Ninapangisha Nafasi za Biashara, Kinondoni Muslim | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninapangisha Nafasi za Biashara, Kinondoni Muslim

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MwanaHaki, Jun 15, 2011.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  WanaJF

  Ninapangisha sehemu mbili za biashara kwenye eneo la maduka na ofisi (BAKWATA Commercial Complex) lililopo Kinondoni Road, kwa jina lingine, Kinondoni Muslim.

  Nafasi ziko mwanzoni kabisa, mara tu baada ya kupita Kivulini Bar, ukitokea Kinondoni Mjini kuelekea City Centre. Ni maduka Namba 1 na Namba 2. Haya yana nafasi kubwa kidogo, takriban 30%, kwani, familia inammiliki maduka namba 1, 2 na 3, ambayo BAKWATA wanayahesabu kama maduka 4, si 3 kama tulivyoyagawa sisi. Tuliona, awali, kwamba kwa mujibu wa vipimo vyao, ingekuwa tatizo kwa mpangaji kufanya shughuli zake kwani nafasi ingekuwa ndogo iwapo tungeligawa eneo hilo kwa 'frame' 4 kama walivyotaka wao.

  Kimsingi, duka namba 1 nilikuwa nilitumie mimi, lakini kwa kuwa hali imebadilika na sitakuwa hapa Dar muda wote, nimeona niyapangishe yote mawili. Ukitaka kujua ukubwa wake, tembelea duka lolote la hapo Kinondoni Muslim, halafu fikiria ukubwa wa nafasi takriban 30%, ndipo utajua ukubwa wake. Ukitaka kujionea mwenyewe, tutafutane kwa simu, 0786-019019. Leo, kesho na keshokutwa nitakuwa kwenye mikutano, lakini ukinitumia ujumbe mfupi, tutawasiliana.

  Kodi ni TZS 250,000 kwa mwezi, mkataba na malipo ni mwaka mmoja. Hata hivyo, kiwango hiki kinazungumzika, kutokana na kila mpangaji atakavyojieleza. Kwa atakayechukua nafasi zote mbili, atafikiriwa zaidi kuliko atakayechukua nafasi moja tu, lakini, atakayetoa "kifunga uchumba" kiasi cha TZS 2,000,000/=, basi, huyo atapewa punguzo kubwa zaidi kuliko yule ambaye hatakuwa na uwezo huo. Mkataba unaanzia Julai 1, 2011 na kumalizika Juni 30, 2012.

  Shukrani.

  ./Mwana wa Haki
   
 2. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kaka mkata wa laki mbili unusu halafu mwaka mmoja nitautoa wapi mimi wakati mie nalipwa mshahara kwa mwezi?
   
 3. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  waachie wenye uwezo na frem za town we katafute za 30,000 tandika au boko. Vp bia na kitimoto panalipa niweke timu?
   
 4. Fanta Face

  Fanta Face Senior Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo maduka nayafahamu yako mahala pazuri sana ila hiyo bei kaka halafu mwaka
   
 5. u

  ureni JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  sema mashart ni nini?manake wabongo tumezoea mashart,halaf mie nina 150,000 kwa miezi sita nilete?
   
 6. u

  ureni JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hakuna mashart?halafu mimi nahitaji kwa 150,000 kwa miezi sita,sema nilete?
   
Loading...