Ninayoyaona Kigali

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Kila baada ya mita kama 100 kuna askari watatu au wanne, full combat wakiwa na mitutu. Wenyewe wanyarwanda wanatembea tu bila hofu, lakini mimi imenikera sana kuishi maisha ya mashaka namna hii.

Nimeuliza wenyeji wanasema kuna tetesi za mashambulizi kutoka kwa majenerali waliokimbia Rwanda, na eti kuna milipuko ya guruneti, ambayo kwa bahati nzuri haijatokea tangu nimefika hapa.

Inavyoelekea bajeti ya ulinzi ya nchi hii ni balaa tupu maana hata kama wanawalipa mishahara kidogo hawa wajeshi, ni wengi mno na pia kuna dalili ya kuzagaa wapelelezi wengi mitaani. Ukitembea unapigwa macho ya udadisi karibu na kila mtu kiasi imani inakutoka.

Haya sio maisha, tuombe Mungu yasitokee kwetu.
 
Huyo ndio Gen. Kagame; Anawaogopa wahutu wa FDLR kwani wamejiandaa kuja kuichukua tene nchi toka kwa watutsi. In actual sense sio nchi ya kukaa iwapo ni mtu wa kubwabwaja kama Bongo yetu ya Kikwete. Sitahama Bongo hata kama "CDM" kama inavyodaiwa wataanzisha Tunisia
 
Acha utoto wewe! We ulipokuwa unakata shauri la kwenda Kigali ulijuwa unaenda Geneva au Vatican City?
 
Kigali haiwezi kutulia, maana Kagame anatumia intelijensia kuwamaliza wapinzani wake kisiasa. Mfano mama Ingabire...maskini amechezea saaana korokoroni mpk kashindwa kushiriki uchaguzi, wafuasi wake hawawezi kukubali watalianzisha tu kiaina.
 
Kila baada ya mita kama 100 kuna askari watatu au wanne, full combat wakiwa na mitutu. Wenyewe wanyarwanda wanatembea tu bila hofu, lakini mimi imenikera sana kuishi maisha ya mashaka namna hii.

Nimeuliza wenyeji wanasema kuna tetesi za mashambulizi kutoka kwa majenerali waliokimbia Rwanda, na eti kuna milipuko ya guruneti, ambayo kwa bahati nzuri haijatokea tangu nimefika hapa.

Inavyoelekea bajeti ya ulinzi ya nchi hii ni balaa tupu maana hata kama wanawalipa mishahara kidogo hawa wajeshi, ni wengi mno na pia kuna dalili ya kuzagaa wapelelezi wengi mitaani. Ukitembea unapigwa macho ya udadisi karibu na kila mtu kiasi imani inakutoka.

Haya sio maisha, tuombe Mungu yasitokee kwetu.

imani hapo ni zero....kwenye reds hapo umekurupuka kwa ama kutoijua historia ya kigali au kwasababu umefika na tu perception yako hapo ni mahali pasipo na amani....ok matukio ya kigali..rwanda na burundi siyo matokeo ya kutomcha Mungu .....rejea historia na utaikuta nukta moja ambapo hata wacha mungu walishiriki hayo matokea na sina kumbukumbu kama hao wacha mungu hawakutumia misaafu unayoitumia wewe.

Hata kama dini na vitabu vyake visingekuwepo basi Mungu angekuwepo tu...I was born with it,how should I leave it to you?
 
Ukijuwa historia ya Rwanda/Burundi hautashangaa vitu vidogo kama hivi,Kagame ana mapungufu yake lakini kaifanyia mengi Rwanda.Hivi unaweza kumtumia Kikwete tweet kwenye twitter kumualika kuja kujumuika na watoto wanaocheza Tennis akajibu na kuja siku hiyohiyo ? hayo yanatokea Rwanda kila siku rais unawasiliana naye na anakujibu.

Soma SAVVY KENYA - The Adventures of a Former Campus Girl
 
Acha utoto wewe! We ulipokuwa unakata shauri la kwenda Kigali ulijuwa unaenda Geneva au Vatican City? Peleka mbele utumbo huu!1
nani mtoto sasa hapa wewe au mtoa mada? kwani lazima uchangie? haya basi tuambie wewe uliyoyaona huko genva au vatican city......... heshima ni jambo la bure kijana usiandike kumtusi mtu wakati anatoa taarifa ya nchi za wenzetu wanavyoishi... ila sikulaumu ndio kwanza una siku 4 jamiiforums so bdo una utoto mwingi ukukua utaacha
 
Watu wa Habyarimana mpaka kesho hawakubali Kagame atawale na bado hawajamsamehe kumuua ndugu yao Juvenali.
 
What is happening in Kigali is innevitable. Wacheni Kagame aiweke nchi sawa kwa sera zake. Anafanya mengi sana Rwanda kimaendeleo, kiuchumi na kijamii. Wanajeshi mitaani na inteligensia kuzagaa ni nyenzo yake. Muhimu Warwanda wanaridhika na hawashtushwi. Km wewe hufurahii rudi kwenu bongo uendelee kuishi na UFISADI, MGAO WENU WA UMEME, ONGEZEKO LA GHARAMA ZA VYAKULA NA BIDHAA BILA MPANGO, ELIMU MBOVU NA MIGOMO KILA SIKU. Karibu sana Tanzania.
 
Wewe umekuja lini kwetu ... Wenzio tumeishazoea... Na ukiwa mwongeaji kesho unapotea....kama msekule.... Hapa lazima utembee umejizatiti huyu Kagame si mchezo...lakini ukifuata taratibu utafurahia sana maisha ya kwetu... Karibu Kigali.
 
Kweli nchi hii ina Demokrasia inayowatosha wao! Kipimo chao kabisaaaaaa! Maana ukiwapa zaidi lazima watachinjana!
 
Acha utoto wewe! We ulipokuwa unakata shauri la kwenda Kigali ulijuwa unaenda Geneva au Vatican City? Peleka mbele utumbo huu!1

Mungu akusamehe, akuokoe kutoka katika ujuha wako. Mimi nachangia kwa wenye kuhitaji habari. Ungekuwa na hekima ungekaa kimya.
 
[/COLOR][/I][/B][/COLOR][/SIZE]

imani hapo ni zero....kwenye reds hapo umekurupuka kwa ama kutoijua historia ya kigali au kwasababu umefika na tu perception yako hapo ni mahali pasipo na amani....ok matukio ya kigali..rwanda na burundi siyo matokeo ya kutomcha Mungu .....rejea historia na utaikuta nukta moja ambapo hata wacha mungu walishiriki hayo matokea na sina kumbukumbu kama hao wacha mungu hawakutumia misaafu unayoitumia wewe.

Hata kama dini na vitabu vyake visingekuwepo basi Mungu angekuwepo tu...I was born with it,how should I leave it to you?

Mtu kama huyu ana faida gani JF? Mimi nimesema wapi kuwa matukio ya Kigali na matokeo ya kutomcha Mungu? Kusoma na kuelimika kweli ni vitu viwili tofauti!
 
Nimesema sikuzote Rwanda is a time bomb. Maendeleo ya kweli ni uhuru wa watu. Kama ungenifungia chumbani na kunipa vyakula na vinywaji mbali mbali na redio na tv n.k n.k bado ningechagua kuwa nje (uraiani) bila vitu vingi!!!!!
 
Hiyo ni kawaida ya kigali,tatizo ni ugeni wako tu.
hapo ni katikati ya DRC kule Gisenyi,UGANDA kule Chanika na BURUNDI kule Butare.nchi hizo zote si shwari na usisahau FDRL bado wapo msituni VIRUNGA.Na Gen kayumba nyamwasa bado ana ushawishi ndani ya rwanda.Kwa hiyo kila siku jioni :ni ratiba ya kawida askari kusambazwa Remela,nyamirambo,kichukiro,kimironko,nyamitarama na kigali yoote.usisahau Kagame haishi "ikulu"bali katikai ya kigali mchanganyiko.
 
Back
Top Bottom