Ninahitaji nafasi ya kufanya 'Internship'. Nimesoma Bsc In Telecommunication CCNA(R&S) Certificate

Nimeshaitumia gia hiyo pale kiwanda cha cocacola mwenge kumuona HR na nilifanikiwa wewe unavaa smart tu ,ukifikaa tu pale unasema na shidah ya kuonana Fulani onyesha confidence ya hali ya juu ikiwezekana vaa Pete ya ndoa , beba kama notebook tatu hivi kubwa kubwa na mafile kadhaa ,kama una suti weka na moka ng'alisha vizuri kma huna gari tafuta funguo nyinginyingi kama za gari hivi weka kiunoni zining'inie miwani safiii kabisa tafuta kitambulisha chenye kamba weka shingoni ionekana kamba tu .ukifika jifanye kama uko busy kidogo ukifika omba kitambu cha mahudhurio hicho muhimu then omba kuonana na Fulani kwa cheo chake akikuuliza tu unashida nae gani jibu kwa kifupi ni confidential tulia usiongee kitu .kama akikwambua unaapointment nae we weka poz kidogo mwambie tu kama hayupo naomba nisaini niondoke . halo watajua wewe so wamchezo mchezo ni MTU wa shughuri yako .
te teh eh hapa hachomoi mtu ningeitumia sana hii kama mambo yangekua hayaja nyooka
 
John locke kwa mtizamo wako ni utumwa ,ila kwangu mimi naona ni fursa ya kujijenga zaidi practical,sina watu labda nitasema watanisaidia connection au kunishika mkono ,nimeona hii ni sehemu ya kuanzia na sipendi kukaa bure nyumbani mda mwingi.Nina marafiki wanne mmoja alikuwa anapiga intern Tigo,wawili huawei,mwengine msalaba mwekundu hawa wote wameajiliwa na wameanza kama intern na hata jeshini haupewi nyota utaanza JKT (utalima wee) ,utakuwa private alafu ndio unapewa nyota na mimi nimekubali kuanzia chini na hata kama sitapata kazi sehemu hiyo basi knowledge ,skill na experience zitanisaidia mbele ya safari.MAISHA NI KUCHAGUA ,na mimi ndio nimeamua kuchagua njia hii najua nitafika,japo nitachelewa ila kufika nitafika.
Asikuzingue, siku hizi dunia nzima kuna volunteering kwa wasomi wapya na hawalipwi. Sisi tu hapa ndio tumechelewa
 
Nilikuwa naomba nafasi ya internship (bila malipo),katika kampuni hizi za networking nina degree ya Telecommunication engineering na vile vile nina CCNA certificate (Routing and Switching).Vitu vingine ninavyovijua
- LAN switching configuration and troubleshooting.

.(VLAN,Intervlan,DTP,VTP,Etherchannel (PAgP,LACP))

-Configuration and troubleshooting of routing protocols (Static route, RIP, EIGRP, OSPF,
ISIS, and BGP).

-NAT configuration and troubleshooting (Dynamic and Static).

-Routing Distribution configuration and troubleshooting.

-Configuration and troubleshooting of MPLS-VPN (mVPN, MPLS-TE).

-L2VPN (Frame relay over MPLS, PPP over MPLS, HDLC over MPLS and Ethernet over
MPLS (VC-type 4 and VC-type 5)).

-DMVPN (IPSec, NHRP) configuration and troubleshooting.

-Redundancy and load balance (HSRP, VRRP, and GLBP) configuration and
troubleshooting.

-Multicast configuration and Troubleshooting (IGMP, BSR, PIM SPARSE-MODE AND
DENSE-MODE).

-Frame-relay configuration and troubleshooting.

-Access control standard, extended, reflexive, context based access control, Time-based
ACL, Dynamic ACL and ZBF configuration and troubleshooting.

-VPN configuration and troubleshooting.

-Wireless configuration.

-ASA firewall configuration and troubleshooting (NAT configuration, IPSec VPN and
configuring firewall failover (active/standby failover, active/active failover), single
context and multiple contexts).

Vyote hivi nimeconfigure kwa kutumia software (GNS3 ,packet tracer).
Hongera kwa kua juhudi kwa icho ulichosomea..Mungu akakupe hitaji la moyo wako
 
Nyie jamaa mnaosomaga izii koz ngumu vyuon mnajionaga sana superior, dharau nying kwa wenzenu wanao soma mambo mengine,,,, nashangaa mnahaso kama sis tuu kwa mtaa kutafuta ajira,,,,,,, maisha hayan formula mungu ndo anapanga,,
Inferiority complex....
 
Nenda airtel, Voda au Tigo
Nimeenda hizo sehem zote, wanamajibu ya kukatisha tamaa na wengine hata hiyo CV yako hawaichukui,mm ngoja ni deal na hizi kampuni ndogo ndogo za networking,kidogo wanapokea ijumaa nilipeleka sehem mbili leo naenda COSTECH
 
Nimeenda hizo sehem zote, wanamajibu ya kukatisha tamaa na wengine hata hiyo CV yako hawaichukui,mm ngoja ni deal na hizi kampuni ndogo ndogo za networking,kidogo wanapokea ijumaa nilipeleka sehem mbili leo naenda COSTECH
Huko nenda kwa mtu specific... Nijuwacho, ukifuata process iliyowekwa, wengine unaokutana nao kwenye process hiyo ni shida... Ntakupa namba ya mtu PM umcheck
 
Jombaa danganya chochote kile uonane na HR aisee....mapokezi hakuna barua inayofanyiwa kazi....
 
Nimeshatuma kampuni kama mbili,ila kuna baadhi ya kampuni (nilizo jaribu kutuma) ukipeleka barua yako, unachoambulia ni kejeli na maneno ya kukatishana tamaa kutoka kwa walinzi na wasichana wa mapokezi ,sometimes unalazimisha wanaipokea lakini unaona kabisa hawatoifanyia kazi .Kama kungekuwa na njia rahisi (hata email) ya kukutana na HR nahisi ingesaidia lkn wale walinzi na mabinti sina hamu nao.kuhusu Labs bado naendelea kufanya sana routing ,switching na security na hivi sasa nimeshadownload vitabu kwa ajili ya kusoma python na juniper.

Nakupa hii mbinu ukifika kwenye ofisi husika usiwaambie unatafuta kazi wala kujitolea waambie unahitaji kuonana Na mkuu wa kutengo unachotaka kufanyia kazi wakikuuliza unatoka kampuni gani waambie we n mtaaluma wa kujitegemea unataka ufanye partnership nao hapo chini na walinzi Na masecretary itakuwa imepungua kama sio kuisha
 
Nakupa hii mbinu ukifika kwenye ofisi husika usiwaambie unatafuta kazi wala kujitolea waambie unahitaji kuonana Na mkuu wa kutengo unachotaka kufanyia kazi wakikuuliza unatoka kampuni gani waambie we n mtaaluma wa kujitegemea unataka ufanye partnership nao hapo chini na walinzi Na masecretary itakuwa imepungua kama sio kuisha
Ok
 
Mkuu kwa CV hiyo haswa CCNA ukienda kuomba intern pale Simbanet watakupa and after one month wanakuajiri...! huwa wanatakaga sana mwenye CCNA au CCNP...
 
Mkuu kwa CV hiyo haswa CCNA ukienda kuomba intern pale Simbanet watakupa and after one month wanakuajiri...! huwa wanatakaga sana mwenye CCNA au CCNP...
Nishawatumiaga kwenye email yao lakini naona kimya hawajanijibu.
 
Back
Top Bottom