Nina mpango wa kurudi darasani nikiwa na umri wa miaka 27 sasa

Vamigo

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
415
Reaction score
851
Bila kupoteza muda mm ni kijana mwenye umri tajwa hapo juu mwenye mke na mtoto mmoja, nawaza kuamua kutatua mgongano WA ki fikra juu yangu binafsi Kwa kuamua Moja, kurudi darasani.

Nilipata four ya 27 mwaka 2015, Sasa nataka nikaitafute elimu ya juu zaid kwakutudia mtihani na kuendelea mbele.

Historia ya elimu yangu mpaka nahitimu kidato Cha nne, niwe muwazi kwamba kwenye masomo yaliyo husiana na mambo ya kikokotozi nilipata f na sina msingi wowote, nikama nilikua nacheza shuleni. Hivyo inanipa ugumu kuamua au kuwa shape wanangu na kuwafundisha pale unapo bidi.

Nitakapo Rudi darasani, nimepanga kuanza na msingi hususani kwenye somo la hisabati, kisha nipate basics ya masomo haya physics, B/math, chemistry na biology Kwa secondary

Kisha A level nijikite kwenye comb hizi PCM, PCB

Chuo nikasomee mambo ya engineering kama sitabadili gia angani.

Licha ya soko la elimi bongo kushuka Kutokana na wasomi kukosa ajira ila nimejiridhisha kwamba elimu haiku guarantee ajira Bali inakupa ufunguo WA mambo mengi, ikiwa ni pamoja na upeo kufikilia na kutatua changamoto kuongezeka, connection kutoka sehemu mbali mbali.


Karibuni Kwa ushauri ndugu zangu elimu haina mwisho, elimu ni ufunguo WA maisha.
 
Karibuni Kwa ushauri ndugu zangu elimu haina mwisho, elimu ni ufunguo WA maisha.
Shule unaenda usome ili uje ulipwe laki mpaka million 3 na kadhaa na kuendelea kwa mwezi au ikiwezekana upewe million 250 au 300 mpaka 500 kwa mkupuo km kiinua mgongo pale unapolaza 60 chini, km una shughuli yoyote unayoweza kuifanya ukaingiza 50,000 mpaka 100,000 kwa siku 1 ningekushauri komaa na hio shughuli achana na elimu. Wote unaowaona wanasoma wanasoma ili waje kupata pesa hususa watoto wanaotoka kaya masikini
 
elimu ni bahari, nenda karudie paper ya form 4 kama umedhamiria

ila kama malengo yako ni ajira, nenda diploma baada ya form 4

Form 4 - 2026
Diploma - 2027 - 2030

Utamaliza diploma ukiwa na 32 / 33

kazi kibao ni za wenye vyeti vya diploma, ukiweza kuingia utaongeza elimu ya degree hata kwa kusomea chuo huria (open university), ni chuo chenye mfumo wa kujisomea nyumbani, mnaenda chuo kufanya mitihani, wanadfunzi wengi ni watu walioajiriwa.
 
Nikiwa kama kijana mwenye degree ila ni saidia fundi ningeshauri uachane na mawazo ya elimu. Za kuambiwa changanya na zako.
Sasa kwanini uchague saidia fundi mkuu, si utengeneze till za uwakala uwe angalau wakala WA miamala kaka,

Binafsi ni wakala pia nimefanya saidia fundi kitu nilicho ji funza nikua ni ngumu sana fundi au saidia fundi kutoboa maisha.

Angalau biashara inakupa ufadhili WA maisha.
 
Bahati mbaya sina mchongo unao niingizia kiasi hicho Cha pesa Kwa siku. Kama una idea tamu namna hiyo usiache kushea mjomba.
 
Hongera kwa mawazo hayo,binafsi nawaza fursa za hela Tu! Elimu nimewaachia wizara husika!
Hustling za mtoto WA kike na kiume ni mbili tofauti madamu wewe kesho unaweza kua mke WA rais ila kwangu ni ngumu kua Rais maana hata elimu tu Sina.

Bby the way ukipata mchongo mzuri nistue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…