Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature currently requires accessing the site using the built-in Safari browser.
Ninauliza Nani Kaiweka Nchi ya TANZANIA Rehani?
Jibu sisi Watanzania wenyewe, kwani kwa kutoutumia uhuru wetu wa kupiga kura tunaendelea kulea hao vigogo wasioleleka.Ninauliza Nani Kaiweka Nchi ya TANZANIA Rehani?
Tatizo letu kubwa kwa maoni yangu ni vyombo vya dola mahakama, polisi, FFU TPDF n.k. Hawa jamaa watapofumbua macho, kubwaga manyanga na kuungana na watanzania katika vilio vinavyohusu maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi na Tanzania, basi hapo ndio utakuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa katika nchi yetu. Lakini sasa hivi watawala wanahakikisha 'kuwalea' vizuri hawa jamaa. Wakinung'unika kidogo tu wameshasikilizwa. Kwa sasa hivi wamewekwa mifukoni mwa CCM hivyo CCM itaendelea kuiweka Tanzania rehani kwa sababu wanajua vyombo vya dola vimo mifukoni mwao.