Nina double life

Nina double life

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
2,842
Reaction score
3,616
Ni hali ya kweli imenipata tangu mwaka 2010. Leo ni mara ya kwanza naisema. Siamini mambo ya misukule, lakini hii hali kweli siielewi, lakini ni kama naifurahia hivi.

Ilitokea hivi mwaka 2010 sikumbuki tarehe siku moja nililala nikaota ndoto kuwa eti niko kwenye mji fulani tofauti na ninakoishi, nikiwa nasoma chuo masomo ya biashara, business administration.

Sijawahi kusoma masomo hayo katika maisha nje ya ndoto kesho yake nikaamka, nikaendelea na siku yangu hadi ikaisha.

Nilipolala tena ile ndoto ya jana yake ikaendelea, nikapata marafiki darasani, nikawa najishughulisha na michezo nikajifunza kuogelea (sijui kuogelea nje ya ndoto!) na mambo mengi mazuri

Huko katika ndoto usiku ukaingia nikaenda kulala hostel, nikiwa usingizini nikaota ndoto kuwa nimeamka ambako niliamkia nyumbani kwangu kwenye maisha yangu ya siku zote.

Kufupisha story, nimekuwa kwenye mzunguko wa ndoto za kama za series, yaani nalala nyumbani naota mwendelezo wa ile ndoto na huko ndotoni nikilala naota nimeamkia nyumbani, kwa hiyo mzunguko unaendelea.

Hata ninavyoandika hapa sijui sasa ndio niko kwenye ndoto au maisha halisi. Kule kwenye ndoto nyingine maisha yameendelea vizuri, nimemaliza chuo, nafanya kazi kwenye kampuni ya kuuza pikipiki, na nimejenga nyumba eneo fulani la mlimani, na nina mke na mtoto wa miaka 4.

Kwenye maisha haya niliyoamkia leo asubuhi ni mtu mzima kuliko yule wa ndotoni, nina mke na watoto wanne wakubwa, wa mwisho yuko form four.

Sina tatizo lolote la kiakili, na wala ninapoamka sijisikii kuchoka popote, nakumbukia tu maisha yangu ya ndotoni na kuyashangaa, basi.

Je, hili ni tatizo? Kuna wengine wenye ndoto za aina hii?
 
Last edited by a moderator:
Au ni wewe tuko pamoja ndotoni?
Huyo mke wangu na mwanangu wa ndotoni sijawahi kuwaona popote nje ya ndoto!
Ndoto ni bayana Mkuu! Hiyo kusali na Familia haitoshi- Funga na kuomba washirikishe viongozi wa Imani yako kuhusu hili.
 
Chunga usije ukaota unakunya, alafu ukiamka ukute kimba kwa bed....
Miushauri wangu ni huo tu.
 
Ni hali ya kweli imenipata tangu mwaka 2010. Leo ni mara ya kwanza naisema. Siamini mambo ya misukule, lakini hii hali kweli siielewi, lakini ni kama naifurahia hivi.
Ilitokea hivi. Mwaka 2010 sikumbuki tarehe, siku moja nililala nikaota ndoto kuwa eti niko kwenye mji fulani tofauti na ninakoishi, nikiwa nasoma chuo masomo ya biashara, business administration. Sijawahi kusoma masomo hayo katika maisha nje ya ndoto. Kesho yake nikaamka, nikaendelea na siku yangu hadi ikaisha. Nilipolala tena ile ndoto ya jana yake ikaendelea, nikapata marafiki darasani, nikawa najishughulisha na michezo nikajifunza kuogelea (sijui kuogelea nje ya ndoto!) na mambo mengi mazuri. Huko katika ndoto, usiku ukaingia nikaenda kulala hostel, nikiwa usingizini nikaota ndoto kuwa nimeamka ambako niliamkia nyumbani kwangu kwenye maisha yangu ya siku zote.
Kufupisha story, nimekuwa kwenye mzunguko wa ndoto za kama za series, yaani nalala nyumbani naota mwendelezo wa ile ndoto na huko ndotoni nikilala naota nimeamkia nyumbani, kwa hiyo mzunguko unaendelea. Hata ninavyoandika hapa sijui sasa ndio niko kwenye ndoto au maisha halisi. Kule kwenye ndoto nyingine maisha yameendelea vizuri, nimemaliza chuo, nafanya kazi kwenye kampuni ya kuuza pikipiki, na nimejenga nyumba eneo fulani la mlimani, na nina mke na mtoto wa miaka 4. Kwenye maisha haya niliyoamkia leo asubuhi ni mtu mzima kuliko yule wa ndotoni, nina mke na watoto wanne wakubwa, wa mwisho yuko form four.
Sina tatizo lolote la kiakili, na wala ninapoamka sijisikii kuchoka popote, nakumbukia tu maisha yangu ya ndotoni na kuyashangaa, basi.

Je, hili ni tatizo? Kuna wengine wenye ndoto za aina hii?
Ninavyo jua double life is a physical concept and not a spiritual one..Mfano wa Double life is like umeoa wanawake wawili mmoja anaishi dar mwingine anaishi Moro na hawajuani na kila mmoja unaishi NAE kanakwamba umemuoa peke yake.Wa dar anajua kazi yako ni mfanyabiashara wa nataka ambae huwa unasafiri safiri mikoani kuchukua biashara ilhali wa moro anajua kazi yako ni mkulima na mfugaji ambae huwa unaenda sana dar.

Mfano mwingine ni pale MTU anapokuaa shoga lakini kaoa mke na anafanya kwa siri.

Akiwa kwa mkewe yeye kidume lakini akienda kwa basha wake huko anageuka mwanamke
 
Hata mimi nilielewa hivyo kumbe ni tofauti kabisa na kichwa cha habari 🙂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom