sasa kama amestukia kuwa unataka kumpa sapraiz ya pete ya uchumba unataka asijiandae? Wacha ajipambe ili upate heshima mjini.Ni kawaida mkuu kwa dada zetu hata usipanick baadae mfundishe kuwa time ni mtaji popote!
Jamani umekosea sana kufuta huo mtoko.. Napata picha ndio ingekuwa mie.. Duh ningenunaje! Maandalizi yote hayo halafu holaaaaaa...! Wee ungemvumilia tuu kwa leo halafu wakati wa maongezi ndio ungemwambia kuwa ni muhimu kwenda na muda, angekuelewa tuu mkuu..!
Mmmmmh... Kama ameweka na kope za kubandika ili atokelezee imekula kwake..Lol
Itabidi hayo tuyaongee wakati mwingine........sasa hivi mind yangu imeishiwa hamu kabisa
Mi naamini unampenda na ndiyo maana unaona anapochelewa inakuuma,sasa kwa kuwa anachelewa mpe nafasi mkuu,polepole ndio mwendo.Akija fanyeni mlopanga kuyafanya mkimaliza ongea nae taratibu kwa kumuelewesha kuonesha kwamba hali hiyo inakukera sana na usingependelea lijirudie wakati mwingine.Inaudhi sana masaa 5 na bora angesema mapema kuwa atachelewa. Picha niliyopata ni kama hajali hivi.
Mi naamini unampenda na ndiyo maana unaona anapochelewa inakuuma,sasa kwa kuwa anachelewa mpe nafasi mkuu,polepole ndio mwendo.Akija fanyeni mlopanga kuyafanya mkimaliza ongea nae taratibu kwa kumuelewesha kuonesha kwamba hali hiyo inakukera sana na usingependelea lijirudie wakati mwingine.
Tambua pia bado yupo kwao kama si kwa wazazi basi walezi so yawezekana anataka kufanya timing awe amekamilisha mambo fulani fulani.Ili aweze kuwa mkeo mwenye sifa uzitakazo tumia pia muda wako kumfunza mambo mazuri ulonayo nawe pia jifunze mazuri yake.ILi kudumu lazimu mvumiliane!
Mpigie simu bana, umwambie walau muonane jioni..! Yaani mwenzio kakesha anachagua mpalo wa kutokelezea nao kwenye mtoko na wewe halafu kirahisi rahisi tuu unaghairisha..! Dah....! Yaani hapa nampatia picha jinsi atakavyokuwa amesikitika..!
Wadada ndivyo tulivyo jamani... Mtuzoeage tuu na kuturekebisha taratibu sio kutuadhibu namna hiyo..!
Shida ya M-bongo n kwamba kupanga mtoko tayari keshapanga na kum-do mtoto wa watu. Sasa akiona muda unaenda anaona atalipia eneo la tukio bila kupata maximum enjoyment.
Kiswahili kigumu wenzangu!!, Hapo kwenye nyekundu sielewi, naona kama TUSI!!