M.E.M.A
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,373
- 472
Baada ya mechi ya jana kati ya Yanga na Al Ahyl..ambayo imehitimisha ndoto za Yanga kwenye michuano hii mikubwa barani Afrika, sasa ni wakati wa kukaa chini na kutafakari. Kejeli za 'Mtani jembe' hazitatufikisha popote, zaidi sana mwaka mwingine tena tutashuhudia team nyingine au ile ile ikikwama mahali pale pale kisha tutarudi na kejeli na mwaka mwingine tutashuhudia team ile ile au nyingine ikikwama mahali pale pale..and that will keep on circling. .
Cha kujifunza ni kuwa hamna fitina hapo, kama wanajua wanajua tu. Unakumbuka mechi ya Barca na Arsenal mwaka...(sikumbuki) kule Nou Camp walimlaumu sana refa kumtoa RVP kwa red card. Ila hadi anatoka na hadi mwisho wa mchezo Arsenal hawakuwa na hata single shot on target au off target. Kuonesha kama unajua unajua tu.
Yanga waache kelele za fitina na waweke malengo ya kucheza Club bingwa ya dunia. Hata wapewe ushindi hapa..wakikutana na Santos, Man City, Barcelona, Real Madrid, Atletico Madrid au Man U unadhani watatoboa au itakuwa kama Haiti kwenye Euro mwaka jana.!?
Kinachoisibu Yanga, Simba, Azam na wengineo ndio hicho hicho cha team ya taifa. Hakuna jipya. Hakuna mafanikio ya haraka haraka..tuwekeze kwenye accademy za kisasa kwanza. Fedha nyingi tunazotumia kupata makocha wa kigeni ziwekezwe kupata walimu bora wa hizo accademy. Bila hili na huu mfumo wa professional watatu tu wa kigeni ndio kabisaa tusahau kuvuka hata raundi ya kwanza...
Chekechea zinamsaidia mwanafunzi pale atakapoingia darasa la kwanza angalau anajua kuimba ..a, b, c, d... Elimu bora ya msingi inamsaidia mwalimu wa sekondari na mwanafunzi, hivyo itamsaidia profesa chuoni kumfundisha mwanafunzi huyo. Sasa iwapo mwanafunzi karuka ruka kote huko kisha umuweke chuo kikuu halafu unamfundisha Civil Engineering na apate first class..kweli!!???? Basi hivi ndivyo tufanyavyo kwenye soka.
Wanasema."wazimu ni kufanya kitu kile kile, kwa njia ile ile na kutegemea matokeo tofauti". Kwa hili hakika...tutaendelea kuitwa Kichwa Cha Mwenda Wazimu.