Mtikila:flora (mutusi kutoka kigali) wa unhcr unawatesa wkimbizi wahuntu tz. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila:flora (mutusi kutoka kigali) wa unhcr unawatesa wkimbizi wahuntu tz.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwamakula, Oct 15, 2011.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  MCH. MTIKILA AMEMTUHUMU BI FLORA NA WENZAKE WANAOFANYA KAZI UNHCR KUWA WANATUMIWA NA KAGAME KUWATESA WAHUNTU WALIOKIMBIA UMAFIA WA KAGAME KUTOKANA NA KUZUIWA KUFANYA SIASA.

  FLORA ANATAJWA KUWA MTUSI ALIYEZALIWA KIGALI NA KUPANDIKIZWA NA KAGAME ILIKUWAKAMATA KIRAHISI WAPINZANI WANAO ENDESHA SIASA ZA UKOMBOZI WA DEMOKRASIA BADALA YA UDIKITETA AMBAPO RAIS KAGAME AMEPIGA MARUFUKU SIASA ZA VYAMA VINGI NA SASA ANAUA MWANASISA YOYOTE ANAYEENDESHA UPINZANI.

  BI .FLORA WA UNHCR AMETUHUMIWA KUMUKAMATISHA MWANASIASA MMOJA AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA SIASA ALIYEKIMBILIA NCHINI KUPATA HIFANZI.

  FLORA ANAFANYA NJAMA ZA KUMUSAFILISHA KWA SIRI KWENDA MIKONONI MWA KAGAME ILI AUAWE.
  SERIKALI YA AFRIKA KUSINI IMEGOMA KUMUKABIDHI MAJOR KAYUMBA NYAMWASA KUHOFIA KUAWA.
  HATA HIVYO KAGAME AMETUMA WATU WAKE KATIKA BALOZI ZOTE BARANI AFRIKA KUWASAKA WAHUNTU A KUWAUA!

  HABARI ZA HIVI KARIBUNI ZIMEMNASA KAGAME KUISHUTUMU TANZANIA KUWA IN WATU WANAO TAKA KUPINDUA SERIKALI YAKE  [h=2][FONT=&quot]RAIS KAGAME AISHUTUMU TANZANIA [/FONT][/h] [FONT=&quot]5th March 10

  Rais Paul Kagame wa Rwanda ameituhumu Tanzania kwamba inaruhusu watu wanaoipinga Serikali yake kuendeleza harakati za kuhujumu nchi hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali juzi na taarifa zake kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Kagame alisema atawasiliana na Tanzania ili watu hao wanaoendesha harakati hizo wakamatwe.Mbali na Tanzania, Kagame pia aliitaja Kenya na Uganda kwamba kuna watu kama hao wanaoendesha harakati dhidi ya serikali yake, lakini akaapa kwamba kamwe hawataweza kuiangusha serikali yake.Katika mkutano huo, Kagame pia alimshambulia mshirika wake wa zamani wakati wa mapambano ya kuikomboa Rwanda, Luteni Jenerali Kayumba Nyamwasa ambaye alikuwa balozi wa nchi hiyo nchini India kwamba ni miongoni mwa watu wanaoendesha chokochoko dhidi ya serikali yake.
  Alisema Kayumba ambaye alivuliwa ubalozi hivi karibuni na sasa amekimbilia Afrika Kusini kuomba ukimbizi wa kisiasa, kuwa wamekuwa na mawasiliano na aliyekuwa mkuu wa mambo ya usalama Luteni Jenerali Patrick Kalegeya katika mipango yao ya kuhujumu Rwanda.
  Majenerali hao wote walikuwa washirika wa Kagame lakini sasa wamekimbia nchi kutokana na kutofautiana na Rais huyo huku wakimtuhumu kwa kuendesha nchi kidikteta.
  Alimtaja Kayumba kwamba alihusika na mashambulizi ya maroketi jijini Kigali hivi karibuni na kwamba ataiomba Afrika Kusini kumrejesha nyumbani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Akijibu tuhuma dhidi yake, Jenerali Kayumba alisema kwamba Rwanda inazidi kuzama katika utawala wa kidikteta na kumtaja Rais Kagame kama mtu asiyetaka kukosolewa na yeyote.
  Jenerali Kayumba ambaye amekwisha kupata hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa Afrika Kusini, alisema Rais huyu anataka watu wa kumlamba miguu kumzunguka lakini si watu wanaoweza kutoa mawazo yao.“Madaraka yasiyokuwa na mipaka huporomoka vivyo hivyo, nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya mtu mmoja tu huku akipingana na wale wenye mawazo tofauti,” alisema Jenerali Kayumba.Kadhalika, Jenerali Kayumba alikanusha vikali kuhusika na mashambulizi ya Kigali ya hivi karibuni na kusema yalipangwa na serikali ya Kagame mwenyewe kwa nia ya kuwapakazia watu asiowataka.Rais Kagame alisema Mwendesha Mshitaka Mkuu wa Serikali, Martin Ngoga, hivi karibuni aliwataja Jenerali Kayumba na Jenerali Karegeya kuwa ndio waliopanga mashambulizi hayo.Wakati Wanyarwanda wakilumbana kuhusu mashambulizi ya Kigali ya hivi karibuni, Nipashe iliwasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, juu ya Tanzania kutuhumiwa na Rwanda, lakini alisema yuko safarini Cairo, Misri.Hata hivyo, alisema kwamba bado serikali hajaipata taarifa rasmi za malalamiko ya Rais Kagame ili iyatazame na kuyatolea tamko.Hata hivyo, Membe alisema Tanzania wakati wote imesema wazi kwamba haifanyi wala kuunga mkono kitendo chochote cha kuhujumu nchi jirani katika ardhi yake. Membe alisema Tanzania ilikwisha kutoa msimamo wake wakati taarifa za kuhujumiwa kwa Rwanda zilipotolewa na maofisa wa Umoja wa Mataifa na kuitaja serikali kusaidia waasi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa kusisitiza kwamba imejitolea kwa nguvu zake kuhakikisha kwamba amani inarejea katika ukanda wa Maziwa Makuu.
  “Ni jambo lisiloingia akilini kusema kwamba Serikali ya Tanzania inaweza kupanga mkakati au kutoa msaada kwa kikundi chochote kinachokusudia kuvuruga amani katika ukanda huu,” alisema Membe ambaye aliahidi kutoa taarifa zaidi akishawasiliana na ofisi yake.[/FONT]
  [FONT=&quot]SOURCE : NIPASHE

  [/FONT]
   
 2. Ngadu

  Ngadu Senior Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo wahutu tu, hata watutsi wenzake kama nyamwasa wakitofautiana naye inakaula kwao.
   
 3. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwamakula, nina wasiwasi na kiswahili chako hasa kwenye hii topic. Kimekaa kama cha Kihutu......
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Afadhali Kagame kasema watu wote mnajua kuliko CCM kusema amani na huku wanaua na kuwaweka magerezani wana mapinduzi .Hili mnalionaje ?
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kiswahili kinajieleza. Ni mhutu anpiga mayowe!! Afadhali udikteta wa Kagame unaleta maendeleo kuliko sisi ambao tuna demokrasia lakini maendeleo hakuna!!
   
 6. y

  yaya JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 7. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Hivi sahihi WAHUNTU au WAHUTU? Mtoa maada ametumia sena neno HUNTU. Ni mtazamo wangu, ila mi binafsi namkubali sana kagame. Ijapokuwa watu wanamtuhumu kuwa ndie aliyehusika kwenye kumua rais mwaka 1994.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,348
  Trophy Points: 280
  Kagame na Kikwete hawana lolote zaidi ya kushindana u handsome, matumizi mabaya ya fedha za umma na vituko vyao kipindi walipokuwa kwenye kambi za kijeshi.
  www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/175183-kagame-akaa-hoteli-ya-sh-milioni-30-kwa-siku-new-york-kikwete-je-2.html
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tuna shida nyingi sana mtikila... komaa na ya nyumbani kwanza, au ndio ushahongwa kama kawaida yako?
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  aiseeeeeeeeeeeeee
   
 11. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mkuu, una uhakika na hapo nilipigia mstari?? mauaji ya raia mfano majuzi huko Igunga ndiyo demokrasia ya kujivunia??
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu demokrasi ipo si vyama vingoi vinashitriki katika uchaguzi na kutumia pesa lukuki za walipa kodi aeti katika kutekeleza demokrasia? Vyama vinapewa ruzuku ati kukuza demokrasia na kuna institution kibao za kukuza demokrasia; NEC, Msajili wa Vyama na nyingine lukuki zinakula pesa kwa jina la demokrasia!! Labda nikuambie kwamba katika nchi kama hii yetu mimi ningepebda kuwe na dikteta atunyooshe kisha tupate akili ya kujadili jinsi ya kutawalana kwa misingi ya kukubaliana. Lakini hii demokrasia pandikizi si demokrasia bali ghasia tu!!
   
 13. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,632
  Trophy Points: 280
  mimi ninachojua,vita ya mwaka 1994 ilikua kati ya watutsi na wahutu,yaani wote walihusika.lakini cha ajabu wanaohukumiwa kufungwa na mahakama inayoshugulikia kesi za rwanda mjini Arusha,inahukumu wahutu tu.watutsi hawahukumiwi.je hapo kuna haki?na muhutu yeyote aliyesoma anatafutwa na kubambikiwa kesi.malengo ya kagame ni kutokomeza wahutu wote ndo maana wahutu wasomi wanakimbia nchi.halafu hata rwanda bado kuna ubaguzi wa elimu.kama tanzania na matajiri.
  Kagame ni noma.roger
   
 14. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe 100%!!! TZ inahitaji dictator kama Kagame.Mfumo wote umeharibika. Ili kuuweka sawa lazima udikteta kwanza, democracy baadaye, ingawa wazungu hawatakubali. Tatizo la udikteta ni kwamba baadaye mtawala anagoma kuondoka madarakani kama Kagame na Ghadhafi.
   
Loading...