Swenailie
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 240
- 229
Wapendwa,
Nimekuja mnishauri nini cha kufanya.
Mimi ni msichana nina umri wa miaka 26 sasa. Niko kwenye uhusiano ila pamoja na yote kuna kijana nilimuona tangu 2011 akanivutia sana nimemfatilia kila siku naona nazidi kumpenda.
Ninapojitahidi tuwe karibu anaipotezea na mimi sijafunguka sana maana naogopa atanichukuliaje pia najua wazi anauhusiano hicho ndicho kikubwa zaidi kinanifanya nisimuweke wazi ninavojiskia juu yake.
Mimi pia nina mahusiano na ninamuheshimu sana mwenzangu anaenipenda ila ukweli moyo wangu hauko kwake. Nimekaa nae miaka mitatu katika mahusiano nikiamini nitampenda ila ndo hivo tena moyo umekataa.
Japokuwa nafanya kila namna kutomkatisha tamaa ajue nampenda ila kweli moyoni hayumo. Kama unavyoona umri unaenda naogopa kumuacha huyu anaenipenda nisipate mwingine wa kuja kufanya nae maisha ila ukweli ni kwamba moyo wangu uko kwingine.
Wakati mwingine najikuta naumia kwa sababu ya hili. Kibaya zaidi huyu ninayempenda hana mda wowote na mimi najaribu kumtumia message kwenye mtandao wa kijamii ananijibu short sana hadi naumia.
Niambieni nifanyeje.