Nimuonavyo Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimuonavyo Dr Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Oct 11, 2010.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Binafsi namuona Dr. Slaa kama mtu maarufu zaidi kwenye Kampeni za uchaguzi wa Mwaka huu. Lakini kwa upande wa Pili namuona kama Daudi kwenye simulizi za Biblia aliyemshinda Goliathi, Daudi alikuwa na Kombeo na Jiwe hata akamshinda Goliathi.

  Dr. Slaa tayari analo Kombeo (umaarufu wake binafsi) lakini sijui kama jiwe (Chama) atakalotumia kuumuulia Goliathi (CCM) ni imara kiasi cha kuweza kumuua shujaa huyo aliyepigana vita vingi na kushinda.

  Isije ikawa jiwe analotaka kulitumia 31/10/2010 ni udongo ulifinyangwa na kuanikwa juani likikutana na matone (kashikashi za uchaguzi) kidogo ya mvua linamong'onyoka.
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "The ballot box is the surest arbiter of disputes among free men."
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  unamashaka na Dr SLAA, unamashaka na CHADEMA. USIOGOPE, TUPE KURA YAKO UONE INAVYOLIPA, HATUTAKUANGUSHA. Tupo tayari kuwatumika waTz woote bila kujali, kabila, dini na ukanda. Chagua CHADEMA KWA MAENDELEO YA TANZANIA.
  [​IMG]
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Silaha kubwa siyo chama ni nguvu ya umma iliyopo nyuma yake. Watu wamechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  tunaomba kura yako, tunaihitaji sana
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumchagua Mchungaji Slaa ni kuisalit nchi, hizi article zinaonyesha wazi nchi itaendeshwa kibibilia sio kiutaalam wa kisiasa na uchumi, hasa ukizingatia mchungaji kasomea na kuandika assignment kuhusu bibilia ambayo watanzania hawatofaidika kabisa na hiyo bibilia

  Na ndi ata mchungaji Slaa kaamua kuachana na bible na kufuata ngono na ulaji kwenye siasa, mchungaji Slaa kavunja miko yote ya Upadri kama vile kuowa na kuacha pia kuowa tena mke wa mtu

  Hii inaonyesha wazi huyu mchungaji si wa kuamini, kote aliko ingia kaamua kutoka, alikuwa kada mkubwa wa ccm kabla ya kukimbia kanisa, huyu ni msaliti asieaminika!!!
   
 7. P

  PWAGU Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ushindi wa safari hii kwa ccm utakuwa wa kishindo kushinda chaguzi zote,kwani wajinga wachache kwa udini wao na umbumbu wao wa kutoelewa siasa inahitaji nini wameamua kuisaidia ccm kwa kueneza udini wao makanisani as if nchi hii ni ya wakiristo pekee.
  Haya tutaona kama hizo kura chache za baadhi ya wagalatia zitamfikisha kokote padre wenu huyo.muslims ni zaidi ya nusu ya wapiga kura na kwa udini huo hakuna kura ya muislamu atakayoipata.......
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "If you don't say anything, you won't be called on to repeat it."
   
 9. k

  kisoti Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumekugundua. Shindwa na udini wako!Na ukiendelea, tutawaomba MODS wa ku- bann

   
 10. R

  RMA JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :llama:Karibu Rais wetu Dr Slaa! :tonguez: :smow:  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!:blah::smow:


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..:tonguez::preggers:


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? :A S 13::blah:


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious! :A S 112::moony:


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!:tonguez::A S 13:


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.


  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya. :blah::moony:


  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..:llama::smow:
  [FONT=Book Antiqua, serif]Kila la heri: mak.ralph@yahoo.com[/FONT]
   
Loading...