Ninaumwa ulimi

driller

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
1,116
240
jamani ninaumwa ulimi kwa mbele yani unauma kama kunakidonda hivi...! na nikiupitisha kwenye meno yani ni balaa...! nisaidieni jamani nifanyejeee..>!?
 
Hahaha,badili tabia umenchekesha,lol!
Pole driller. Ndo tatizo la camp, unakua umechoka unakula minyama tu na canned fruits ambazo zimepikwa na hazina vitamin C. Anza kula matunda fresh na mboga za majani, kachumbari pia. Vidonda vya ulimi vikijirudia muone dr kabla fizi hazijaanza kuvimba na kutoa damu. Pole sana.
 
Habari zanu wapendwa,

Naomba ushauri wenu ambao utaweza kumsaidia mtoto wa ndugu yangu ambaye anasoma form 6 lakini amepatwa na ugonjwa usiojulikana wa uvimbe kwenye ulimi kama kaupele kamoja tu yapata kama wiki 3.

Sasa analia kwa maumivu makali sana kiasi cha kushindwa kula anaweza kunywa uji wa baridi tu, sasa wenzake wapo shule lakini yeye ndo hivyo tena.

Tulishampeleka katika hosp kadhaa bila mafanikio tunashindwa kujua huu ni ugonjwa gani na tiba yake inapatikana wapi jamani?

Asanteni sana.
 
Back
Top Bottom