Nina tatizo la hofu ya kuona au kusikia mkasa uliopelekea watu kupata majeraha

Srinivan Ramanujan

Senior Member
Nov 1, 2019
159
201
Tatizo langu kubwa ni uoga uliopitiliza wa kuona majeruhi au kusikiliza visa vilivyopelekea watu kupata majeraha.

Hali hii imekuwa ikinitesa sana, maana punde tu nisikiapo au nionapo majeruhi moyo wangu unapatwa na baridi kali sana, hofu kupitiliza na nakuwa natetemeka mwili.

Nimegundua hali hii sio ya kawaida baada ya kufanya kautafiti kidogo nimegundua katika sekta hii nazidiwa ujasiri mpaka na wanawake.

Mfano hata nikiwa kwenye daladala halafu nje ikatokea ajali na kuna majeruhi basi mimi nitafunga macho au kuangalia pembeni.

Naombeni msaada jamani maana hali hii inanitesa sana nashindwa kuwa hudumia watu wangu wa karibu wapatapo matatizo.
 
Sikuombei mkuu ila huwa hivo kitu unachopata wasiwasi nacho kwa muda mwingi hutokea ndomana nakwambia kemea na uikatae hio roho

Cc Smart911
Nakuelewa vizuri sana mkuu lakini maneno uumba alafu ukizingatia kwenye reply yako ya juu umetumia "will" though najua hauna maana wala nia mbaya sema nilikuwa nakukumbusha tu, pale ingependeza zaidi ungetumia "might".
 
Huna tatizo. Inategemea malezi na mazingira uliyokulia. Kwa mfano: Mimi pia sina ujasiri wa kutazama majeruhi,hata sijawahi na siwezi kuchinja mnyama yeyote hata kuku! Nahisi uchungu sana kuona mnyama anachinjwa,au mtu akiuwawa. Familia yetu ilikuwa marufuku kutazama horror movies.
 
Huna tatizo. Inategemea malezi na mazingira uliyokulia. Kwa mfano: Mimi pia sina ujasiri wa kutazama majeruhi,hata sijawahi na siwezi kuchinja mnyama yeyote hata kuku! Nahisi uchungu sana kuona mnyama anachinjwa,au mtu akiuwawa. Familia yetu ilikuwa marufuku kutazama horror movies.

Umenifungua kidogo mkuu, shukrani kwa mchango wako maana nilikuwa nahisi kama nina mapungufu flani.
 
Sio mapungufu, ni mazoea yako tu. Na sio lazima kuweza kuangalia, unless unafanya kazi ya kutoa huduma ya kwanza, kubeba wagonjwa au mtoa huduma hospital.
 
Back
Top Bottom