Nina tatizo la usikivu. Je, ninaweza kusomea kozi gani kuendana na hii hali?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
814
1,057
Tatizo limenianza ghafla mwaka juzi na hali imekua ikiendelea kuwa mbaya kila siku zinavyozidi kwenda...(Nilishajaribu specialist ENT na kufanya matibabu pale Temeke,Ekenywa, AAR lakini sikupata afadhali)

Nilihitimu advance level mwaka jana (Art combination) na sikuanza chuo ila mwaka huu nahitaji kuanza ila bado nina ukakasi wa kuchagua kozi.....(Binafsi yangu nilipenda Sheria ila hali yangu ya kuwa na usikivu hafifu na profession nitakayokua imenifanya nibadili mawazo)

Naombeni ushauri wakuu kwenye hili....ila ukizingatia hali niliyo nayo na profession nitakayokua baada ya kumaliza hiyo kozi
 
Husikii kabisa?

Nina jamaa yangu anasikia kwa mbali sana hata darasani alikuwa hasikii vizuri. Akawa anakomaa tu mwenyewe mpaka PCM akafaulu.

Akaomba chuo cha ualimu, akapangwa Monduli. Alivyofika walivyojua tatizo lake akafukuzwa.

Ila baadaye wakamuita akarudi chuoni, na sasa hivi ameajiriwa huko Njombe kama Mwalimu.
 
Hivi hili tatizo kuanza ukubwani maDk walikuambia chanzo huenda ni nini? I can feel you pambana kibabe
 
Nina Dawa na Nina amini asilimia Mia uta pona uki utumia

Chukuwa maji ya vuguvugu
Mdalasini, na chumvi changanya vyote alafu uchuje yale maji uta kuwa una ya Tumia kwa jimwagilia Toni ya maji ayo maskioni kwa mda wa siku Saba majibu uta nipa
 
Ninakushauri usomee education, ualimu wa watu wenye mahitaji maalumu, najua utajifunza lugha ya alama na utakua mwl mzuri kwa watu wenye shida kama hiyo.

Udom wana hiyo course inaitwa Special Needs Education ni nzuri sana kwasababu ya mazingira rafiki..utapata walimu na wanafunzi wenzio wenye suala kama lako na mtasaidiana na utaweza kufikia pale sehemu unataka kwa urahisi zaidi.

Sehemu nyingi hua na changamoto za ukalimani kwahiyo mafanikio yako yatategemea zaidi uwepo wa hao wakalimani,kama hawapo duuuh ni shida kuna walimu hua wanatembea na slides kama hawajui vile, usikate tamaa kuna mazingira rafiki ya kujifunzia na Mungu akusaidie.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
 
Husikii kabisa?

Nina jamaa yangu anasikia kwa mbali sana hata darasani alikuwa hasikii vizuri. Akawa anakomaa tu mwenyewe mpaka PCM akafaulu.

Akaomba chuo cha ualimu, akapangwa Monduli. Alivyofika walivyojua tatizo lake akafukuzwa.

Ila baadaye wakamuita akarudi chuoni, na sasa hivi ameajiriwa huko Njombe kama Mwalimu.
Mtu anafukuzwaje chuo kisa usikivu hafifu?
Inakuwajekuwaje?
 
Tatizo limenianza ghafla mwaka juzi na hali imekua ikiendelea kuwa mbaya kila siku zinavyozidi kwenda...(Nilishajaribu specialist ENT na kufanya matibabu pale Temeke,Ekenywa, AAR lakini sikupata afadhali)

Nilihitimu advance level mwaka jana (Art combination) na sikuanza chuo ila mwaka huu nahitaji kuanza ila bado nina ukakasi wa kuchagua kozi.....(Binafsi yangu nilipenda Sheria ila hali yangu ya kuwa na usikivu hafifu na profession nitakayokua imenifanya nibadili mawazo)

Naombeni ushauri wakuu kwenye hili....ila ukizingatia hali niliyo nayo na profession nitakayokua baada ya kumaliza hiyo kozi
Taja combination yako tukusaidie mkuu.
 
Mkuu ninashida kama yako na tunagroup whatsap wenye shida za usikivu. Kama unataka unaweza nipatia namba inbox wakuunge huko kwani huko tunashare mengi sana kwa ajili ya wenye hearing loss nk.

Kuhusu cha kusoma degree, kwa ushauri wangu nenda ualimu maalumu pale udom, kama hali ni nzurinzuri ya usikivu bado unaweza omba tu ualimu wa kawaida chuo chochote kama wengine.

Nimekushauri ualimu ili usijeteseka baadae kwenye suala la ajira sababu serikali huwa inatoa nafasi maalumu za ajira kwa walimu wenye ulemavu (walemavu). Naonaga ni kada ya ualimu tu sijui kada zingine.
 
Ninakushauri usomee education, ualimu wa watu wenye mahitaji maalumu, najua utajifunza lugha ya alama na utakua mwl mzuri kwa watu wenye shida kama hiyo.

Udom wana hiyo course inaitwa Special Needs Education ni nzuri sana kwasababu ya mazingira rafiki..utapata walimu na wanafunzi wenzio wenye suala kama lako na mtasaidiana na utaweza kufikia pale sehemu unataka kwa urahisi zaidi.

Sehemu nyingi hua na changamoto za ukalimani kwahiyo mafanikio yako yatategemea zaidi uwepo wa hao wakalimani,kama hawapo duuuh ni shida kuna walimu hua wanatembea na slides kama hawajui vile, usikate tamaa kuna mazingira rafiki ya kujifunzia na Mungu akusaidie.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
Mkuu pole kwa changamoto unayopitia...mawazo haya ☝️ ni sahihi kuyatumia.
 
Tatizo limenianza ghafla mwaka juzi na hali imekua ikiendelea kuwa mbaya kila siku zinavyozidi kwenda...(Nilishajaribu specialist ENT na kufanya matibabu pale Temeke,Ekenywa, AAR lakini sikupata afadhali)

Nilihitimu advance level mwaka jana (Art combination) na sikuanza chuo ila mwaka huu nahitaji kuanza ila bado nina ukakasi wa kuchagua kozi.....(Binafsi yangu nilipenda Sheria ila hali yangu ya kuwa na usikivu hafifu na profession nitakayokua imenifanya nibadili mawazo)

Naombeni ushauri wakuu kwenye hili....ila ukizingatia hali niliyo nayo na profession nitakayokua baada ya kumaliza hiyo kozi
Tupo wengi humu
 
Back
Top Bottom