Nina mashaka na huyu mwanamke

Sioni Shida hapo. Unahukumu kwa hisia. Timiza wajibu wako
 
Kama limbwata basi nitakuwa nimeshakula sana. Maana angalau kila siku mbili katika wiki huwa anakuja na tunapika wote chakula hapa kwangu. Au mara moja moja huwa ananiletea chakula kwangu.. na wakati mwingine huwa nakula nyumbani kwake.

Kama lengo litakuwa hilo, basi limbwata za kwenye chakula zitakuwa hazijafanya kazi. Au unaonaje?
Mkimbie huyo manzi ni mshirikina anakuandalia limbwata
 
Inawezekana,

Ila sijawahi mshuhudia akifanya hivi kabla. Sijawahi mhisi kwa jambo la namna hii. Na ni mara yangu ya kwanza naona hili. Unadhani sina sababu ya kuuliza?
Hakuna kitu chochote kibaya hapo. Ila wewe unataka kumtafutia sababu tu.
 
Lakini, ni maridhiano ya hiari ndio yataleta tija na upendo halisia. Kama kuna nguvu imetumika, ikikaribia kuisha utaongeza nzito zaidi.. nakuendelea nakuendelea. Mwisho wa siku tutakuwa tunabomoa hatujengi
Wanaume dawa yenu ndogo, hueleweki taratibu unaeleweshwa
 
We jamaa yaani mnatenda dhambi za uchafu afu eti mnasali pamoja??????! Shit! Umenikumbusha dada mmoja alikuwa anajiita mpendwa na rafiki yake akawa anakuja na Biblia eti wamekuja kuomba wakaishia kupeana mimba. Guys hamuwezi fanya mapenzi nje ya ndoa afu mkaingia kwenye sala wote mkiwa wazinzi!!
 
Naelewa, wakati mwingine kama binadamu tunafanya hayo makosa. Mara kwa mara. Lakini faraja inaongezeka kama kunakuwa na nafasi ya kuweza kusali pamoja, ni kutengeneza matarajio bora mbeleni.

Dhambi inaweza isiwe kuzini tu, kuna kudanganya , wizi, kutamani n.k ukinihukumu kwamba ninasali halafu nazini, basi wahukumu pia wanao sali na wanaiba, wanadanganya n.k.

Shukrani.
 
Kwa sababu umeshamuona anachofanya basi limbwata lake halitafanya kazi tena. We endelea kujilia mema ya nchi.

Kingine cha muhimu, mpaka hapo umeshamjua hana uvumilivu. Nyakati kama hizo ndizo huwa nzuri kumjua mwenzio uvumilivu wake ukoje. Kwa dalili hizi huko mbeleni mkipatwa na magumu basi hatasita kufanya mambo tofauti na unavyotegemea.
 
Ukija JF eleza vitu vyote unavyoweza ona vitasaidia watu kuelewa na kushauri just in a single comment...

Haya we baki usubiri wenye muda wa kuuliza maswali...

Sayonara

Unaweza kunichokoza upate maelezo ya kutosha. Niulize maswali ya kutosha ili niweze kukujibu. Siwezi kuweka kila kitu.
 
Balehe inakusumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…