Nina mashaka na akili ya John Thobias wa ATN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina mashaka na akili ya John Thobias wa ATN

Discussion in 'Sports' started by Mwana Mtoka Pabaya, Oct 24, 2012.

 1. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Jana kwa masikio yangu wakati wa kipindi cha Uchambuzi wa Magazeti, nimemsikia mtangazaji John Thobias wa kipindi hiki akifanya kile nachokiita muendeleo wa kuibomoa fani ya habari.

  Katika namna ya kushangaza, jamaa huyu ambaye nina mashaka na uwezo wake wa kukumbuka ni wapi alipo na anafanya nini alionesha upenzi uliokithiri kiasi cha kusahau kazi yake na kuleta ushabiki.

  Alikuwa akisoma habari katika kurasa za michezo ktk magazeti mbali mbali ambapo kwa makusudi kabisa, badala ya kuwa msomaji kama alivyoajiriwa akajifanya muamuzi:

  Kichwa: Seintfit: WAAMUZI BONGO NI KIKWAZO - hii akaisoma na kuongezea maneno yake mengi kupamba jinsi waamuzi wanavyoboronga na kuikwamisha simba kuifunga Mgambo JKT

  Kichwa: Baada ya mfululio wa Sare, Kocha Simba aanza visingizio - hii alisema hivi "ah hii achana nayo haiko more technical"

  Kichwa: Yanga.... - hii akasema "ah hizi habari za Yanga, hazina mashiko" na akaendelea na habari nyingine.

  Je, ATN ina mgogoro na Yanga au ni mapenzi ya John Tobias kwa Simba?
  Kazi yake ni kutusomea vichwa tu - digest au kutuambia ipi ni habari na ipi si habari? Hapa nachokiona ni huu utaratibu wa kuajiri presenters wasio na maadili. Yupo Mwenzake pale pale ATN anaitwa Kelvin Moto, huyo yeye ni kuisifia Manchester United hata siku ilipotandikwa 3 kwa 1 na Barca Wembley aliisifia kuwa imecheza mpira mzuri lakini bahati haikuwa yao.

  Huu ni ugonjwa gani wa kuonesha mapenzi studio?
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Unapochanganya dini na mambo ya dunia tegemea mambo kama hayo. Kigezo cha kuajiriwa ATN ni kuwa muumini kwanza, vingine hufuata.
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Mkuu sema jamaa unamuelewa vibaya. mi huwa namsikiliza kila siku na ndo mtu mtu pekee katika media za tanzania anaye soma magazeti kwa ufasaha. kuhusu michezo kwa tanzania kila mtangazaji utajua yupo upande gani kama utamfuatilia. michezo anasoma kwa mbwembwe ili kuwavutia watu waangalie mechi kwenye king'amuzi chao cha ting.
  ni kweli magazeti mengine yana habari zisizo na mashiko ndo maana akasema "hii ya yanga haina mashiko" na hakuisoma kama unakumbuka. muache dogo apige kazi hakuna mbadala wake. mia
   
 4. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushauri uache kutazama atn . Kuanzia leo hamia refio imani au soma al anuur. Unataka kila mtu awe na mawazo km yako?
   
 5. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Refio imani kwani mi nataka kujifunza ujinga? Kawashauri watu wa Mbagala, Manzese, Mburahati na Kigogo, mimi naishi Mbezi. Na hilo gazeti unaloniambia nitalisoma pindi nitapoanza kufuga majini

  Sikusema kila mtu awe na mawazo kama yangu, ila kama mwana habari anatakiwa awe NEUTRAL.
   
 6. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Nini kinakufanya ufikirie kuwa nimemimina uzi kwa ajili ya siku hii moja tu? Suala habari ya Yanga kukosa mashiko wala haihusiani na habari yenyewe, bali inahusiana na mapenzi yake kwa Simba.

  Siku Yanga ilipochukua kombe la Kagame nilimsikia laivu akinena mara baada ya kusoma habari hiyo katika Mwanaspoti "Mpira hauna adabu bwana timu zenye kupiga mpira wa mkali ndio hivyo tena"

  Kukosa kwake mbadala ni kupi?
   
 7. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kuna haja pia ya kuhoji akili ya Maulid Kitenge wa RadioOne na ITV.
   
 8. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa mimi ni Mkurugenzi wa hiyo station ningempiga Warning 1 kali sana,akirudia anaenda kujiunga na Ezekiel Kamwaga kwenye ku'report issue za Club aipendayo,shwaini!
   
 9. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Sijaona ubaya wowote aliofanya! Huwezi kuficha mapenzi! yeye ni shabiki wa chama kubwa! wekundu wa msimbazi! Taifa kubwa! Mnyama! kesho tunamlambisha azam koni lake.
   
 10. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Umefikiria kwa ufupi sana.
  Hata uwe mpenzi kiasi gani, linapokuja suala la uandishi wa habari unatakiwa usiegame popote.
  Hebu jiulize, ukishawaonesha watu kuwa unaipenda Lipuli halafu ndo iwe nini? Zaidi unajikuta ajira inaning'inia na ulichopata hakuna.
   
 11. M

  Masuke JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Maulid Kitenge afadhali kidogo, balaa ni yule mwenzake Omar Katanga.
   
 12. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  John Thobius anasoma magazeti! hajaandika habari! wewe ndio unafikiria kwenye vaccum!
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh teh!
  Naona umechanganywa na neno mwandishi wa habari, ukilitafsiri kwa kizungu ni 'news writer', kuna uwezekano mkubwa kuwa hakuna news writer, bali kuna scriptwriter, producer, director, anchor, reporter, photojournalist na kadhalika. Lakini in most cases hawa wote ni waandishi wa habari na wanatakiwa wafuate codes za journalism ethics, mojawapo ndo hiyo ya kuobserve neutrality kwenye wanachokitengeneza.
  Got it?
   
 14. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  John Thobius ni deiwaka pale ATN hana qualifications za uandishi wa habari.umenipata dogo?
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wote sifuri, kwanza wanahribu kabisa kiswahili hawa watu....ndiyo madhara ya kukimbia hesabu secondary, inamfanya mtu kuw ana uwezo mdogo wa kufikiri na kuanalyze
   
 16. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mwanzo umemsifia kwa alichokifanya, nikakueleza mapungufu yake na kwanini hakutakiwa kufanya vile sasa hivi unaniambia hana qualification.
  Ni makosa kuajiri mtu asiye na vigezo, kwani atakapokinukisha uongozi ndo utakuwa matatani.
   
 17. Blood Hurricane

  Blood Hurricane JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,151
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Umeshasema ATN ulitegemea nini sasa? Ni TV isiyokuwa na mpya kabisaaaaaaa.
   
 18. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2012
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,156
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
   
 19. M

  Masikrodinga JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  kweli kbs PrN KAZI, Kitenge anaboa mbaya afu mby zaidi mwnyewe anajiona fundi kweli, jamaa kajaa mapenzi kweli. After game ya Simba na Mtibwa na mashabk wa Simba walikuwa wanatuma maoni wakisema kwamba Simba lazima wakae chini watafute tatizo ni nn hadi timu ifanye vibaya kiasi hiki kutoka sare tano na kufungwa mechi moja kati ya mechi nane walizocheza, eti yeye akasema hakuna haja ya kukaa chini na kujiuliza kwan hayo ni matokeo ya kawaida na timu bado haijafanya vibaya wakati Yanga ilipotoka sare na Prison na kufungwa na Mtibwa alisema lazima Yanga wakae chini na wajiulize kwa nn timu ifanye vibaya namna hiyo, sasa jiulize kweli huyu mtu yuko fair kitaaluma?
   
 20. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni jambo muhimu sana kuangalia kigezo cha dini kwani ukifanya mzaa kwenye hili unaweza kuajiri magaidi!
   
Loading...