Nina changamoto ya presha

Nina changamoto ya presha

Naxria abdalla

Senior Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
178
Reaction score
311
Jaman habari zenu mimi nina changamoto ya presha na nimegundua kutokana na number zangu zinavyojieleza mara inapanda mara inashuka naitaji kuicontroll kabla haijaniletea shida kubwa zaidi iwe kwa dawa au kawaida,naomba kwa upole tu munibariki njia za kuicontroll,plz hii ni serious sana,apo chini daktar amenipa dawa je hizi dawa ndio zile ambazo natakiwa kutumia maisha yangu yote?
20260411_115119.jpg

Maoni ya Mdau
Kama ni presha inayotokana na mazingira ya muda mfupi kama vile msongo wa mawazo (stress) e.g. kazi nyingi mno, matatizo ya kifamilia, chakula, au ugonjwa, etc, presha hii ni ya muda tu na itarudi chini na utaendelea kama kawaida hata bila kutumia dawa.

Lakini kuna tatizo la presha ya kudumu, inayotokana hasa na umri mkubwa na figo kushindwa kufanya kazi vizuri, au matatizo mengine ya kibiologia, presha hii haitibiki na kuisha kwa kutumia dawa ulizopewa. Utatakiwa kutumia dawa hizo maisha yako yote. Usiogope kwani wengi hufanya hivyo. Zingatia matumizi ya dawa na epuka mambo yanayoweza kusababisha presha kupanda kama vile kula vyakula vyenye chumvi nyingi, mafuta mengi, epuka hasira, msongo wa mawazo, etc.
 
Jaman hbr zenu mm nina changamoto ya presha na nimegundua kutokana na number zangu zinavyojieleza mara inapanda mara inashuka naitaji kuicontroll kabla haijaniletea shida kubwa zaidi iwe kwa dawa au kawaida,naomba kwa upole tu munibariki njia za kuicontroll,plz hii ni serious sana,apo chini daktar amenipa dawa je hizi dawa ndio zile ambazo natakiwa kutumia maisha yangu yote?
View attachment 3570942
Kama ni presha inayotokana na mazingira ya muda mfupi kama vile msongo wa mawazo (stress) e.g. kazi nyingi mno, matatizo ya kifamilia, chakula, au ugonjwa, etc, presha hii ni ya muda tu na itarudi chini na utaendelea kama kawaida hata bila kutumia dawa.

Lakini kuna tatizo la presha ya kudumu, inayotokana hasa na umri mkubwa na figo kushindwa kufanya kazi vizuri, au matatizo mengine ya kibiologia, presha hii haitibiki na kuisha kwa kutumia dawa ulizopewa. Utatakiwa kutumia dawa hizo maisha yako yote. Usiogope kwani wengi hufanya hivyo. Zingatia matumizi ya dawa na epuka mambo yanayoweza kusababisha presha kupanda kama vile kula vyakula vyenye chumvi nyingi, mafuta mengi, epuka hasira, msongo wa mawazo, etc.
 
ni vizuri ukionana na daktari uso kwa uso, ili akuhoji apate taarifa kamili, kisha vifanyike vipimo, na kisha atapanga njia za kutibu au kuidhibiti hiyo presha.

I insist, ni muhimu sana kuonana na daktari.

Epuka dawa za kushauriwa na watu wasio madaktari, sio kila dawa ya presha ni kwa ajili ya kila mtu. 😎💊
 
ni vizuri ukionana na daktari uso kwa uso, ili akuhoji apate taarifa kamili, kisha vifanyike vipimo, na kisha atapanga njia za kutibu au kuithibiti hiyo presha.

I insist, ni muhimu sana kuonana na daktari.

Epuka dawa za kushauriwa na watu wasio madaktari, sio kila dawa ya presha ni kwa ajili ya kila mtu. 😎💊
Vipimo gani tena wakati ndio nimepima nipo na presha
 
Umenikumbusha enzi zile za kipindi cha Ze Comedy Show, Mpoki anamuigiza Capt. John Komba (RIP) akihemea juu juu (presha inapanda, presha inashuka).

Pole sana.
 
okay, trust your doctor.. tumia dawa, then rudi hospitali siku uliyopangiwa kurudi ili ifanyike assessment.
Kama bado matokeo hayaridhishi, ataadjust dosage, kubadili au kuongeza dawa nyingine..

Kukiwa na umuhimu wa rufaa, utapewa rufaa
 
Kama uko Mwanza au Kanda ya ziwa fanya mpango ukamwone Dr. Kataraiya, utapata ushauri mzuri na tiba nzuri sana!
 
Back
Top Bottom