Imepita miaka 17 tangu nikutane na kupotezana na huyu Dada.
Pia ni miezi kadhaa toka niondoke nchini na kwenda Moja ya nchi za Afrika Magharibi kikazi, nimerejea nyumbani mwisho wa wiki iliyopita na nimeripoti kazini jumatatu ya Jana, tukio ninaloenda kukuhadithia limetokea Leo hii na muda huu, "Muda wa Lunch"
Mimi hupenda sana inapofika muda kama huu kutoka katika chumba cha ofisi yangu na kwenda kupata Misosi na Kuzimua kidogo konyagi ndogo au Ganja, kisha hurejea kazini kuhudumia taifa hili lenye wananchi maskini kama Mimi, sasa Leo mchana nikapata taarifa za mgahawa unaokimbiza sana hapa mjini kwa sasa nikaona isiwe shaka ngoja niende zangu hapo nikapate Msosi, sikuwa peke yangu nilikua na moja kati ya watu wangu wa karibu ambaye ndiye alinipa habari za mgahawa huu.
Mara baada ya kufika tukapokelewa na muhudumu mmoja mzuri sana, mzuri kiukweli, kwa bashasha akatukaribisha na kutuhudumia, muhudumu huyu sura yake si ngeni sana machoni pangu, Ila sikumbuki nilikutana nae wapi.
Mungu si athumani, yeye alinikumbuka na kunitambua kisha akaanza kunikumbusha jinsi nilivyo-mfatilia sana enzi hizo akiwa bado mbichi, hapa ndipo kumbukumbu zangu zikarejea sawasawa, miaka 17 iliyopita huyu binti alinitesa sana tena sana (maana nilikua namzimia kinoma) wakati huo mimi nilikua nasoma stashahada yangu na yeye alikua ni mtoto wa mkuu wa chuo nilichokua ninasoma,
Kilichonifanya niandike Uzi huu ni jinsi binti huyu alivokuwa akinijibu miaka hiyo ya 2000 kila wakati nilipotaka kuongea nae, yeye alinidharau sana na kupenda kunijibu SINA MUDA.. Leo naona kapata muda, Hakika maisha ni duara, Leo na Mimi nimemjibu sina muda ila kama ana yeye ana Muda anitafute (nimemuachia namba), na naona kasha nitumia SMS
Ninawashauri jambo wadada, kuweni makini na tambueni kuna kesho (Japo Haifikagi), Maringo na nyodo ni hulka yenu ila mnapaswa kuwa makini.