Nina sh 1.5m nataka niwekeze hapa;

Lucky01

JF-Expert Member
Nov 19, 2016
215
250
Habar zenu wanajamvi,natumai mko wazima.
Mimi ni mwanafunzi wa chuo katika mishe zangu nimeweza kufanikiwa kupata faida ya sh 1.5m,nikaona nitumie hii hela kununua mashamba ya miti ya mbao huku Mafinga ambayo yanauzwa kwa sh laki 1.5 kwa miti ya miaka miwili kwa ekari moja so nnauwezo wa kununua around eka 10 kwa hiyo hela ambayo huko mbeleni ninaweza kupata faida kubwa.Naomba ushauri wenu wadau kuhusu changamoto katika biashara hii....
Nawasilisha
 
I and myself

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
319
500
changamoto ya kwanza kuungua moto kwa miti yenyewe.. kama una weza nunua hata heka mbili.. arafu hela nyingine angalia hapo chuoni kwenu biashara gani waweza fanya ambayo haita kuchukulia mda mwingi.. mfano waweza nunua ream paper arf ukatoa karatasi nne nne au tatu tatu ukawa unazunguka kwa wanafunzi wenzio ukawa una wauzia kwa sh mia tatu au mia mbili inategemea na wewe mwenyewe na uwepo wa soko..
 
monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,187
2,000
Kuna jamaa anayauza ntakutumia namba yake PM
Mkuu hiyo issue nilishawahi kuifatilia wiki iliopita nina classmate wangu ana mashamba huko,ila ni Miaka 5-7 kupata Mti,minimum years mengine ni Mpaka 10years.
sijawahi kusikia 2years Mkuu
 
Lucky01

JF-Expert Member
Nov 19, 2016
215
250
Mkuu hiyo issue nilishawahi kuifatilia wiki iliopita nina classmate wangu ana mashamba huko,ila ni Miaka 5-7 kupata Mti,minimum years mengine ni Mpaka 10years.
sijawahi kusikia 2years Mkuu
Ngoja niwaulize majamaa zangu walionunua huko
 
structuralist

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,231
2,000
Ni vigumu kama sio haiwezekani kabisa kuwa na madhamba ya miti inayokomaa ndani ya miaka miwili, please do not raise your hope that much.

Pili umesema umepata faida ya 1.5M ila hukusema ni kutokana na biashara gani na pengine ilikuchukua muda gani kupata hiyo faida. Kama ni biashara halal na ndani ya Muda mfupi umeweza kupata faida ya 1.5M kwanini usiendelee na hiyo biashara? Kwanini usiwekeze zaidi kwenye hiyo biashara?
NB:kwa kusikia na uelewa wakawaida miti huchukua wastani kwa kiwango cha chini kabisa 7 Yrs. Sio muda mrefu ila kwakubwa muda unakwenda sana ila ishu ni pale kitu cha kusubiri miaka 7 wewe uwe na matarajio ya miaka 2 hapo ndipo ishu ilipo ila kama utawekeza ukiwa unajua kuwa it acha kua miaka 7 hakuna shida. Kila la kheri.
 
Mkuu napiga mishe za kilimo cha vitunguu so ni halali na nataka nifanye nifanye kitu kwa sababu sitaki hela yangu ikae tu benki bila kuwa na faida yoyote....ahsante kwa maoni yako
 
Ototo

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
1,120
2,000
Mkuu napiga mishe za kilimo cha vitunguu so ni halali na nataka nifanye nifanye kitu kwa sababu sitaki hela yangu ikae tu benki bila kuwa na faida yoyote....ahsante kwa maoni yako
Mkuu mimi niko interested sana na kilimo nitakutafuta baadae tuzungumze zaidi, kuhusu kilimo cha vitunguu
 
Lucky01

JF-Expert Member
Nov 19, 2016
215
250
Ni vigumu kama sio haiwezekani kabisa kuwa na madhamba ya miti inayokomaa ndani ya miaka miwili, please do not raise your hope that much.

Pili umesema umepata faida ya 1.5M ila hukusema ni kutokana na biashara gani na pengine ilikuchukua muda gani kupata hiyo faida. Kama ni biashara halal na ndani ya Muda mfupi umeweza kupata faida ya 1.5M kwanini usiendelee na hiyo biashara? Kwanini usiwekeze zaidi kwenye hiyo biashara?
NB:kwa kusikia na uelewa wakawaida miti huchukua wastani kwa kiwango cha chini kabisa 7 Yrs. Sio muda mrefu ila kwakubwa muda unakwenda sana ila ishu ni pale kitu cha kusubiri miaka 7 wewe uwe na matarajio ya miaka 2 hapo ndipo ishu ilipo ila kama utawekeza ukiwa unajua kuwa it acha kua miaka 7 hakuna shida. Kila la kheri.
Mkuu labda umenielewa vibaya namaanisha shamba lina miti ya miaka miwili siyo miti inayokomaa kwa miaka miwili........ahsante
 
Smart Technician

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
633
1,000

Hio biashara ni nzuri ila inachukua muda ushauri wangu hakikisha unaponunua aina ya miti yaweza kuuzika
Hakikisha eneo halina vichaka vinene na matukio ya kuchomeana moto mara kwa mara
Hakikisha unaponunua unafaamiana na mtu hata mmoja utakae kuwa unamtumiahela hela kidogo kwa kukulindia
 
Ahsante Sana Mkuu kwa ushauri wako ntaufanyia kazi...ubarikiwe
 
Cute shy

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
1,150
2,000
Naomba mkuu unielekeze hiyo biashara inayokuingizia vizuri, mimi muda ninao, nitashukuru
Hio biashara ni nzuri ila inachukua muda ushauri wangu hakikisha unaponunua aina ya miti yaweza kuuzika
Hakikisha eneo halina vichaka vinene na matukio ya kuchomeana moto mara kwa mara
Hakikisha unaponunua unafaamiana na mtu hata mmoja utakae kuwa unamtumiahela hela kidogo kwa kukulindia
 
Smart Technician

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
633
1,000
Naomba mkuu unielekeze hiyo biashara inayokuingizia vizuri, mimi muda ninao, nitashukuru
Kuna mbinu nyingi za hii biashara kutegemea na aina ya miti
Kama ni miwati
Unanunua miti ikiwa mikubwa unakua unauza rejereja kwa watu wanaojengea kama milunda
Unakua unawauzia wanaochoma mkaa kama wapo katika hilo eneo
Unauza maganda ya miwati bila miti wanachuna huku miti imesimama wanakuachia miti hio miti utauza kama kuni za vigogo vya kupasua na nguzo za fence

Kama ni pines(mipaina)
Nunua miti iliyo midogo alafu kaa kama mwaka au miezi michache nenda mjini unakoishi (najua unaishi mjini ndiyo mana unaipata jf) tafuta mtu mwambie nina miti kijijini naiuza lazima akija nunua utamuuzia kwa bei ya juu
Nunua miti na subiri ikue alafu unapasua mwenyewe na kuuza mbao
Nunua miti mikubwa ipasue weka mbao stoo ikauke ikikauka vizuri bei huwa juu
Nunua miti mikubwa bila eneo ambalo ipo miti usipasue tafuta mtu mjini mpeleke kwenye miti yako muuzie
Tafuta mteja wa miti kabla ya kununua miti akikuambia bei nenda katafute miti kama aliokuambia nunua kwa bei ya chini alafu unamuuzia

Kama ni milingoti
Nunua milefu kama nguzo nenda kwa wanao nunua nguzo wauzie hii huhitaji kupelekewa
Nunua miti mikubwa pasulisha mbao na uza mbao

Nunua miti pasua mbao na uzipeleke mikoa yenye bei nzuri na uziuze(hii usipokua makini faida inaweza isionekane ila ukitulia huleta faida kubwa)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom