Nina wasiwasi na kamati inayoundwa na Bunge kuichunguza Tanzanite-Mererani

Nsibhwene

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
293
217
Kumekuwepo na mchakato wa Bunge unaendelea ukilenga kuchunguza mgodi wa tanzanite mererani.
Hofu yangu ni kutokana na uadilifu wenye mashaka juu ya Bunge letu tukufu ambalo kwa muda mrefu limeshiriki kuhalalisha nchi kufisadiwa na wajanja.
Napata mashaka iwapo nyuma ya muvi hii kama kuna nia njema hasa kwa maslahi Mapana ya Taifa.
Katika hali ya kawaida, bunge lenye wabunge makini kamwe wasingeweza kumpa Mwenyekiti mwenye sifa za chenge aliongoze bunge.
Kwa muktadha huo, ninakuwa na mashaka iwapo kamati hiyo haina nia ya kum pre-empty JPM asitie mguu wake mererani na hatimaye kugusa maslahi ya mafisadi.
Mbaya zaidi JPM naye kaamini kwamba kamati ya bunge itatoka na kitu cha maana. Hamna kitu pale, JPM.
Unda timu yako nyingine maana kama ulivyogundua kuwa vita ya uchumi ni ngumu, mimi naamini kwamba hawa jamaa wa bunge wanania ovu. Walisubiri nini miaka yote kuunda kamati za aina hii hadi wasubiri umeanzisha mapambano ndio watangulie kuunda kamati zao.
Mienendo ya wabunge imetufanya tubaki na imani kwa Kiongozi wa nchi tu.
Imulike kamati ya bunge na wasiachwe kufanya kazi wenyewe. Kila atakayeingia kwenye kamati husika awe under surveillance katika kipindi chote cha uchunguze. Wasitufanye watz tutaendelea kurogwa muda wote. Tumepata mganga, ambaye ni JPM jemedari wa majeshi.
Hajui kumung'unya wala kupepesa.
Kanyaga twende
 
Back
Top Bottom