Ninalazimishwa kumuoa dada yangu, naombeni ushauri

Hakuna undugu hapa. Kama unampenda na labda hao wanaotaka umuoe wamempenda kwa tabia zake basi oa tu. Undugu huu unaouandika wewe ni wa kuunga na gundi shurti utie mate vinginevyo hata gundi itagoma kufanya kazi.

Habari zenu watu wazito,

Naamini mko salama,

Kuna jambo 1 linaniumiza kichwa kuhusu kumuoa dada yangu kwa kawaida hii aiji akilini kuoa ndugu yako wa karibu wala haileti picha nzuri kabisa.

Wakuu hii iko hivi..
Baba yake, baba yangu mimi alikuwa na shangazi yake ambaye mjukuu wa huyo shangazi aliolewa na mjomba wa upande wa mama yangu lakini akazaliwa mtoto wao wa nje ambaye baadaye akaja kumuoa dada wa baba yangu mimi na huyo mtoto akaja kuoa binamu wa baba yangu na mtoto wa jirani wa mdogo wake dada yake baba yangu alikuwa na watoto wakike mmoja akaolewa na upande wa waarabu na mwingine akaolewa ila hajapata mutoto lakini rafiki yake shangazi wa kaka yake baba yangu mimi ndio nimeambiwa nimuoe.

Sasa huyo nina muona kama dada yangu siwezi kumuoa kwa sababu ni moja wa upande wa ndugu zetu.
 
Hakuna undugu hapa. Kama unampenda na labda hao wanaotaka umuoe wamempenda kwa tabia zake basi oa tu. Undugu huu unaouandika wewe ni wa kuunga na gundi shurti utie mate vinginevyo hata gundi itagoma kufanya kazi.
Ni kweli mkuu huu undugu sio wa kawaida ila nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi.
 
Hii ndiyo jf ya digital na
Uongo wake

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Back
Top Bottom