Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,794
Habari za asubuhi wapendwa,
Ajira yangu ya kwaza ilikuwa katika shirika la kigeni, katika shirika lile nilikutana na makaka wawili wa ki-Sukuma wakiwa waajira wenzangu. Nitawaelezea kama A na B.
A alikuwa ni kaka wa miaka 30-34 na wakati ule alikuwa kati kati ya research ya PhD yake, kwakweli huyu tulimuona kama kaka mkubwa, alitupa ushauri na alipenda sana tusome. B alikuwa kati ya 24-25 yeye ndiyo alikuwa amemaliza tu USDM, huyu nilikuwa karibu nae Zaidi kwani umri wetu kwa wakati ule haukuwa umepishana sana pia wote tulikwa wa-Katoliki hivyo tulikutana kanisani mara nyingi. Maka wote wawili hawa hawakuwa wanywaji wa pombe.
Mimi na B tulikula lunch pamoja, na J2 baada ya misa kulikuwa na mkahawa tulipata kifungua kinywa. Akiwa bado hajaoa alikwa ananiambia akienda nyumbani moja kwa moja baada ya misa J2 inakuwa ndefu. Tuliifupisha J2 kwa kusoma magazeti na kufungua kinywa mpaka saa sita hivi ndiyo kila mtu alielekea kwake. Kwakweli mahusiano yetu hayakuhusisha mapenzi, lakini tulikuwa marafiki wazuri sana.
-Wote wawili walikuwa wachapa kazi, walifanya kazi sana wala hawakujali muda wa kumaliza kazi lakini kusiwe na kipolo.
-Wote walikuwa nadhifu na wakujipenda pia walikuwa na kujisikia lakini pia walikuwa wakarimu mno.
-Hawakuwa watu wa majungu na umbea na walipenda sana elimu.
Hii ya kusikia wa-Sukuma wanao forge vyeti na elimu kwakweli ni mbali na mazoea ya wa-Sukuma niliowazoea.