Nina mashaka na huyu mwanaume

Nina mashaka na huyu mwanaume

letmary

New Member
Joined
Sep 18, 2017
Posts
3
Reaction score
5
Poleni na majukumu wana MMU, naomba niende kwenye Mada moja, kwa Moja Nina mahusiano na mwanaume mmoja, Mimi ni mfanyakazi Na mwenzangu ni mfanyakazi pia,mishahara yetu haitofautiani Sana japo yeye ananizidi kidogo, Cha kushangaza toka nimekuwa nae kwenye mahusiano haishi kulalamika hana hela(sina tabia ya kumuomba hela)amekuwa na tabia ya kunililia shida kila siku,kosa akiona hela nyingi kwenye pochi lazima aombe, niliwahi kuzungumza nae kuhusu tabia yake na future yetu akadai ana majukumu huko kwao ndo maana hela yake haikai. Ana mpango wa kwenda kutoa posa mwaka kesho,naombeni ushauri wenu jamani niko njia panda, huyu mtu akinioa ataihudumia familiar ipasavyo kweli? Tatizo lake jingine sio mpambanaji kabisa, hata ukimuomba ushauri wa jambo la kujenga majibu yake ni zero,naombeni ushauri wenu jamani huyu mwanaume kweli atanifaa iwapo tutaingia nae kwenye ndoa?
 
Mkuu zinduka tutoka ucngizini,huyo jamaaa!nihatar kwa afya yako,kapnda mkwanja huyo,so be careful ma dia
 
wacha ujinga wewe,,,, ushapata bwana mwingine unatafuta sababu........juilize mmetoka wapi,,, je ni sahihi kwao ana majukumu........mipango yenu ya baadae kwa pamoja mmeipangaje,,,, au umemwachia yeye apange maana ndo katabia kenu........unafikiria hapa ndo penye suluhisho?????.....jipange dada.....ndoa ni maisha na sio utegemezi........utakimbia wangapi jiulize.......watakuchovya wangapi???? umejichunguza na wewe mwenyewe????
 
Pole sana dada. Mwanaume ambaye awezi kuwajibika mwanzoni mwa mahusiano huyo atakusumbua mbeleni. Wanaume wengi kipindi hiki wanapenda kuhudumiwa. Fikiria mwanaume anatafuta mchumba wa kuoa anaulizia anafanya kazi gani? za kuambiwa changanya na zako. Atakusumbua mbeleni.

Fanya maamuzi mapema.
 
Back
Top Bottom