Nina tiba ya kumaliza umaskini - Prof. Muhongo

Nina tiba ya kumaliza umaskini - Prof. Muhongo

Upanga Mkali

Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
96
Reaction score
83
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu, hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.

Pamoja na mambo mengine, Muhongo alitumia muda mwingi kutoa takwimu hali ya umasikini na utajiri kwa wananchi wa Tanzania, bila kusahau baadhi ya nchi ambazo zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kujikita kwenye kuzalisha wataalamu na watafiti, akiwamo yeye, ambaye si tu ni Profesa, bali pia amebobea kwenye nishati kwa miaka mingi.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya wanachama wa CCM na Watanzania katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria, Musoma Mjini, Profesa Muhongo alisema kwamba anayo tiba ya umasikini wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba anatumia utaalamu wake kwa kusimamia mambo ya gesi, mafuta, umeme, bila kusahau elimu kwa ajili ya kuwakwamua wananchi wake.

"Nchi ina upungufu mkubwa wa takwimu hali inayowafanya viongozi washindwe kujua namna gani wanaweza kuondoa umasikini na kero zinazowakumba wananchi wake, hivyo hata wale wanaosema wanataka uongozi, hawajui wangapi wenye uhitaji.

"Ukiacha takwimu ambayo kwa Dunia ya sasa ni lazima, nchi yetu lazima ijiamini, kuongeza ushindani, kuongeza upendo, bila kusahau rushwa ambayo kwa uhakika inapaswa kupigwa vita kwa vitendo ili nchi yetu isonge mbele," alisema Muhongo.

Kuhusu uchumi, Profesa Muhongo alisema kwamba ni aibu Tanzania kupitwa kiuchumi na Mataifa waliyokuwa nayo sawa, akitolea mfano wan chi za Brazil, China, India na Kenya ambao wao wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye elimu na utafiti.

Alisema nchi ikiwa na watafiti, wananchi wao hawataishi kwa mashaka, huku akisema endapo atapitishwa kuwania nafasi hiyo na kuwa rais wa Tanzania, atahakikisha kwamba anakuza uchumi wan chi kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 10 na 15 kwa kipindi cha miaka mitano hadi 10 ya urais wake.

"Nimeweza kufanya kazi ya gesi na mafuta kwa miaka kadhaa kwenye nchi mbalimbali, hivyo hakika kama chaguo ni wataalamu, basi mimi nastahili kwa sababu sioni mwingine mwenye uwezo wa kutangaza kuondoa kero za Watanzania na jinsi atakavyoziondoa.

"Ndio unaweza kusema utaondoa umasikini kwa wananchi au kuongeza mishahara, lakini ili hilo liweze kufanikiwa kwa vitendo, ni lazima pia katika kipindi cha uongozi wako uweze kukuza uchumi wako kwa kiasi kikubwa, bila hivyo hakuna kitu," alisema Muhongo.

Aidha Profesa Muhongo alisema kwamba Duniani kote nchi zimepiga hatua kwa kuwekeza kwenye wataalamu na viwanda, hivyo Tanzania inapaswa kuangalia namna ya kuwekeza kwenye sekta hizo, bila kusahau sekta ya elimu yenye umuhimu mkubwa.

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alisema kwamba akiwa Waziri wa Nishati na Madini, ndio mtu ambaye alifanikiwa kwa vitendo kutekeleza ilani ya CCM kwa kuhakikisha kwamba vijiji vingi vinapata umeme kwa kuongeza bajeti na kusimamia kwa vitendo wakala wa umeme vijijini (REA).

Alisema kusudio la kuhakikisha kwamba wananchi wake wanaendelea kupata umeme kwa bei nafuu ni kati ya mambo anayoona yanafaa kuongezewa chapuo na usimamizi wa aina yake, hivyo mwenye uwezo wa kulitatua hilo ni yeye.

Chanzo: tanzaniatoday
 
aturejeshee hela zetu kwanza then ndo aje atuletee ngonjera zake
 
Jamaa hana mpinzani huyu lazima achukue hii dollla, maana anaonekana ni mwanamapinduzi wa kweli kwa maendeleo ya mtanzania
 
Wakati akitangaza Nia Pamoja na Mengi aliyoyasema nilivutiwa sana na Takwimu mbalimbali alizokuwa nazo na ukiangalia ni sahihi kabisa huwezi kusema utaleta Maandeleo katika Nchi ilhali hujui takwimu za wakati huu zipoje maana ndizo zitakusaidia kuleta Maendeleo....Lakini Pamoja na mipango yake Je, ataweza kuitekeleza ndio swali kubwa kwetu.
 
Huyu ndo rais ajaye, kuna watu waliona hilo mapema wakaamua kumchafua ila yupo vizuri na watu wameshajua ukweli go Muhongo!
 
Kati ya hao waliojitokeza sioni aliyemzidi hata kwenye hotuba yake kaeleza tatizo, ukubwa wake na kutoa suluhu ya kulitatua
 
Hekimamali ukitaka kujua huyu jamaa ni jembe angalia alichofanya kwa muda mfupi aliokaa wizara ya nishati na madini na mambo makubwa aliyofanya hiyo maana yake ataweza
 
aturejeshee hela zetu kwanza then ndo aje atuletee ngonjera zake

Yeye hajachukua hela za escrow mkuu huyu jamaa jina lake halija appear kokote ,huyu ni jembe na tukiteleza tukimpa mwengne zaidi ya muhongo tujue tumekwisha na tutaendelea kuwa maskini tu
 
Wakati akiwa waziri mgao wa umeme tuliusahau sasahivi kila siku kuna mgao tena bila taarifa
 
Anaweza
Atapitishwa na chama kwenye mchujo wa kwanza
Na akipita ataleta upinzani sana
Subiri uone
 
Hekimamali ukitaka kujua huyu jamaa ni jembe angalia alichofanya kwa muda mfupi aliokaa wizara ya nishati na madini na mambo makubwa aliyofanya hiyo maana yake ataweza
Sema Mh. huyu anaonekana mtu wa Majigambo sana kuna wakati alisema huwa anawapa wenzake hizo tafiti sema wanashindwa kuzitumia..
 
Wakati akitangaza Nia Pamoja na Mengi aliyoyasema nilivutiwa sana na Takwimu mbalimbali alizokuwa nazo na ukiangalia ni sahihi kabisa huwezi kusema utaleta Maandeleo katika Nchi ilhali hujui takwimu za wakati huu zipoje maana ndizo zitakusaidia kuleta Maendeleo....Lakini Pamoja na mipango yake Je, ataweza kuitekeleza ndio swali kubwa kwetu.

Ondoa shaka, huyu mzee ni jembe.... yupo juu halipingiki. Just imagine kipindi kifupi alichokuwa pale wizarani makubwa aliyoyafanya. Tuombe hao CCM wampitishe, mzee mzuri
 
Hayo majigambo sio tatizo, tunahitaji kutumia uwezo wake kulifikisha mbali taifa letu
 
Upanga Mkali

Huyu mtu ni hazina kweli. Acheni utani jamani. Ni mtu ambaye hata leo mkisema tumtose ila ipo siku lazima mtakuja jutia na hata vizazi vya badae vitakuja kutuuliza kama tulikuwa na akili timamu au la. Hii ni kwa wote CCM na UKAWA, sijaona mtu kama huyu kwa kweli.
Mtangaza nia yeyote aliyeshindwa kuongelea tatizo la siasa kila mahali,porojo na uvivu wa watanzania huyo hataweza kuja kuliondoa tatizo lililopo la umaskini wa Tanzania na hapo ndo aliponikosha huyu mtu kwa sababu ndo pekee aliyeweza kulielezea hili tatizo.

Nilisomaga mahali fulani ila sikumbuki vizuri waliandika ukimuajili mzimbabwe mmoja ni sawa na wakenya 3 na watanzania 7(mtanirekekebisha mnaokumbuka vizuri). Hii inaonesha ni kwa jinsi gani watanzania tulivo watu wa tantalila na hatuna hulka ya kufanya kazi na kujituma.
Huyu mtu anaitajika pale juu kama kiongozi ili abadilishe hii mindset kwenye jamii yetu.Kingine ni jinsi alivo na facts na alivo realistic, anakwambia kabisa siwezi kuahidi mishaara juu au kitu fulani kabla sijakuza uchumi na akasisitiza kukuza uchumi.

Nilimpenda zaidi aliposema tatizo la wafugaji na wakulima ni teknolojia,aisee hapa alinikosha sana. Kusema kweli tatizo hili dawa yake pekee ni kumpa teknolojia bora mfugaji awe na ng'ombe wachache awafuge kwenye eneo dogo kisasa na apate faida kubwa, same kwa mkulima alime kwenye eneo dogo kisasa na apate faida kubwa. Tukisema kuwaamisha na kuwatengea maeneo kila siku mwisho wa siku nchi yote itageuka jangwa na hata tutakosa kila kitu na kuangamia taifa zima. Mfano tu Morogoro na chalinze tu kulivoanza kugeuka jangwa kwa miti kukatwa na wafugaji.

Tuache utani aisee Prof Muhongo ni hazina ya kipekee ndugu zanguni.
 
Last edited by a moderator:
Hayo majigambo sio tatizo, tunahitaji kutumia uwezo wake kulifikisha mbali taifa letu

Tulifanya kosa kubwa sana miaka 10 iliyopita,kumkubali JK.Sasa mwaka huu,yawezekana tukafanya kosa kubwa sana iwapo CCM itamkataa Pro.Muhongo kupeperusha bendera yao katika uchaguzi mkuu kwenye nafasi ya Uraisi.

Prof.Muhongo ni zaidi ya tunavyomjua wengi wetu.Huyu ni jembe ambalo halijui kuvisha maua penye ukweli.Politic kwake ni platform tu ya kufikia hapo anapopataka,lakini katika uhalisia yeye ni kiongozi wa vitendo zaidi.
 
Jamaa hana mpinzani huyu lazima achukue hii dollla, maana anaonekana ni mwanamapinduzi wa kweli kwa maendeleo ya mtanzania

mimi ni mtu ninawachunguza sana hawa jamaa....

kuhusu Profesa Muhongo....moyo wangu unamtazama hivi kutokana na mambo mbalimbali

1. ni mtu ambaye hufanya kazi na takwimu......na sio porojo. so far sijaona mgombea yeyote ambaye utendaji wake na mikakati yake inazingatia takwimu kama huyu jamaa.....watanzania kwa muda mrefu tumechekwa kuwa tumekuwa interested na matokeo kama vile hospitali na barabara lakini hatujali ni kiasi gani tunaporwa....hii ndio imepelekea wao kuchukua dhahabu sie kutujengea kadispensary....

2. ni mtu ambaye hakubali kuyumbishwa hata na kundi lake ... alichokifanya kuichanachana tanesco mara baada ya kuwa waziri na kuirekebisha ni ushahidi mzuri wa hili......

3. ni mtu anayemg'ang'ania swala wake vema.....tunaweza kupima kwa kuangalia deliverables alizozitengeneza akiwa wizarani....ina maana ana uwezo wa kunganagania mafanikio ya ahadi zake...

4. ni mtu mwenye exposure ya kutosha has kwa concern ya nchi ya wakati huu..gasi na mafuta.....

5. ni kiongozi mzuri....wakati tunapima ubora wa wagombea wetu ni vema tuangalia sifa zao kwa wale wa karibu (anaowaongoza) na wale wanaopokea matokeo au wanufaika (beneficiary),,,,,,,,I swear, katikaa wagombea wote nliosikia sikia umbeya kuhusu wao so far Muhungo amependwa na watumishi woooote waliokuwa chini yake wizarani.....lakini pia amependwa na wananchi aliowatumikia kwa kuweza kuwapatia deliverables wanazozihitaji....................

6. najua wapo wataozungumzia arrogance....shida kidogo ni usmart wa kisiasa...ambalo linaweza kurekebishika.......lakini pia ni ushahidi kuwa uwongo uwongo yeye hapana........

7. anatoka kabila dogo?????

8. naamini kabisa huyu ni Mkapa mwingine.........mtu ninayemkubali sana so far....

naomba kuwakilisha
 
Back
Top Bottom