Nina uhakika simu yangu imedukuliwa

Nina uhakika simu yangu imedukuliwa

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,863
Reaction score
7,059
Mimi huwa sikubaliani na roho ya HOFU na siipagi nafasi kabisa katika mazingira yoyote yale.

Niliwahi kugongana na watu wasiojulikana wakachukua simu yangu kwa uchunguzi zaidi. Kesho yake nikaenda kuchukua SIM Card nyingine kwa namba ile ile nikijua wazi wataanza kunimonitor. Ilichukua muda mrefu sana mpaka kuja kupata simu yangu.

Siku hizi nikiitumia napata notification kuwa kuna Application inataka kuaccess system without authorization. Pia ninapata viashiria vingi kuwa simu au namba yangu iko monitored.

2019-07-12 21.36.07.png


Yote hayo hayanitishi na naitumia kwa mambo yangu yote hata yale ya faragha ikiwemo kutoa maoni yangu. Kunifuatilia mimi wanapoteza tu kodi zenu. Ninajua fika sina jambo baya ninalokusudia na hilo tu linatosha kunifanya nisihofu lolote.

Ikataeni hofu. Msijirudishe kwenye zama za mawe eti kuhofia loosers fulani watakuwa wana jerk off kupitia mazungumzo yako.
 
Burned phones zinapatikana wapi na ni bei gani?
 
application zote ili ziweze kufanya kazi lazima ziombe access Mfaano whatsapp ili iweze kupiga voice call itaomba uipe permission kwa microphone na ili iweze kupiga picha itaomba permission kwa camera na ili ipate location itaomba kwa gps.

wewe cha msingi angalia ni application gani na inataka permission gani?
 
Mimi huwa sikubaliani na roho ya HOFU na siipagi nafasi kabisa katika mazingira yoyote yale.

Niliwahi kugongana na watu wasiojulikana wakachukua simu yangu kwa uchunguzi zaidi. Kesho yake nikaenda kuchukua SIM Card nyingine kwa namba ile ile nikijua wazi wataanza kunimonitor. Ilichukua muda mrefu sana mpaka kuja kupata simu yangu.

Siku hizi nikiitumia napata notification kuwa kuna Application inataka kuaccess system without authorization. Pia ninapata viashiria vingi kuwa simu au namba yangu iko monitored.

View attachment 1156493

Yote hayo hayanitishi na naitumia kwa mambo yangu yote hata yale ya faragha ikiwemo kutoa maoni yangu. Kunifuatilia mimi wanapoteza tu kodi zenu. Ninajua fika sina jambo baya ninalokusudia na hilo tu linatosha kunifanya nisihofu lolote.

Ikataeni hofu. Msijirudishe kwenye zama za mawe eti kuhofia loosers fulani watakuwa wana jerkoff kupitia mazungumzo yako.
Wewe ni nani embu toa mask usoni
 
Hofu inaleta mauti, hiyo message ni matokeo ya system applications kujaribu kuomba ruhusa ya Kufanya update kwenye simu yako. Inaweza kuwa android OS au applications nyinginezo. Hivyo ondoa hofu, kwanza unapodukuliwa huji kujua, utaona tu mambo hadharani.

Na ingekuwa ukidukuliwa unapewa notification, basi tungekuwa mbele sana ya teknolojia. Hivyo relax kiongozi, ila kuwa mwangalifu tu.
 
Nenda hapo kwenye view apps then weka screenshort ya hiyo apps

Ungejua mazingira ya simu yangu kuchukuliwa ungeelewa kwa nini nilikuja na conclusion hiyo. Kama nilivyosema hainisumbui.

Pia kuna viashiria kuwa hata namba yenyewe iko kwenye uangalizi maalumu kwa sababu hata nikiweka SIM Card kwenye simu nyingine bado kuna vitabia vinanifuata.
 
Hofu inaleta mauti, hiyo message ni matokeo ya system applications kujaribu kuomba ruhusa ya Kufanya update kwenye simu yako. Inaweza kuwa android OS au applications nyinginezo. Hivyo ondoa hofu, kwanza unapodukuliwa huji kujua, utaona tu mambo hadharani.

Na ingekuwa ukidukuliwa unapewa notification, basi tungekuwa mbele sana ya teknolojia. Hivyo relax kiongozi, ila kuwa mwangalifu tu.

Naelewa sana hilo unalosema na mimi siyo mgeni kwenye matumizi ya technology, lol.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom