Tatizo letu kubwa kwa maoni yangu ni vyombo vya dola mahakama, polisi, FFU TPDF n.k. Hawa jamaa watapofumbua macho, kubwaga manyanga na kuungana na watanzania katika vilio vinavyohusu maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi na Tanzania, basi hapo ndio utakuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa katika nchi yetu. Lakini sasa hivi watawala wanahakikisha 'kuwalea' vizuri hawa jamaa. Wakinung'unika kidogo tu wameshasikilizwa. Kwa sasa hivi wamewekwa mifukoni mwa CCM hivyo CCM itaendelea kuiweka Tanzania rehani kwa sababu wanajua vyombo vya dola vimo mifukoni mwao.