nina swali la interview ya udereva

Master jay

Senior Member
Joined
May 28, 2012
Posts
194
Reaction score
32
nimetoka kwenye usaili wa udereva huku moshi, lkn cha ajabu limeletwa gari lenye ubovu wa gia, usukani kwa ajil ya usaili, hv wadau ndo utaratibu huo kwa kuleta gari lenye matatizo ihal kuna magari mazima?
 
Si ndo wajue gari likikuharibikia utalia na kupiga simu dunia nzima kama snowhite ama utaingia chini ya uvungu kama King'asti?
 
Last edited by a moderator:
Inategemea ndg.
Subiri majibu yako
Sehemu nyingine unapewa gari nzuri na sio bovu ila usali hauna kanuni yoyote.

Tulizana!
 
hv mgari m'bovu, gia zipo shaghala baghala, unapewa udrive dk 2, si lazima ushindwe? Labda kama si interview utaendesha bila mashaka, king'asti
 
Labda iyo ndo interview yenyewe wamekupa gali bovu wakuone je unaweza kumudu au unaweza kundua kwa haraka kama wewe ni dereva kweli!
 
Japo udereva sio fani yangu, lakini ktk hali kama hiyo: Kuwaonyesha kuwa umegundua lina matatizo ya gia, na kuishia kuwaelimisha juu ya madhara ya kuendesha gari likiwa ktk hali hiyo pamoja na kuwashauri nini kifanyike (Kama una ziada ya ufundi - tengeneza kwanza badala ya kuendesha, vingnevyo omba aletwe fundi kwanza); yawezekana ndio kufaulu kipengele hicho cha usaili. Madhara yanaweza kuwa ni kuharibika zaidi kwa gari, ajali na kupoteza/kuathiri nguvukazi na mali, kufunguliwa mashtaka na/au kulipishwa kwa kuendesha gari likiwa ktk hali hiyo....... Hivyo, kama dereva usingeweza kuendesha gari kama hilo kwa kuchelea kumsababishia hasara muajiri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…