Nina mashaka na kazi anazozifanya Rais Magufuli

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
843
Mheshimiwa Rais wetu anafanya kazi nzuri na nzito kwa ajili ya Taifa letu, ila nina mashaka huenda kazi nzuri na nzito anazozifanya zikadumu kwa muda tu, nahasa kwa kipinda atakachokuwa madarakani. Na baada ya yeye kuondoka madarakani anaweza akaibuka Rais ambaye ana mtazamo tofauti akavuruga jitihada nzuri tutakazo kuwa tumefikia.

Hivyo nashauri akumbuke kuunda mifumo mbalimbali ya nchi yenye uwezo wa kizalendo na kuendeleza mema yenye maslahi kwa Taifa, maana tatizo kubwa la nchi yetu ni mifumo iliyopo, ni mtazamo wangu tu.
 
Mheshimiwa Rais wetu anafanya kazi nzuri na nzito kwa ajili ya Taifa letu, ila nina mashaka huenda kazi nzuri na nzito anazozifanya zikadumu kwa muda tu, nahasa kwa kipinda atakachokuwa madarakani. Na baada ya yeye kuondoka madarakani anaweza akaibuka Rais ambaye ana mtazamo tofauti akavuruga jitihada nzuri tutakazo kuwa tumefikia. Hivyo nashauri akumbuke kuunda mifumo mbalimbali ya nchi yenye uwezo wa kizalendo na kuendeleza mema yenye maslahi kwa Taifa, maana Tatizo kubwa la nchi yetu ni mifumo iliyopo, ni mtazamo wangu tu.
Wenzio kule Lumumba hawataki mfumo, wanataka matukio ya kushangilia tu. Nimtajeeee ....... ndiooooo
 
Hapa ndio unapo jiuliza Marehemu Kenyatta aliona nini hadi akamwambia Mwl Nyerere kuwa ni kama anaongoza maiti.
Hivi Magu hajamaliza hata miezi 6, hatua anazochukua tija yake haijaonekana, ahadi hata 5% bado, Uhuru wa uwazi ndani ya serikali mashakani nk nk .
Halafu mtu na akili yake anakuja na hoja kama hii? Kwa nini tusisubiri miaka miwili kisha tuone matatizo yameshuka au kupanda kwa kiasi gani
 
cha msingi anachoweza kufanya ni kubadili katiba! Ambacho sidhan km atafanya!
Huu wimbo wa katiba watu wanachezeshwa bila kujua,katiba haiwez kutatua matatizo.hata tu tuwe na katiba nzuri kupita zote duniani bila usimamizi madhubuti hamna kitu dadayangu. Hebu fikiria kitu kimoja unachofikiri kikibadilishwa kitaleta tija.
 
Ninamuunga mkono JPM kwa utumishi uliotukuka.Mimi nimezaliwa na kulelewa eneo inapolimwa kahawa.Ilikuwa inahudumiwa miaka 3 bila mkulima kupata kitu,mwaka wa 3 unaanza kuonja ladha ya kazi yako.Mwaka wa 5 Kahawa iliyotunzwa vizuri mfululizo na hali ya hewa nzuri ndiyo inakupa matunda ya kukulipa. Ukimudu kuendelea kuitunza inakulipa wewe,wanao na wajukuu zako.Ukiipuza inakupuuza. Ni kahawa naongelea.

Wapo waliolelewa maeneo ya wazalishaji mchicha.Kazi ya kuihudumia ni siku 14 tu au 21 inakulipa.Mchicha haurithiwi na watoto achilia mbali wajukuu.Kama unavyokuwa haraka ndivyo unavyokufa haraka.

Magufuri anapanda mbegu ya muda mrefu. Njia sahihi anayopaswa kufanya kama afanyavyo mchimbaji wa shamba la kahawa kuumia kwenye ardhi ngumu ni kuirudisha katiba ya Mh.Joseph Sinde Warioba ili hata muda wake utakapokwisha kuwe na nyenzo ya kuwadhibiti watawala.

Ndoto ya 2020 kuwa JPM hataiona ikulu endapo katiba ya Warioba ikipita ni ndoto ya wendawazimu. Wenye akili timamu hawataisifia katiba iliyosimamwa na Joka la Makengeza na timu yake wala kuwapa ikulu wanunuzi wa kura.

Wapinzani halisi wa JPM hawapo upande wa pili,wamebaki waganga njaa na wanunuzi. Hatuuzi utu wetu.Mtenda haki ataitawala Tanzania kwa kura halali.
 
Mheshimiwa Rais wetu anafanya kazi nzuri na nzito kwa ajili ya Taifa letu, ila nina mashaka huenda kazi nzuri na nzito anazozifanya zikadumu kwa muda tu, nahasa kwa kipinda atakachokuwa madarakani. Na baada ya yeye kuondoka madarakani anaweza akaibuka Rais ambaye ana mtazamo tofauti akavuruga jitihada nzuri tutakazo kuwa tumefikia.

Hivyo nashauri akumbuke kuunda mifumo mbalimbali ya nchi yenye uwezo wa kizalendo na kuendeleza mema yenye maslahi kwa Taifa, maana tatizo kubwa la nchi yetu ni mifumo iliyopo, ni mtazamo wangu tu.

nchi haiwezi kujengwa na mtu mmoja, nchi inajengwa na wananchi wote. yeye katimiza wajibu wake tena kwa kufanya makubwa sana sasa wewe na mimi tunatimizaje wajibu wetu katika kujenga nchi?

lipo tatizo la wananchi kuangalia viongozi bila kujua ni wajibu wao kuweka viongozi makini madarakani.

anayoyafanya raisi kwa sasa misimamo yake hii ilionekana kabla hata hajaingia madarakani lakini badala ya kuona ndiye mtu wa kuleta mabadiliko tunayoyataka pengine tulitumia misimamo hii kudai alituambia eti kama hatutaki kulipa nauli za vivuko tupige mbizi bila kuangalia misimamo hiyo ina faida gani kwetu sisi wananchi wanyonge tunaotegemea matumizi mazuri ya kodi zetu ndio mkombozi wetu.

sasa kama wananchi tutachezewa ngoma tukaona hawa waliotuchezea ngoma ndio tuwape kura itakuwa kosa la raisi wa sasa au kosa letu? kama tukiendekeza rushwa na misaada midogo tunayopatiwa ama wakati wa uchaguzi tutaona hao ndio wametukumbuka then itakuwa kosa la raisi?

tatizo kubwa ni ujinga na ujinga huu si wa elimu ya mfumo rasmi maana katika hili hata maprof tunaweza kuwa nao bado katika ujinga huu.

huu ni ujinga wa kuhusisha maisha yetu na mambo mbalimbali yanayotuzunguka.

tunaweza kuwa tunalamikia jambo lakini tunasapoti chimbuko la tatizo hilo.

utamsikia msomi mkubwa nchi hii akisema wananchi hawataki kusikia siasa kuongelea utawala bora na mambo mengine bali wao wanataka kusikia maji, umeme, barabara bila kutambua mchakato ulipo kuanzia mipango, usiamiaji, utekelezaji wa mipango unaweza kuathiri upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi na bila kuweka taratibu zikaa vizuri huduma hizo haziwezi kupatikana.

haya tutayalinda sisi wenyewe wananchi kwa
1. kutambua wajibu wetu
2. kutambua viongozi bora ni watu wa aina gani? na kura zetu ndio zinaamua viongozi. kama tukichagua pumba tusimlaumu tu kama tukichagua mbegu bora tujisifie wenyewe pia.
 
Mheshimiwa Rais wetu anafanya kazi nzuri na nzito kwa ajili ya Taifa letu, ila nina mashaka huenda kazi nzuri na nzito anazozifanya zikadumu kwa muda tu, nahasa kwa kipinda atakachokuwa madarakani. Na baada ya yeye kuondoka madarakani anaweza akaibuka Rais ambaye ana mtazamo tofauti akavuruga jitihada nzuri tutakazo kuwa tumefikia.

Hivyo nashauri akumbuke kuunda mifumo mbalimbali ya nchi yenye uwezo wa kizalendo na kuendeleza mema yenye maslahi kwa Taifa, maana tatizo kubwa la nchi yetu ni mifumo iliyopo, ni mtazamo wangu tu.
Nitamkubali pale tutakapopata katiba ya mwananchi ambayo itaweka mfumo mzuri wa uwajibikaji kwa viongozi na mwananchi. Haya mengine inategemea mtu na mtu, akija mwengine anaweza kufanya yake maana sheria inamlinda na inaruhusu yeye kujiachia. Ila katiba ikikaa vizuri tutakuwa salama zaidi.
 
Back
Top Bottom