Nina shauri utoaji wa leseni za udereva wa magari hasa kwa magari ya usafirishaji mizigo kuwepo chuo angalau kila mkoa

Jan 22, 2023
8
2
Nina shauri utoaji wa leseni za udereva wa magari hasa kwa magari ya usafirishaji mizigo
Kuwepo chuo angalau kila mkoa kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo tofauti na ilivyo sasa ni Morogoro Kihonda au Dar es salaam Chang'ombe pekee.

Hali kama hii inachangia upatikanajia wa leseni nyingi ambazo sio za mafunzo rasmi au halali kwa sababu ya baadhi ya madereva kushindwa kufika vyuo kwa sababu za kiuchumi au kushindwa kuzimudu gharama.

Na hali kama hiyo ndiyo inapelekea ajari nyingi barabarani zinazo sababishwa na madereva wa malori ambao wanaleseni zilizo kosa mafunzo.

Pia ninge shauri askari wa usalama barabarani wanapokuwa wanakagua magari na leseni za udereva wawe wanakagua na vyeti ili kubaini kama kweli wamepatiwa mafunzo na vyuo vinavyotambuliwa na leseni wazi nazo zinafanana na mafunzo husika na iwe kila baada ya miezi mi tatu(3).

Kwa kufanya hivyo naamini tutapunguza ajali nyingi na kuokoa maisha ya watu wetu.
 
Back
Top Bottom