Nina marafiki waliowahi kusoma Kenya na Uganda Primary, wameteseka kupata ajira, Je kusomesha mtoto nje ni kumpunguzia uwezekano wa kuajirika Tanzania

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Nina classmates waliowahi kusoma nje ya nchi elimu ya msingi kwa shule za Uganda na Kenya.

Walirudi Tanzania kuendelea na elimu ya sekondari hadi vyuo kusomea IT, HR, Accounting, Law, Engineering na procurement.

Ni moja tu alieajiriwa serikalini, hao wengine wapo walio kampuni binafsi wengine walishakata tamaa na ajira

Swali langu ni wanapitia changamoto ya ajira kama ilivyo kwa wengine waliosoma hapa au kuna la ziada ?
 
wanaajiriwa vizuri, sample space yako ni ndogo sana kuthibiisha hii kauli yako mkuu tena kwa hizo career sijui HR ni kipengele mkuu nimemmaliza 2018 Darasani tulikuwa 84 ila tulioajiriwa hadi sasa hatufiki 15
 
Mbona watu kibao nawafahama waliendaga kusoma uganda saivi wote wapo serikalini naona pia hizo kozi walizo soma zimechangia
 
Tatizoni ni kitu walichokisomea, hakihitajiki sokoni.
Kwa wale wote wasiokuwa na ajira, tatizo lao ni wamesomea kitu kisichohitajika sokoni.
Wakatafute fani inayohitajika sokoni wasome, na sio wasome kwanza ndio waanze kutafuta soko.​
 
Huwa naamini mtu anapo enda kusomea nje Huwa anarudi na kitu extra hao ndo tunategemea wafungue makampuni waajiri wengine lakini imekuwa tofauti
 
Ndio, hakikisha unapomsomesha unamuandalia njia ama mtaji wa biashara
 
Kwan waliosoma izo HR hapa bongo wangapi wameajiriwa hapo ishu sio kusoma nje ishu n kozi za kiboya izo mfano wangesoma mambo ya nuclear unazani wasingeajiriwa hata iran ingewaajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…