila hahitaji mbeleko wa chadema atachana mda siyo mrefu.
 
Niliisoma hiyo habari, lakini haikuwahi kupata ushahidi wa moja kwa moja. Lakini pia kama wazo lake lilikuwa ni kutowafukuza badala yake wapewe onyo, basi ni dhahiri kwamba bado ni mtu anayeamini katika msamaha, na yafaa asamehewe.

Basi haukusoma hiyo habari maana habari ninayoongerea hausiani ni kusamehana bali ni undumilakuwili.. kwa viongozi anaongea ili na kwa madiwani anawambia ufanye kinyume na alichowashauri viongozi... Pia lile sakata la mida 8 na masalia hata Mkumbo yumo kama ulimsoma vema mida 8.
 
Kitila Mkumbo huyo huyo unayeshauri asamehewe majuzi tu kaandika mfululizo wa makala hapa jamvini title yake anasema Tanzania inahitaji chama mbadala wa CCM na CDM; hapa mtu mzima huitaji kuwa na shahada ya uzamivu kuona kutambua kwamba kwa maoni yake Kitila Mkumbo CDM na CCM vyote sawa " vyote mangalanya" vyote havifai! kama huo ndio mtazamo wake basi hakuna sababu kwa CDM kumsamehe kwa sababu chama chenyewe anakiona kwamba hakifai!!
Na hata hivyo Kitila alikuwa anaihitaji CDM kuliko CDM ilivyokuwa inamuhitaji yeye; alitakiwa alitambue hilo; CDM ni Taasisi ambayo inatakiwa kuwa endelevu, lakini Kitila ni kinyume chake sio Taasisi bali "a mere mortal and a dispensable individual at that!!"; kitu cha kuendeleza hapa ni taasisi ili idumu lakini sio watu binafsi ambao kwa vyovyote vile ipo siku ama wataelekea mbele ya haki au watastaafu na au kuachana na siasa; let go Kitila and the likes of his ilk; Ndumila kuwili; wasaliti.

Kitila alitakiwa asiishie kutumia akili ndogo ya Zitto na Mwigamba peke yake bali angetumia na akili yake mwenyewe ambayo anayo kubwa tu! lakini this time around hakuitumia ipasavyo akaacha gap akili ndogo ya Zitto na Mwigamba zikatawala akili yake kubwa;
He should blame himself not CDM.

CDM itaishi tu na kusonga mbele toward full ukombozi bila Kitila and the likes of him.
Adieu Kitila; God speed
 
wasomi wapo wengi bana achana nae utamsahau tu

Kweli Mkuu. Inaonekana jamaa ana mahaba sana kwa Mkumbo. Duniani kote usaliti kwa taasisi pengine ndilo kosa kubwa zaidi. Stahili za wasaliti kwa taasisi kama majeshi, Serikali, na baadhi ya dini zinaeleweka. Haiyumkiniki kuwaza msamaha kwa watu wa aina hii.
 
Kitila Mkumbo huyo huyo unayeshauri asamehewe majuzi tu kaandika mfululizo wa makala hapa jamvini title yake anasema Tanzania inahitaji chama mbadala wa CCM na CDM; hapa mtu mzima huitaji kuwa na shahada ya uzamivu kuona kuwa tafsiri fupi ni kwamba kwa maoni yake CDM na CCM vyote "mangalanya" havifai! kama huo ndio mtazamo wake basi hakuna sababu kwa CDM kumsamehe kwa sababu chama chenyewe hakifai!!

...

Kweli Mkuu; kupitia hizo makala zake ambazo pia zili-appear kwenye baadhi ya media nilishindwa kumwelewa huyu jamaa kama alikuwa na hayo mawazo akiwa bado yupo Chadema au baada ya kufukuzwa Chadema. Hii ni hoja muhimu sana kuijua ili kumfahamu vizuri huyu mtu.
 
Siyo kila anayekuja na mawazo tofauti au mtizamo tofauti ni mwanaCCM. Acheni utoto huo. Ni kwa lipi baya nililomsema Ben Saanane? Sijawahi kutofautiana na Ben Saanane, ila nimemtolea mfano tu, focus ya mjadala hapa ni Kitila, kama una la kuchangia kuhusu Kitila fanya hivyo.

Mkuu hawa madogo ni wakupuuza.......mimi naungana na waliowapa jina misukule/vifaranga......yaanihuwa hasomi mada akikuona una wazo mbadala yeye anaharisha tu....................wengi wao tabia zao ni kama wanamziki wa bongo fleva hupennda kujisifia na kupeana majina ya wanamziki maarufu na kuigiza' kwa upande wa hawawenyewe hujidai ni wanakombozi wa nchi kwamba wao ni wazalendo zaidi.......wanaamini kwamba 'sumu' wanazolishwa na kina Slaa ni kweli 100% wengi wao hawataki kazi wanaamini kula nchi Slaa akiingia madarakani ndio maana wanaitana ''makamanda''!
 
mbona unakataa utoto kitoto zaidi...wewe ndiye mtoto...huna dili..hembue rudia ulichoandika.Wabongo mnajishusha sana hadhi kwa fikra za njaa hizi...wewe mhemko nani anao...?Kitila kaadhibiwa km sheria zitakavyo na hakuwa ameonewa.sasa mnataka msamaha wa lazima?HIyo logic ya wapi.. Acha undezi wewe

Akili za bavicha zipo hivi sababu ya bange na viroba!

1620987_688701521226278_62794813_n.jpg
 
Back
Top Bottom