Nimuweke kundi gani??

Nimuweke kundi gani??

leoniamahela

Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
12
Reaction score
4
Mwenzenu nina mpenzi lakini nikaja kugundua nina mwenzangu ambae walikuwa wote kwa muda mrefu lakini huyu mwanaume anasema eti hampendi yule mwanamke. Sasa nifanyeje maana anadai nimpe muda wa kumuacha.

Nipeni ushauri je nimpe huo muda au niachane nae??
 
jiulize hivi wewe una nini cha kumzidi huyo mwenzio hivi kwamba adumu na wewe asikuache kumfuata mwingine?jiulize huyo mwenizo alipendwa mwanzoni hivyo hivyo upendavyo wewe lakini sa hivi anataka kuachwa wewe u nani usiachwe?huna mapungufu?we ni malaika hukosei?uko tayari kukosana na rafiki yako na pengine mmeshibana sana kwa ajili ya kijana huyo asiye na hekima?ukishatafakari hayo maswali nadhani utajua ni maamuzi yapi sahihi kwako,kila la kheri.
 
yaani naona hapa ushauri ameshaupata! Blue G una akili sana!
jiulize hivi wewe una nini cha kumzidi huyo mwenzio hivi kwamba adumu na wewe asikuache kumfuata mwingine?jiulize huyo mwenizo alipendwa mwanzoni hivyo hivyo upendavyo wewe lakini sa hivi anataka kuachwa wewe u nani usiachwe?huna mapungufu?we ni malaika hukosei?uko tayari kukosana na rafiki yako na pengine mmeshibana sana kwa ajili ya kijana huyo asiye na hekima?ukishatafakari hayo maswali nadhani utajua ni maamuzi yapi sahihi kwako,kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:
KWI KWI KWI jf bana huyo anataka umpe muda ili nini?............. agegede lwa mwishomwisho? kwa mtazamo wangu naona huyo ni msanii wa mapenzi. siku zote mlikuwa pamoja na alikuwa naye mbona hakumuacha ili abaki na wewe? madam serious walk away while you can.
 
Mwenzenu nina mpenzi lakini nikaja kugundua nina mwenzangu ambae walikuwa wote kwa muda mrefu lakini huyu mwanaume anasema eti hampendi yule mwanamke. Sasa nifanyeje maana anadai nimpe muda wa kumuacha.

Nipeni ushauri je nimpe huo muda au niachane nae??

yaani ni rahisi sana ni sawa na kufiwa na mtoto wako unaempenda unalia siku ya kwanza na ya pili ya tatu unaona kawaida tu.. malovee ni hatari tupu..

#Via_Mapenzi_Ya_Sasa
 
Mwenzenu nina mpenzi lakini nikaja kugundua nina mwenzangu ambae walikuwa wote kwa muda mrefu lakini huyu mwanaume anasema eti hampendi yule mwanamke. Sasa nifanyeje maana anadai nimpe muda wa kumuacha.

Ha ha ha!!!

Kuna watu sijui mna akili za kuazima, sasa hujajiuliza kama hampendi kwa nini ndani ya huo muda wote mrefu walikuwa wote???

Ushafanywa msukule hapo, kama una mpango wa kuendelea kula wa chuya na pumba basi endelee kujiegesha tu hapo ukisubiri akili zikurudie.
 
Mmm shosti moyo wako unakubali hayo ulia abiwa usubiri kama mpaka amalizane na wenzio? ivi umeshajiuliza mpaka hapo cheo chako kwa huyo bwana ni kipi? kwani yeye anambili au ana moja kama biladamu wengine mpaka akujibu maneno hayo?
ivi ni pesa zake michezo yake uzuri au nini mpaka unakua mtumwa wa penzi lake eti mpaka amalizane na huyo yani hapo inabidi umsubirie mwenzio,au uliambiwa yuko hukuambiwa WAPO?
 
kha! Kwani we ulikuwa wa bahati mbaya?? Kwa taarifa yako kumuacha huyo wazamani ni ndoto. chagua kuwa lover B ama kuchapa lapa.
 
Si amekuambia uumpe muda, sasa unataka sisi tufanyaje?? Au tuupunguze??
 
Ushakuwa spea tairi jombaaaa... Run for your life
 
Mwenzenu nina mpenzi lakini nikaja kugundua nina mwenzangu ambae walikuwa wote kwa muda mrefu lakini huyu mwanaume anasema eti hampendi yule mwanamke. Sasa nifanyeje maana anadai nimpe muda wa kumuacha.

Nipeni ushauri je nimpe huo muda au niachane nae??

Mwambie akishakuacha akuambie na wewe ufanye mpango wakuwaacha hao wako wa zamani...
 
Back
Top Bottom