Ninaipenda Mno CCM Kuliko Nchi Yangu!

Ninaipenda Mno CCM Kuliko Nchi Yangu!

HAPANAAA!!!!

KWA HILI LA KUPENDA CHAMA KULIKO NCHI UMEJIONDOA AKILI.

Haivumiliki huo ni ujuha na wendawazimu,kwetu sisi wenye AKILI TIMAMU,AKILI NZURI KIPAUMBELE NI KUPENDA NCHI YETU TANZANIA KWANZA VYAO BAADAYE.

Nina uhakika umeisoma mada na ukakurupuka kuchangia, ukipewa mtihani unatakiwa usome swali kwa umakini! Nakushauri urudie kuisoma mada utagundua mtoa mada ametumia staili kule kwetu tunaita kisengere nyuma
 
Kuna wanaCCM ambao wapo radhi kuipigania CCM yao vyovyote vile wawezavyo,hata ikibidi kuyaweka maslahi ya nchi pembeni watafanya hivyo.Tumeona kashfa nyingi za ufisadi zilizoiandama serikali ya CCM na jinsi wanaCCM walivyosimama kidete kukitetea chama chao.Wamefikia hatua ya kuwanadi Kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya wahusika wa ufisadi kugombea kuongoza ofisi kubwa kabisa hapa Tanzania ya urais.

Hizi ndizo aina ya siasa tunazozihitaji hapa Tanzania?
Mkuu, title ya thread yako ilinipandisha jazba kali nikaifungua kama kichaa ili 'nikumwagie maji moto' Kumbe si wewe mhusika ila unawasema wengine! Wanaopenda ccm kuliko nchi yao ni wauwaji!Ndio hao mafisadi wanaoimba ndioooooo bungeni.Tutawafanyia kitu moja mbaya sana na halali mwezi oktoba mwaka huu.Tumwombe Mungu tuwepo siku hiyo!
 
Ila ndo hiihii tanzania inawawekeni mjini kupitia ufisadi wenu ccm nyinyi..
 
Lazima kuna pepo flan huwaingia hao watu. Si bure, walikuwepo walioipenda ccm mpaka wakaapa kuilinda kwa nguvu zao zote, wako wapi? Mbona wameiacha?
Ntaipenda nchi yangu Tanzania wala sio Chama chochote kile kwani naweza badilisha chama siwezi badili Taifa.
 
Huna uzalendo.utapendaje chama kilicho fanya madawa yakakosekana mahospitalin.wamafunzi wanakaa chin.watu wanakwapua pesa wanaachwa tu kama kuku wa kienyeji.jifunze kua mzalendo wa nchi yako kwanza,chama baadae
 
Back
Top Bottom