Miaka ya 80 nilikua mdogo sana kuweza kuweka kumbukumbu....lakini niliwahi kusoma gazeti la Uhuru enzi hizo kichwa cha habari kilikua `Samwel Sitta Aden Rage wafukuzwa kazi...Rais Julius Nyerere amewafukuza kazi mkurugenzi mtendaji wa CDA Ndugu Samwel Sitta na ofisa Utawala Ismail Aden Rage kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma....
Mkuu kama unalo hilo gazeti naombwa tumwagie au tukumbushane kwa kirefu ilikuaje
Dogo ninajua unahitaji kuelewa mambo, hapo kwenye nyekundu nitakuweka sawa,
Samwel Sitta hakuwahi kufanya kazi CDA na kufukuzwa kazi,pia
Aden Rage hakuwa afisa kulingana na kisomo chake cha cheti cha uhasibu SHYCOM alikuwa kalani tu wakupakua mizigo ya CDA toka DSM kwenda Dodoma ilipo CDA, sasa katika mizigo hiyo ndo walikuwa wanaiba mingine na wenzie maana ilikuwa sindicate fulani, miongoni ya mizigo hiyo zilikuwa ni furniture za ikulu ya Chamwino
Cheo chake
Rage kilikuwa ni clearing and forwarding clerk.
Kufukuzwa kwao kazi.
Noma ya wizi huo aliisanua mbunge Severini Supa kufuatia ile kesi kuu ya ubunge kati ya Padri Simon Chiwanga na yeye Padri Severino Supa ambapo ilidhihirika Padri Simon Chiwanga wakati huo alikuwa waziri wa elimu alitoa rushwa ya majembe kijiji cha Nkong`onta ambapo sasa ni sehemu ya chuo kikuu cha UDOM, ikumbukwe enzi hizo wabunge walikuwa wanapewa alama maalum kuwatambulisha ambapo ilikuwa jembe na nyumba sasa Padri Chiwanga alama yake ilikuwa ni jembe
Katika kesi hiyo padri Chiwanga alipigwa chini ubunge na jaji malehemu Rugakingila.Noma ya akina
Rage ilisanuka ikamfikia Nyerere kwa sababu Mkurugenzi wa mamlaka ya usitawishaji makao makuu alikuwa Sir. George Kahama , sasa katika hiyo kesi kuu yeye alikuwa upande wa Padri Chiwanga na inasemekana alitumiwa na
Chiwanga kupenyeza mlungula kwa jaji Kahwa Rugakingila kwa kuwa walikuwa kabila moja , huo mlungula ulikataliwa na haki ikatendeka, kuona vile ndipo nae Supa kupitia wapambe wake wakaanika wizi uliokuwa unafanywa na Rage na genge lake chini ya utawala wa Sir George Kahama.
Rais Nyerere alimhamisha Sir George Kahama na akawafukuza kazi akina Rage na genge lake walikuwa 9.
Habari hizo wakati huo zilikuwa ni gumzo Tanzania nzima mtu kuvuliwa ubunge ndio ilikuwa tukio la kwanza, na hilo gazeti unalosema ulisoma lilikuwa ni dairy news.
Weka kumbukumbu zako sawa dogo.