Nina tatizo la Vidonda mdomoni, Naombeni ushauri

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
14,007
13,799
Habari wakuu,

Kama mada inavyoeleza nina tatizo la vidonda mdomoni hasa kwenye ulimi. Umechubuka kiasi kwamba napata wakati mgumu kunywa chai yamoto au yenye tangawizi na pia vyakula kama dagaa naanza kuviogopa.

Nilijaribu kutumia machungwa na malimao ila vilivyopona ni vya pembezoni ndani ya kinywa ila vya ulimi vimegoma. Nikaenda pharmacy kununua Nystatin, japo ilinisaidia ila ilivyoisha naona kama tatizo linaanza kurudi.

Nisaidieni njia ya kumaliza tatizo kabisa. Siumwi Pangusa wala gonjwa lolote la ngono na #Uvinza sijui hata kuna ladha gani.

Nawasilisha.
 
Ni fangus ndio zinakusumbua. Nyistatin kama dawa ya fangus imedunda, kwahiyo unatakiwa kutafuta dawa ya fungus nyengine yenye nguvu kuliko nyistatin.
 
Acha uvivu wa kula matunda.. Una upungufu wa vitamin C.. Kula machungwa ya kutosha.. Kufikia kesho utakuwa umepona.. Ugonjwa unaitwa scurvy!
 
Umetumia dawa gani mkuu?
Dawa fulani ya kienyeji baba mzazi kanipa. Ni majani yamekaushwa hivyo unayapitisha maji kidogo then unakamua maji yake.Inatoa juisi nyeusi hivi ambayo naipitisha pitisha mdomoni hasa kwenye ulimi kisha nameza.

Mwanzoni kipindi naanza kuitumia ilikuwa inawasha kwa mbali sababu nilikuwa na majeraha mengi kwenye ulimi ila baadaye hata kuwasha ikaacha maana vidonda vilianza kupungua.

Zamani ilikuwa nikiamka asubuhi siwezi kukunja ulimi ila sahivi naukunja hadi unafika kwenye gego.
Naelekea kupona kabisa.
 
Ahsante. Mungu akusimamie.
 
Back
Top Bottom