OCD inanitesa, sijui nifanyeje!

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili. Niliishi miaka mingi nikijiona wa tofauti ila niliamini ni jinsi nilivyo tu bila kujua nina tatizo linalowakumba watu wengi tu Duniani.

Nilijua kuhusu OCD kwa mara ya kwanza hapahapa JF kupitia uzi ulioelezea tatizo hilo. Nilichukulia poa kwa kudhani ni jambo la kawaida ila jinsi siku zinavyozidi kwenda maisha yangu yanakuwa ya tofauti na watu wanaonizunguka.

Hali ninazozipata ni:

1. Mysophobia / Germophobia - extreme fear of germs and contamination. Aisee hiki kitu kinanitesa vibaya mno. Nimekuwa ni mtu wa kunawa mikono pale nitakaposhika kitu chochote kile, siwezi kushika kitasa cha mlango kwa mkono mtupu aidha nitatumia karatasi au nikishika basi moja kwa moja ni kuchukua sabuni na kunawa mikono. Kitu kikianguka chini siokoti. Mtu akigusa chakula changu siwezi tena kula hicho chakula. Siwezi kumpa mtu mkono labda iwe ni lazima kufanya hivyo. Nikiwa nakula mkono wangu wa kulia ni maalumu kwa kazi hiyo tu na ikitokea nimeshika kitu chochote kwa bahati mbaya basi nitaacha kula na kwenda kunawa tena. Siwezi kutumia kitu chochote kwenye public toilet, kama ni ndoo nitatumia ya kwangu peke yangu.

Hali hii inanitesa na kufanya kuwa ngumu mimi kuchangamana na jamii na watu wanaonizunguka kwasababu ni ngumu watu kuelewa tatizo nililonalo.

2. False memory OCD - hapa ndiyo tatizo kubwa lilipo. Napata msongo wa mawazo kutokana na matukio yasiyo ya kweli yanayotengenezwa na ubongo wangu. Ninaweza kukaa ghafla tu nikapata mawazo kuwa kuna jambo baya limenitokea wakati uliopita na nitatumia masaa kulirudia hilo tukio kwa kila namna lilivyoweza kutokea nikijua fika siyo kweli mpaka pale nitakapopata ahueni au kuhisi hakuna kilichotokea. Kuna kipindi nilitumia siku 3 mfululizo nikiwa na mawazo tu, ni jambo linalonipotezea muda ila nashindwa kujizuia kabisa. Kwa watu ninaoishi nao huwa naweza kuwauliza maswali ili kupata uhakika wa tukio fulani kutokea na wakinipa majibu yasiyokamilika ndiyo mawazo yanazidi kabisa.

3. Real events OCD - hapa huwa napata mawazo mengi kuhusu mambo niliyowahi kufanya wakati uliopita. Vitendo hivyo huwa vinanipa mawazo nikijihisi nimekosea watu au nilifanya vitendo vya aibu. Matukio hayo huwa yanafanya najutia vitu nilivyowahi kufanya. Ni ngumu kukwepa hayo mawazo kwasababu yanajirudia kila muda ninapokuwa nimetulia.

Mawazo imekuwa ni sehemu ya maisha yangu.

3. Compulsive / repetitive behaviors - vitendo hivi vya kujirudia ndiyo zilikuwa dalili za mwanzo na kujigundua kuwa nina OCD. Mwanzo nilikuwa naona ni vitu vya kawaida tu. Kuosha mikono mara kwa mara, kuhakiki kuwa nimefunga mlango na kuhesabu: namba ninazozihesabu ni 1-7 au 1-10, bila kufanya hivyo nitakuwa na wasiwasi usioelezeka na hata nikihakiki bado ninakuwa na hofu na nashindwa kujizuia kupata hofu. Kuuliza maswali kuhusu matukio fulani ambayo hayajawahi kutokea ili tu nipate uhakika. Kukwepa maeneo yanayopeleka mimi kupata mawazo ya kitu fulani, mahali ninapoishi kuna njia sipiti japokuwa ndiyo shortcut ya kwenda dukani. Nikipita hiyo njia basi mawazo yataanza, sababu wala siyo ya msingi ila nashindwa kabisa kuzuia hilo.

OCD imepelekea maisha yangu ya kijamii kuwa magumu kwa kuogopa kufanya vitu kadhaa nikiogopa matukio mabaya kutokea. Mawazo ndiyo yametawala maisha yangu, nimekuwa mtu wa peke yangu peke yangu tu. Nashindwa hata kuwaeleza watu wangu wa karibu hali ninayopitia kwasababu nahisi hawatanielewa kwa kuona siyo tatizo.

Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo. Ningependa kujua wale wanaopitia hali hii kipi kimewasaidia kupunguza hili tatizo.
 
Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo.
Umejifunga hapa!

Katika kutoa ushauri client ndiye anakuwa na solution ya tatizo lake.

Kama utakubali kuwa unaweza kuchange fanya hivyo kwa kuchukua hatua Mara 1. Maisha ni kujifunza

Kama unaamini huwezi kubali kuishi vile ulivyo. Itafikia watu watakuelewa tu.
 
Unahitaji tiba haraka mno....

Kuna hatua mbili....

1)Psychotherapy....mazungumzo na mshauri tiba ambaye atakuandalia hatua tiba.

2)Madawa yaitwayo Antidepressants.....

Pole sana mkuu na kila la heri katika matibabu hayo ,amen

#DoNotDoHarm
 
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili...
Mgonjwa unasema tatizo si rahisi kuondoka?!!!

Huo ndio UGONJWA wenyewe....

Nimekueleza hapo juu nenda hospitali ukutane na Psychiatrist atakusaidia ila humu utakuwa unatafuta tiba ya mazungumzo(psychotherapy) ambayo si RASMI na hata kama utapewa majibu na wataalamu wa afya ya akili haitokuwa bora zaidi ya kukutana nao....

Kila la heri
 
Mimi nilikuwaga na tatizo la over thinking, na imagine vitu ambayo havipo au kitu nikiwaza natengeneza scenario kibao tatizo hili nililimaliza baada ya kupewa ushauri mdogo tuu kwamba nitafute hobby ninayo penda ninywe bia kidogo niwe na tabia ya kutoka usiku na kutembea maeneo tofauti tofauti na pia nilipewa recomendation ya kusoma vitabu vya napoleon hill haswa haswa outwiting the devil niliacha hiyo tabia na mpaka sasa naishi vizuri una bahati wewe huna aibu mimi kilifika mda naogopa kuonekana nikiwa na tembea naona watu wananiangalia au wananisema
 
Mimi nina tatizo la kula kucha na peni so powa.Vikucha vidogo kinoma na peni zangu zipo kama miswaki kwa juu.
 
Unahitaji tiba haraka mno....

Kuna hatua mbili....

1)Psychotherapy....mazungumzo na mshauri tiba ambaye atakuandalia hatua tiba.

2)Madawa yaitwayo Antidepressants.....

Pole sana mkuu na kila la heri katika matibabu hayo ,amen

#DoNotDoHarm
Asante kwa maoni. Nitaufanyia kazi ushauri wako.
 
Umejifunga hapa!

Katika kutoa ushauri client ndiye anakuwa na solution ya tatizo lake.

Kama utakubali kuwa unaweza kuchange fanya hivyo kwa kuchukua hatua Mara 1. Maisha ni kujifunza

Kama unaamini huwezi kubali kuishi vile ulivyo. Itafikia watu watakuelewa tu.
Nimeichukua hii. Asante kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom