Nina wazo zuri la kipindi cha Televisheni ambacho naamini kitakuwa na watazamaji wengi siku moja kwa wiki. Je, nifanyeje kuuza hii idea?

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Leo wakati nawaza kuhusu vipindi kadhaa vya television Tz nikajikuta napata aidia ya kipindi kizuri sana ambacho naamini kikisimamiwa vizuri basi channel husika itatazamwa sana.

Lakini nataka hili wazo niliuze kwa mmiliki wa TV, channel au media yoyote ambayo inarusha Maudhui kwa Kiswahili Tanzania kwa njia ya picha mjongeo.

Kama nikikosa watu wa kukubaliana nao hilo wazo nitaliweka hapa jukwaani kama lilivyo Ila nitaomba jamii forums wanilinde ili watakaokopi walipe halo baadaye.

Nawakaribisha.
 
Siku hizi ni ngumu kuuza idea mkuu, we fanya kutengeneza Demo, peleka kipindi clouds au wasafi muingie maubaliano kuwa kikiruka kikapata wadhamini mtagawana mapato au utakuwa ukilipia airtime.

Kama idea wengi wanazo ni ngumu sana kubadilisha idea kuwa kitu halisi, tengeneza demo kwanza. Unaweza kuimagine kitu flani lakini kukiweka wenye uhalisia ukashindwa, na hakuna kitu kigumu kama kutengeneza muendelezo wa vipindi bora vya TV.
 
If wishes were horses even beggars would ride.

Kama mawazo yangekuwa Benz basi hata ombaomba wangeendesha.
 
Wazo zuri! Yaani uwaze mwenyewe then u-prove ni zuri mwenyewe!

Kisaikolojia hii tunaita "Mental Built in disorder " One Mental idea can't be proved good unless other Mental say so!!

Mawazo yote ya binadamu yeye huzani yapo sawa!

Mfano: Anaewaza ukahaba huita wazo zuri, anawaza kuvuta bangi huita wazo zuri, anaewaza kuiba kura huita wazo zuri!

kwahiyo Hicho kipindi chako Nina mashaka nacho
 
Siku hizi ni ngumu kuuza idea mkuu, we fanya kutengeneza Demo, peleka kipindi clouds au wasafi muingie maubaliano kuwa kikiruka kikapata wadhamini mtagawana mapato au utakuwa ukilipia airtime. Kama idea wengi wanazo ni ngumu sana kubadilisha idea kuwa kitu halisi, tengeneza demo kwanza. Unaweza kuimagine kitu flani lakini kukiweka wenye uhalisia ukashindwa, na hakuna kitu kigumu kama kutengeneza muendelezo wa vipindi bora vya TV.
Huko atapigwa tu.

Bora afe na idea yake.

Hap jamaa ni MAHARAMIA WALIOKUBUHU.
 
Huko atapigwa tu.

Bora afe na idea yake.

Hap jamaa ni MAHARAMIA WALIOKUBUHU.
Unajua mkuu kwa hali ilivyo ni afadhali utake a risk, kwasasa hakuna mtu anaweza kununua wazo. Inabidi utengeneze demo na kama demo ya kipindi ni nzuri mtu akashawishika, kwa competetion iliyopo kwenye TV sasa kila mtu anataka watazamaji, sidhani kama mtu anaweza kukupiga. Unajua vipindi vya TV na movie ni kama studio na producer. Ninaweza kukupa wazo langu lakini usilifanye kama mimi.

Na unaweza kuwa na wazo lakini usilifanye kama ulivyokuwa unaliimagine.

Mfano kile kipindi cha Qwisa cha ndani ya kiza, kile anachoonyesha ni chini ya kiwango ya alichokuqa ana imagine. Ninadhani alitaka kutengeneza kitu kama cha channel za crime and investigation, yani mtu anahadithia halafu yanaonyeshwa matukio mpaka mtazamaji anahisi labda ni uhalisia. Lakini ndo hivyo budget, na utaalam kikaishia kuwa vile.
 
Mkuu nakushauri either anzia YOUTUBE, au tengeneza synopsis then itumie kwenda kuombea wadhamini.

Television nyingi bongo hazina content, muda mwingi wanapiga muziki hivyo ukienda kupeleka idea yako utaporwa na hakuna kitu utafanya.

Ukijifanya kujitetea, hao watu wana kundi kubwa la misukule itakuATTACK kuwa unatafuta KIKI.

Baghdad ana jina kubwa ila check anavyohangaika na idea yake ya The Bartender kutaka kuporwa na Wasafi media.

Ruge mwenyewe kapora sana idea za vipindi vya watu. Unaenda unawasimulia wanakwambia, they're not interested, ukitoka baada ya wiki unashangaa kitu kinaruka hewani kama kilivyo na wewe hukushirikishwa.
 
Unajua mkuu kwa hali ilivyo ni afadhali utake a risk, kwasasa hakuna mtu anaweza kununua wazo. Inabidi utengeneze demo na kama demo ya kipindi ni nzuri mtu akashawishika, kwa competetion iliyopo kwenye TV sasa kila mtu anataka watazamaji, sidhani kama mtu anaweza kukupiga. Unajua vipindi vya TV na movie ni kama studio na producer. Ninaweza kukupa wazo langu lakini usilifanye kama mimi. Na unaweza kuwa na wazo lakini usilifanye kama ulivyokuwa unaliimagine.
Mfano kile kipindi cha Qwisa cha ndani ya kiza, kile anachoonyesha ni chini ya kiwango ya alichokuqa ana imagine. Ninadhani alitaka kutengeneza kitu kama cha channel za crime and investigation, yani mtu anahadithia halafu yanaonyeshwa matukio mpaka mtazamaji anahisi labda ni uhalisia. Lakini ndo hivyo budget, na utaalam kikaishia kuwa vile.
Mkuu issue siyo kutake Risk. A wiseman takes calculated risks.
 
Mkuu issue siyo kutake Risk. A wiseman takes calculated risks.
Mkuu siku hizi hapa tz hakuna mtu unaweza kumuuzia mawazo. Ngoja nikwambie wazo ambalo tulikuwa nalo toka mwaka 2010 ni hili la mpesa na Airtel Master card, tulipambana nalo mpaka tigo na voda lakini majibu ni kwamba hawanunui mawazo, tutengeneze demu ya wazo. Mwisho tukaachana nayo kwanza ndo tulikuwa tuko chuo hata pesa hatuna.

Hata mimi siwezi nunua wazo la mtu mpaka uniletee demo maana wazo ni wazo tu.
 
Unajua mkuu kwa hali ilivyo ni afadhali utake a risk, kwasasa hakuna mtu anaweza kununua wazo. Inabidi utengeneze demo na kama demo ya kipindi ni nzuri mtu akashawishika, kwa competetion iliyopo kwenye TV sasa kila mtu anataka watazamaji, sidhani kama mtu anaweza kukupiga. Unajua vipindi vya TV na movie ni kama studio na producer. Ninaweza kukupa wazo langu lakini usilifanye kama mimi. Na unaweza kuwa na wazo lakini usilifanye kama ulivyokuwa unaliimagine.
Mfano kile kipindi cha Qwisa cha ndani ya kiza, kile anachoonyesha ni chini ya kiwango ya alichokuqa ana imagine. Ninadhani alitaka kutengeneza kitu kama cha channel za crime and investigation, yani mtu anahadithia halafu yanaonyeshwa matukio mpaka mtazamaji anahisi labda ni uhalisia. Lakini ndo hivyo budget, na utaalam kikaishia kuwa vile.

Kipindi cha Kwisa ni copy and pasting ya vipindi flani vya Kenya ambavyo wao huonesha Historia za Maisha ya watu maarufu kwa mfumo wa maigizo huku muhusika akihadithia. tofauti na mfumo wa vipindi vya crime.

Back to Mada, Idea nzuriiii wala sio issue naamini hata wengi wanazo ila tatizo ni kuangalia watu gani wanaweza kuwa sponsors wa vipindi.

Hata uwe na kipindi kizuri vipi na kiki kiasi gani kama hakiwezi vutia sponsors kuweka pesa yao ni kazi bure.

Media zinahitaji content lakini kwa kipindi hiki kigumu pia zipo desperate kupata pesa. Ukiwa na wazo zuri na kuweza kupull sponsors unaweza kununua airtime mwenyewe TV station yoyote ila ukiwategemea bila hii kitu. Utaona unakaziwa.
 
Kipindi cha Kwisa ni copy and pasting ya vipindi foani vya Kenya ambavyo wao huonesha Historia za Maisha ya watu maarufu

Back to Mada, Idea nzuriiii wala sio issue naamini hata wengi wanazo ila tatizo ni kuangalia watu gani wanaweza kuwa sponsors wa vipindi.
Hata uwe na kipindi kizuri vipi na kiki kiasi gani kama hakiwezi vutia sponsors kuweka pesa yao ni kazi bure

Media zinahitaji content lakini kwa kipindi hiki kigumu pia zipo desperate kupata pesa. Ukiwa na wazo zuri na kuweza kupull sponsors unaweza kununua airtime mwenyewe ila ukiwategemea bila hii kitu. Utaona unakaziwa
Hata hajacopy kutoka kwao, maana na hao wa kenya wamecopy kutoka vipindi vya nje sasa sijui na hao wa nje walicopy kutoka wapi
 
Hata hajacopy kutoka kwao, maana na hao wa kenya wamecopy kutoka vipindi vya nje sasa sijui na hao wa nje walicopy kutoka wapi

upo sahihi, Hata clouds, wasafi na wengine wengi content zao zote wanacopy za nje

na radio na Tv za mikoani nao wanacopy hizi media houses kubwa

Tatizo ni moja, Hizi media nyingi wanaajiri kwa kujuana sana kimjini mjini au kidogo kwa mtu ambaye yupo katika cycle ya media au entertainment industry tayari..

Huwa hawana system za wazi za kuvumbua vipaji vipya ndio maana utakuta kuna challenge za kutafuta watangazaji tu ila sio content makers..

Hapo ndo tatizo huanza mkuu
 
East africa wanachukua vipaji toka redio za mkoa wanavikuza vinawakimbia. Ila kitu ambacho I am sure, ukiwa na pesa ukatengeneza kipindi kizuri ukanunua airtime ukapta wadhamini basi unapiga pesa. Mfano kipindi cha redio cha njia panda, japo ilikuwa back then kipindi sebastian ndege aliendelea kuwa ndiye mwenye nacho akawa analipia airtime na clouds hawakuweza kukimwibia.
 
Aisee ,

Aina ya wazo langu wala halihitaji vitu vingi sana

Ingawa kwa jinsi lilivyo kuna mahali linagusa, na kuna watu wanaguswa kwa namna ambayo itawafanya watake kutazama kila wiki...
Kwa namna hii aidea ilivyo content yake ni endelevu.

Anyway bado nasoma ushauri wenu
 
East africa wanachukua vipaji toka redio za mkoa wanavikuza vinawakimbia. Ila kitu ambacho I am sure, ukiwa na pesa ukatengeneza kipindi kizuri ukanunua airtime ukapta wadhamini basi unapiga pesa. Mfano kipindi cha redio cha njia panda, japo ilikuwa back then kipindi sebastian ndege aliendelea kuwa ndiye mwenye nacho akawa analipia airtime na clouds hawakuweza kukimwibia.
Hata salama kwa sasa anafanya kununua airtime tu sababu brand yake inaweza kumpatia sponsor popote. Ila kama ni mtu unaeanza bhasi uwe na demo au hata kitu kama social media account ambayo inaweza kumvutia sponsor kuweka pesa yake maana hawa watu wanapenda numbers sana. Kuwekeza pesa yao kwenye idea tu ni risk kubwa.
 
Siku hizi ni ngumu kuuza idea mkuu, we fanya kutengeneza Demo, peleka kipindi clouds au wasafi muingie maubaliano kuwa kikiruka kikapata wadhamini mtagawana mapato au utakuwa ukilipia airtime.

Kama idea wengi wanazo ni ngumu sana kubadilisha idea kuwa kitu halisi, tengeneza demo kwanza. Unaweza kuimagine kitu flani lakini kukiweka wenye uhalisia ukashindwa, na hakuna kitu kigumu kama kutengeneza muendelezo wa vipindi bora vya TV.
Mbona unamkatisha tamaa mzee kwani unaijua uwezo wake?? Ni ngumu kwako sio kwa wote binadamu hatupo sawa mkuu
 
Back
Top Bottom