Nina Imani kubwa na CHADEMA - Prof. Baregu

Nina Imani kubwa na CHADEMA - Prof. Baregu

Prof Baregu mulimtukana sana humu JF kwa matusi ya wazi kabisa pale alipotoa ya moyoni juu ya mwelekeo wa chadema na siasa zake! Mulimshambulia huyu Mwl wangu na roho iliniuma sana kwa maana namjua msimamo wake!

Vijana wa Bavicha mulimvua nguo huyu Mzee wa watu na Kama kawaida yenu mulimuita Msaliti! Leo hii mnakaa mnasema uzee dawa? Haya maneno yanatoka moyoni au? Poleni sana!

Hivi ni yupi ambae hamjawahi kumuita msaliti ndani ya chama chenu? Mbowe alipompigia Magoti JK kumshukuru kwa kazi nzuri yaani mulimporomoshea mitusi ati msaliti mkubwa ndani ya chama!

Kazi mmnayo nyie kwenu kila mtu akinena baya basi ni msaliti!

Wewe umeona hayo tu wakati mwenzako lizbon alimsifia kwa mgongo wa chupa aliposema"nikiambiwa kuchagua chama changu na Nchi nitachagua Nchi yangu"ila leo tena anamuitwa "reject"
Maccm bwana
 
Wewe umeona hayo tu wakati mwenzako lizbon alimsifia kwa mgongo wa chupa aliposema"nikiambiwa kuchagua chama changu na Nchi nitachagua Nchi yangu"ila leo tena anamuitwa "reject"
Maccm bwana

Tatizo elimu yao ya Ngumbaru hawakuweza kumuelewa Prof Baregu.
 
Kina MM na wenzake walikuwa wanafikiri mtu mzima angejiunga na kigenge chao.

hakika namkubali huyu mwamba.

Hakuna Professor mwandamizi aina ya Baregu atakayeweza kujidhalilisha kujiunga na kakikundi ka wahuni ACT. Ni Dr. Mjinga tu, Kitila Mkumbo ndo mshipa wa aibu umefyatuka
 
Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Professor Mwesiga Baregu amesema ana Imani kubwa na chama chake katika kuleta uongozi bora nchini.

Professor Baregu aliyezungumza na waandishi nje ya Ukumbi ambao mkutano wa Kamati Kuu ukiwa unaendelea amesema kuna watu ambao wanakesha wakiomba ili Chadema isambaratike lakini akaonya watu wa aina hiyo watasambaratika wenyewe.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa mjumbe wa Tume ya Katiba amesema kwa umri wake ameona na kupitia mambo mengi katika siasa na hivyo akasema ana uhakika Chadema itafika mbali katika siasa za Tanzania.

Mimi Binafsi, simwamimi saaana Baregu. Ila statement hii inaibua matumaini mapya na imeonyesha tofauti kati ya vitoto (ifweero, Mchange) na big babies (Kitila Mkumbo) na wasomi tumbo, Zitto na Kitila
 
Last edited by a moderator:
Wenye nia njema na Tanzania ni wale wanaoikubali CHADEMA na wale waliojitoa mhanga kuikomboa Tz.
 
Back
Top Bottom