Nina umri wa miaka 30. Sitaoa ndani ya miaka 20 ijayo

elishaezekiel

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
563
1,461
Nakubali mwili una mahitaji yake lakini akili pia ina mahitaji yake.

Mahitaji ya mwili most of the time huizidia akili na akili nayo kukubali kutawaliwa na mwili, hii ni kwa wengi wetu kama siyo wote.

Natambua nguvu ya uhitaji wa ngono kwa watu wote-wanawake na wanaume ijapokua wanawake huplay sana game ya passivity na kuact as if Ngono kwao siyo a big deal. Katika kuhusiana kwangu na wanawake nimethibitisha pasi shaka kuwa wanawake wanapenda Ngono kuliko wanaume.

Lakini wanaume uhitaji wetu kingono umetuingiza kwenye mahangaiko makubwa ya maisha na umetunyima fursa nyingi kwa kujikuta tumeanzisha hata familia bila kuwa tayari au namtu ambaye baadae unagundua siyo type yako.

Unakuta mwanamme anaahirisha fursa nyingi ambazo zingemuendeleza yeye binafsi au inamuwia vigumu hata kuondoka sehemu moja kwenda sehemu nyigine ya Dunia kwa sababu hayupo peke yake... tayari anajikuta anawatu wanamtegemea.

Naamini Mobility kwenye hustle za maisha inategemea na kiasi gani upo Huru, Upo mwenyewe kiasi kwamba ukiwa Mwanza au Mbeya au South Africa au Misri au Ulaya ama Marekani au Asia huna chako cha kuhofia kupoteza huko nyuma ulikokuacha ama hakuna Mtu wa kukuliza upo wapi ama unarudi lini. Hii ni Ngumu kwa mtu aliye fungwa na Pingu za maisha.

Neno lenyewe Pingu linaeleza wazi haupo huru. Sigmund Freud aliwahi kusema “ All Energy is sexual” Katika muktadha huu ninaouzungumzia naweza kumwelewa Freud na kutafsiri hivi “Mahangaiko yote ya Watu ni ili watimize mahitaji yao ya ngono au matokeo ya Ngono zao”

Basi kwa kufanya hivyo nitakuwa na uwezo wa kufanya mambo yangu kwa Uhuru zaidi, kuepuka Kero, Kuepuka Usumbufu wa Kuhangaika kwa ajili ya mtu badala ya kuijali zaidi Nafsi yangu ,Kuepuka Kumilikiwa na mtu as if umekuwa Mali yake, Kwa sababu Mtu siyo mali ya Mtu.

Utakuta mtu anakuita” My” ama “Wangu” bila kuelewa uzito wa hayo maneno ya Umiliki. Mtu ni raia wa ulimwengu unaweza ishi popote na kati ya watu bilion 7 mtu hajazaliwa ili ajiattach na mtu na kusema huyo mtu aliumbwa kwa ajili yake.

At 50 nitaassess tena uhitaji WANGU wa kuongeza miaka 20 mingine.
 
Mmmmh! Umri wa kuoa ukitimia nachojua utaoa hata bila kuambiwa na yeyote au kulazimishwa!

Mind you, umri wa kuwa tayari kuoa na kuanzisha familia sio sawa na umri wako wa miaka like 30, 32...... ila tu ni ukubwa na utayari wa kuwa huko!

May be you are destined to marry at 50 and that will be your time bro.........Enjoy tu kwanza aiseee maisha yenyewe mafupi haya na dunia unadhani yetu basi
 
Hasara kwa nani?

Life expectancy ni miaka mingapi?

Oa mapema, zaa mapema upate kuwalea watoto na kuspend muda na wao na kuwawekea msingi mzuri wa maisha.

There is no joy like having little babies of your own and coming home to their little hugs and laughter.

Kuitwa My Wangu kusikusumbue akili utamfundisha hata Mdada wa kazi akuite My Boss Wangu.
 
Kwakuwa akili yako unadhani maisha ni kutembea duniani kote......Hilo Ni la kwako hukatazwi kila mtu anakipaumbele chake.

Wengine kwao maisha ni kuwa na mke na watoto na hufurahia sana kukaa nao nyumbani hata kama kijijini

Kama ilivyokuwa kwa Magu yeye kwenda nje haikuwa ladha yake.

Lakini wapo watu wanaosafiri na kuzunguka na familia zao.

Acha ubinafsi uliokomaa.
 
Mmmmh! Umri wa kuoa ukitimia nachojua utaoa hata bila kuambiwa na yeyote au kulazimishwa!
Mind you, umri wa kuwa tayari kuoa na kuanzisha familia sio sawa na umri wako wa miaka like 30, 32...... ila tu ni ukubwa na utayari wa kuwa huko!
May be you are destined to marry at 50 and that will be your time bro.........Enjoy tu kwanza aiseee maisha yenyewe mafupi haya na dunia unadhani yetu basi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi nondo ulizompa kama namuona hapo alipo alivyokua mpole
 
Ukiona ndoa inakufanya ushindwe kufanya fursa za maana kwa kuhisi unamilikiwa ,ujue bado unasafari ndefu ya kukua.
Ila kuna mdau hapo amesema ndoa si kwaajili ya kila mtu ,nawewe labda ni miongoni mwa hao (si kila mtu).ishi upendavyo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Huo mtazamo wake wa maisha tafadhali uheshimiwe

Huna ithibati ya kuukejeli sababu maisha yake atayaishi yeye sio wewe.

By the way sio lazima tufuate pattern zile za kimaisha katika jamii kila mtu huchagua lililojema kwake.

Mwenye kutaka kuoa aoe, asiyetaka akae bachelor sio ugomvi ,majivuno,Tambo na kukejiliana.

Maisha ni uchaguzi kila mtu Ana chaguo lake

Aheshimiwe
 
Ku

Hakuna aliyekejeli mtazamo wake kiongozi ,naona umeisoma comment yangu kwa mtazamo tofauti pia... Hujawahi ona mtu anaoa akiwa na miaka 50 na bado anafika hadi miaka 80 (hiyo ndomaana ya safari ndefu ya kukua ) don't take it personal aise

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom