Nimwambieje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimwambieje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nasema, Jul 16, 2012.

 1. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wadau wa MMU?Nilikuwa na boyfriend kwa miaka mitatu, tukaachana ktk hali ambayo iliniumiza sana moyo wangu, nikawachukia wanaume.Nikakaa kwa miaka miwili bila boyfriend. Sasa akatokea huyu kijana, akanipenda, kwa kuwa nilikuwa sitaki kuwa naye nikiogopa kuumizwa tena, nikamwambia nina mpenzi so aachane na mimi. Hakukata tamaa, akaendelea kunishawishi, hasa kwa kuwa tulikuwa tunaonana mara kwa mara - sehemu tunazofanyia kazi huwa tunaonana mara kwa mara na kwa kipindi cha kama miezi mitano nimekuwa nafanya naye kazi kwenye team moja ya consultancy.Nikajikuta naanza kumpenda, nikaanza naye uhusiano yeye akijua kuwa nina mpenzi na yeye ni kama anaiba tu. Sasa ndio nampenda mno na napenda niwe na mahusiano naye rasmi na serious. Sitaki kumpoteza. Tatizo ni je, namwambiaje kwamba nilimdanganya?Inakuwa vigumu kwangu kujua nianzaje kumwambia kwa sababu nilimjengea mazingira kuwa nina mpenzi serious, akawa haji au anaogopa kuja nyumbani kwangu; anajua hakika mwenyewe akirudi itakuwa balaa. Nilimdanganya BF wangu amehamia Mwanza na kwamba huwa naenda kumsalimia na yeye huja kwangu, nipo Dodoma kwa sasa. Ni kweli nilisafiri kwa private consultancy kwenda Mwanza mara mbili, na huyu boyfriend mpya aliamini kuwa naenda kwa mpenzi. Mimi huwa naenda nyumbani kwa huyu BF mpya bila tatizo lolote, na sasa baadhi ya watu wake wa karibu wameshanifahamu.Naomba ushari wenu, ipi ni namna nzuri ya kurekebisha makosa niliyofanya? Natanguliza shukrani.
   
 2. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,669
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Duuuuhh!!
  wanawake bwana...... Nasema,kwa techniques zile zile za kumuaminisha kuwa una mpenzi na akaamini unae,waweza vilevile kutumia techniques nyingine kum convert na akaamini ulikuwa unamdanganya ......

  Mytake: Hata kama jamaa atakuja kuamini kwamba yupo alone kwako,he will never trust you for 100% make atahisi bado kuna mambo mengine umeyaficha na ipo siku labda utayasema.......

  goodlucky...
  The Magnificient
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  si umwambie tu ulimdanganya lakini kwa sababu ulishawahi kuumizwa na ukaogopa kufanyiwa tena hivyo,kama ana akili he will understand,kama amepangiwa kuwa wako he will be yours,if not achana naye akiamua kusepa kisicho ridhiki hakiliki,,,
   
 4. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Umefanya kosa kubwa sana kukubali awe mpenzi wako (muongo halafu huna msimamo) huyo jamaa hakuamini 100% hata utakapo mueleza ukweli hata kuamini, pia atakuwa anaamini kwamba; kama uliweza kumsaliti mpenzi wako wa awali utashindwaje kumsaliti yeye? Siku nyingine ukitaka kukataa kitu/mtu siyo lazima kusema uongo, haulipi.
   
 5. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  taratibu usimshtukize..slow down again,make a wish.....maadam alikupenda na ww umempenda ni rahisi kukuelewa with time lakini......kaa chini ongea nae mambo mbalimbali ya mustakabali wako mf kuolewa..tell him you are wishing to be maried....,to have a family,raise ur kids..na u feel to be responsible and ready..then weka pending,...atakuuliza vp bf wako ana mpango gani na ww........apo ndo patamu...tell him haeleweki on that area na amebadilika sana kipindi umemtembelea........weka mazingira fulani yatakayoonyesha now ur free...kama kweli yupo serious atapropose utamjua maongezi yake.........some other time muulize anawaza nn kuhusu maisha?..msome vzuri with time .....usifanye gafla na wala usimwambie haukua na mtu kwa haraka............ila one day hukoooooooooo ujage kumwambia....atachekaje!!!..it hapened kwangu the same scenario
   
 6. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Magnificent, ndio maana naomba ushauri wenu ili nisipoteze trust kwake. Mkonowapaka wewe mwenzangu una kaexperience, asante sana, u can imagine how I feel now. Nitakupm kwa msaada zaidi.Bra-Joe, si kweli kwamba sina msimamo, but it happens sometimes especially ktk mapenzi.
   
 7. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  em tuma pm iyo spend upate tabu wakat maujanja yapo..........
   
 8. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kitu kingine ni kwamba, inaonekana inamuuma sana mimi kuwa na mpenzi mwingine! Maana mara kwa mara anamuulizia na kumtaja, "jamaa anakuja lini? mtaoana lini? mtazaa watoto wangapi? je mimi utaniacha? ikitokea ukapata mimba jamaa atakuua!" Naumia sana moyoni! Na nimeanza kupata woga!
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  vp kama naye atakuwa na mtu ambaye anamalengo naye na wewe alikuweka wa kupoozea tuuu kama ulivyomfanya yeye aamini hivyo??
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  uniambie hivyo labda nikukute bikra ila kama siyo unataka ugonvi wewe sita amini kabisaa sijui labda wanaume tunatofautiana!
   
 11. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Duh! Henge, naomba isiwe hivyo. Na nafikiri hana, coz nahisi angekuwa naye ingekuwa rahisi sana kwake kusema kuwa ana girl.
   
 12. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Shosti ukweli usiuseme kibustani kitaota mbawa,nenda nae pole pole mulize anakupenda kiasi gani na Yuko tayari kua na wewe hata ukimalizana na Huyo wa mwanzo yeye atakupokea kwa mikonoo miwili ? Jibu lake nimuhimu kupima umesimamia wapi.... Muombe mungu kwa sana Kama Ana kheir na wewe utampata...
   
 13. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asante kwa ushauri wako Promiseme. Nitautumia asali isiingie sisimizi!
   
 14. F

  FAMILY LAW Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole bibie usiogope mwambie ukweli kua huo ni mpango ulioupanga mahususi kwa kua ulishawahi kuumizwa na anza kumruhusu kuja kwako na wewe mtambulishe kwa jamaa zako mruhusu awe huru na wewe,, mpigie cm hata saa 8 ucku na kumwambia maneno matamu ya mahaba
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Dah!Mwambie tu kwani utakachomwambia sio kibaya.Nadhani atakuelewa!
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Kabla ujamwambia ukweli mpe kitu roho inapenda mpaka adate!

  Ukisha maliza kazi hiyo mwambie ukweli.
   
 17. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Iko dalili kubwa utazidi kutuchukia wanaume, safari sio kifo tutafika tu na kusikia kilio kingine.
   
 18. kapolo

  kapolo JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Usimwabie kama ulimdanganya,ila mtengenezee mazingira ya kumuonesha umeachana na huyo BF hewa...anza kumkaribisha kwako na mfanye awe huru,then unaeza kumwambia umeamua kuachana na yule BF hewa.
   
 19. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,669
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160

  Lazima imuume...lazima...
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  toka nae out,
  hang nae....
  Mfurahishe...
  Mchekeshe...

  Then mwambie......
  Kisha mfanye awe huru kuja kwako.....
  Hakikisha anakuja kwako......
   
Loading...