Nina mashaka na akili ya John Thobias wa ATN

Nina mashaka na akili ya John Thobias wa ATN

leo nilibaatika kumchungulia...niliona akisoma habari moja tu ya michezo coz zote zilikuwa zinazungumzia mgogoro wa simba
 
Mbona mitambo hipo ming kwenye vyombo vyetu vya habar!!!Bora wameacha kuonyesha epl coz walikua hawana wanaloweza kuchambua.Hata utotol nina mashaka km walicheza japo chandimu
 
Jana kwa masikio yangu wakati wa kipindi cha Uchambuzi wa Magazeti, nimemsikia mtangazaji John Thobias wa kipindi hiki akifanya kile nachokiita muendeleo wa kuibomoa fani ya habari.

Katika namna ya kushangaza, jamaa huyu ambaye nina mashaka na uwezo wake wa kukumbuka ni wapi alipo na anafanya nini alionesha upenzi uliokithiri kiasi cha kusahau kazi yake na kuleta ushabiki.

Alikuwa akisoma habari katika kurasa za michezo ktk magazeti mbali mbali ambapo kwa makusudi kabisa, badala ya kuwa msomaji kama alivyoajiriwa akajifanya muamuzi:

Kichwa: Seintfit: WAAMUZI BONGO NI KIKWAZO - hii akaisoma na kuongezea maneno yake mengi kupamba jinsi waamuzi wanavyoboronga na kuikwamisha simba kuifunga Mgambo JKT

Kichwa: Baada ya mfululio wa Sare, Kocha Simba aanza visingizio - hii alisema hivi "ah hii achana nayo haiko more technical"

Kichwa: Yanga.... - hii akasema "ah hizi habari za Yanga, hazina mashiko" na akaendelea na habari nyingine.

Je, ATN ina mgogoro na Yanga au ni mapenzi ya John Tobias kwa Simba?
Kazi yake ni kutusomea vichwa tu - digest au kutuambia ipi ni habari na ipi si habari? Hapa nachokiona ni huu utaratibu wa kuajiri presenters wasio na maadili. Yupo Mwenzake pale pale ATN anaitwa Kelvin Moto, huyo yeye ni kuisifia Manchester United hata siku ilipotandikwa 3 kwa 1 na Barca Wembley aliisifia kuwa imecheza mpira mzuri lakini bahati haikuwa yao.

Huu ni ugonjwa gani wa kuonesha mapenzi studio?

Hahahaaa sijui kwanini mimi kanifurahisha kweli huyo jamaa... Hapa hadi najuta kukosa kipindi chake! Hahahaaaa, kuanzia sasa mtakuwa navizia nikikuta anasoma yeye tu magazeti ndo nasikiliza... Jamaa anaweza kufanya usahau maumivu ya Simba kufungwa!
 
leo nilibaatika kumchungulia...niliona akisoma habari moja tu ya michezo coz zote zilikuwa zinazungumzia mgogoro wa simba

Hehehe.....ndo.waandishi wa michezo wa bongo.. baadhi Yao full usanii
 
Back
Top Bottom