Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,883
- 5,270
Habarini ya jumapili.
Mimi ni mpenzi sana wa muziki wa taarab asilia. Kwa tafsiri nyepesi, taarab asilia ni muziki wa taarab ulioanza toka miaka ya 1940 hadi hadi miaka ya 1990 mwishoni au 2000 mwanzoni. Taarab hii sifa zake: kimidundo ni kuwa taratibu (low tempo) na kupigwa kwa vyombo halisia vya muziki kama zeze, gitaa, ngoma n.k, kiuandishi/maudhui kutawaliwa na mafumbo na tafsida zaidi. Hii ndio taarab anzilishi kabla ya mapinduzi ya kimapigo yaliyoletwa na kompyuta (higher tempo) na kimaudhui yaliyoletwa na mabadiliko ya kisiasa(ujamaa to ubepari), ya kijamii(influence of western culture) na kuzaa taarab ya kisasa ya kina Mzee Yusuf.
Upenzi wangu umestuck kwenye taarab asili. Ya kina shakila na band yake ya JKT, kina patricia hilary, Egytian musical club n.k.
Kipindi pekee ninachokifahamu kinapiga muziki huu ni Masabkher (kama nimeandika sawia) cha tbc radio. Naombeni kujuzwa ni radio gani tena ina kipindi maalum cha muziki huu.
Asanteni.